Showing posts with label H/KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label H/KIMATAIFA. Show all posts

2015-04-10

Huyu Ndo Mtanzania Anayetuhumiwa Kwa Ugaidi Kenya.....Jana Alifikishwa Mahakamani Chini Ya Ulinzi Mkali


Mtanzania anayedaiwa kuhusika katika shambulizi la kigaidi lililoua watu 148 katika Chuo Kikuu cha Garissa – Kenya, Rashid Charles Mberesero, jana alifikishwa mahakamani na kuwekwa kizuizini kwa mwezi mmoja wakati polisi wakiendelea kukusanya ushahidi dhidi yake.

Mtuhumiwa huyo ambaye pia anafahamika kwa jina la Rehani Dida alirejeshwa Nairobi kutoka Garissa alikopelekwa awali kwa ajili ya kuhojiwa baada ya kukiri kujihusisha na kundi la Al- Shabaab.

Mahakama jijini Nairobi ilisema jana kuwa mtuhumiwa huyo ambaye hakutakiwa kujibu tuhuma hizo na wenzake wanne watalazimika kuwa chini ya uchunguzi mkali wa polisi kwa kipindi cha mwezi mmoja na baadaye wanaweza kusomewa mashtaka ya kuhusika katika shambulizi hilo lililoua watu hao, wengi wao wakiwa ni wanafunzi.

Haikufahamika mara moja sababu za kuamuliwa kuwekwa kizuizini kwa muda huo mbali ya taarifa kueleza kuwa ‘watashikiliwa na polisi tena katika kituo cha siri’.

Mwendesha Mashtaka, Daniel Karuri aliiambia Mahakama hiyo kuwa Mtanzania huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tano, alikuwa amepanga safari ya kuelekea Somalia kwa ajili ya kujiunga na makundi ya kigaidi.

Watuhumiwa hao ni kati ya 14 waliotiwa mbaroni hivi karibuni baada ya shambulizi hilo la kigaidi.

Mahakama hiyo pia imewaamuru washukiwa wengine kuendelea kushikiliwa na polisi kwa muda wa siku tano hadi 15.

Awali, Karuri aliiambia Mahakama hiyo kuwa polisi walikuwa wakifuatilia kwa karibu uhusiano baina ya wale waliofanya shambulizi hilo na mfanyabiashara mmoja anayemiliki hoteli mjini Garissa. Inasemekana kuwa watu waliotekeleza shambulio hilo walikuwa wamelala katika hoteli hiyo.

Hakula chakula cha shule
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kigwe, mkoani Dodoma alipokuwa akisema Mberesero baada ya kufaulu kutoka Gonja, wamesema hakuwahi kula chakula chochote shuleni kwa kipindi cha mwezi mmoja aliokaa akisubiri kuhamishwa na kubadilishiwa mchepuo wa masomo.

Wakizungumza na mwandishi wetu shuleni hapo jana, wanafunzi wa kidato cha tano, Yoram James na Thomas Godwin, walisema siku zote alizoishi shuleni hapo alikuwa akila kwa mama lishe jirani na shule hiyo.

“Lakini alikuwa na mkarimu kwetu wakati mwingine alikuwa akitununulia maandazi ya kunywea chai,” alisema Yoram.

Hata hivyo, walisema kutokana na upole wake, jinsi anavyoongea na kutumia muda mrefu msikitini, walimpa jina la Ustaadhi.

“Alikuwa akienda mjini mara kwa mara, nadhani alikuwa akiomba ruhusa kwa walimu au alikuwa akitoroka,” alisema Thomas.

Thomas alisema Rashid alikuwa akipenda kucheza mpira wa miguu kwa hiyo alitenga muda wake kwa ajili hiyo.

Uhamisho wake
Mkuu wa Shule hiyo, Ramadhan Bakari alisema ofisi ya elimu mkoa ilituma taarifa ya kuwataka wanafunzi wanaopenda kubadilisha mchepuo kuandika barua ya maombi.

“Rashid alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi watano walioomba kubadilishiwa mchepuo kutoka Sanaa kwenda Sayansi, walikubaliwa wanne akiwamo yeye,” alisema Bakari.

Hata hivyo, mwalimu huyo alisema Rashid alikuwa akihangaika ahamishiwe Shule ya Sekondari ya Bihawana, tangu aliporipoti Kigwe.

“Hatuwezi kuzungumza kuhusu tabia zake maana hapa hakuishi siku nyingi, alikuwa kama yuko njiani,” alisema.

“Aliondoka hapa shuleni kwenda Bihawana Agosti 19, mwaka jana baada ya taratibu kukamilika,” alisema.

Uvumi wasambazwa
Hofu imetanda katika maeneo mbalimbali baada ya kusambazwa ujumbe kwenye simu na mitandao ya kijamii ukidaiwa kutolewa na Umoja wa Mataifa (UN) kutahadharisha watumishi wake waepuke kukaa katika makundi makubwa na mikusanyiko katika majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha leo kuepuka mashambulizi ya kigaidi.

Hata hivyo, Msemaji wa UN, Usiah Ledama alikanusha umoja huo kuhusika na ujumbe huo akisema ni feki na hauna ukweli wowote.

Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, Diwani Athumani alisema hata kama ujumbe huo ni feki, bado Jeshi la Polisi linachukua tahadhari kuhakikisha Taifa linakuwa salama.

“Huo ujumbe uwe feki au wa kweli, lazima tuchukue tahadhari, Tanzania si kisiwa, tutakuwa salama kwa asilimia 100, kwa hiyo ulinzi unaimarishwa,” alisema.

Alisema ni lazima kila mtu awe mlinzi wa mwenzake na ahakikishe kuwa anakuwa mzalendo kwa kutoa taarifa zozote ambazo anadhani zitalisaidia Jeshi la Polisi katika ulinzi.

2015-04-09

MTANZANIA ALIYEKAMATWA KWA SHAMBULIO LA GARRISA KUPANDISHWA KIZIMBANI LEO

Mtanzania aliyekamatwa Kenya akishukiwa kuhusika na shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa wiki iliyopita Rashid Charles Mberesero.

Mtanzania aliyekamatwa Kenya akishukiwa kuhusika na shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa wiki iliyopita lililosababisha vifo vya watu takribani 150 na wengine wengi kuachwa majeruhi, Rashid Charles Mberesero mwenye umri wa miaka 20 ni mwanafunzi wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Bihawana Dodoma, lakini uongozi wa shule hiyo umesema kuwa, Rashid alitoweka shuleni hapo tangu Desemba mwaka jana. 

Habari zilizothibitishwa na wazazi wake ni kwamba mwanafunzi huyo anasoma katika Shule ya Sekondari ya Bihawana, Dodoma, baada ya kufaulu katika Shule ya Sekondari Gonja mkoani Kilimanjaro. 

Taarifa hizo zimekuja wakati Mberesero maarufu kwa jina la Rehani Dida, akitarajiwa kufikishwa mahakamani leo jijini Nairobi baada ya watuhumiwa wengine kufikishwa mahakamani juzi.

GPL

2015-04-08

HIVI NDIVYO AL-SHABAB WALIVYO WAFANYA WANAFUNZI WA KIKE KABLA YA KUWAUA.......bofya kuona video

A survivor of the deadly terror attack in Garissa University has told the media how the Al Shabaab tricked female students to draw them out in the open and kill them like insects.

Narrating his story, Francis Gicobi, a second year Bachelor of Education student, said many female students fell for Al Shabaab’s lies and that’s why they were killed in large numbers compared to male students. 

Gicobi noted that when Al Shabaab stormed the women’s hostel, they tricked them to comply with their orders to come out because they would not be killed since Islam does not permit them to kill women.

Many females students fell for this lie and came out and the Al Shabaab sprayed them with bullets indiscriminately killing them like insects

The Al-Shabaab shouted

“Kama hamtaki kufa, tokeni hapa nje nyote kwani kulingana na dini yetu, hatuui wasichana na kwa hivyo mtoke taratibu kwa gorofa hadi hapa chini, au mpigie baba zenu simu waje wakuokoe. (If you don’t want to die, come outside. According to our religion, we do not kill girls. Walk down the stairs to the ground level, or alternatively call your fathers to come and save you),” narrated Gicobi. 


“Female students walked to the ground floor of the storied building in droves only for the attackers to indiscriminately spray them with bullets,” he added.

However, he thanked God for keeping him alive to tell Kenyans what he witnessed on that fateful day.

“I thank God for saving me to be able to tell Kenyans what I witnessed as my innocent colleagues were riddled with bullets like animals,’’ he said.

HUYU NDIO MTU ANAYEJIGAMBA KUWA YEYE NI ‘MUNGU' KENYA


Je, umewahi kusikia mtu anajiita Mungu na ni binadamu wa kawaida na wafuasi wake wanaamini kuwa yeye ndiye muumba wao? Yuko magharibi mwa Kenya anajiita Jehova Wanyonyi na anadai kuwa yeye ndiye Mungu.
 Paul nabiswa alimtembelea kwake katika kijiji cha Chemororoch kilomita hamsini kutoka mji wa Eldoret na kuthibitisha hilo. 


2015-04-07

KABURI MOJA WALIMOZIKWA WATU 425 LAGUNDULIKA KINSHASA-DRC

                                       Mji wa Kinshasa-DRC.

Vyombo vya habari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, vimeripoti kuwa, kaburi kaburi la umati ambamo kulizikwa mamia ya watu limegundulika karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa. 

Waziri wa Mambo ya Ndani wa DRC, Evariste Boshab Mabudj

Kanali wa RTBFTV wa Kongo ametangaza kuwa, zaidi ya watu 425 walizikwa pamoja ndani ya kaburi hilo. Hata hivyo vyombo vya habari vina shaka juu ya namna ambavyo mauaji hayo yalivyofanyika na ni nani muhusika wake. 


Baadhi wananchi wanasema kuwa, mauaji dhidi ya watu hao yalitokea wakati wa machafuko ya mwezi Januari mwaka huu, huku wengine wakisema kuwa, mamia hao walifia hospitali.

Kaburi hilo limegunduliwa katika eneo la mji wa Maluka, katika viunga vya mji wa Kinshasa baada ya malalamiko ya wakazi wa eneo hilo kushindwa kuvumilia harufu kali iliyokuwa ikitokea eneo la kaburi hilo, hivyo kuamua kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na serikali ya nchi hyo.

Baadhi ya duru zimethibitisha kuwa wahanga hao waliuawa katika machafuko ya tarehe 19-21 mwezi Januari, wakati wa maandamano ya kupinga njama za serikali kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo kwa lengo la kumbakisha zaidi madarakani Rais Joseph Kabila.

Hata hivyo Evariste Boshab Mabudj, Waziri wa Mambo ya Ndani wa DRC alipotakiwa kuzungumzia suala hilo amekanusha madai hayo na kusema kuwa, wahanga hao walipoteza maisha kwa maradhi hospitalini.



GPL

Jeshi la Kenya Lafanya Shambulio Somalia Kulipiza Kisasi Baada ya Al Shabaab Kuuwa Wanafuzi 148 Kenya


Ndege za kijeshi za Kenya zimeshambulia maeneo ya wapiganaji wa kundi la Alshabaab katika taifa jirani la Somalia .

Ndege hizo zililenga maeneo mawili ya jimbo la Gedo,linalotumiwa na wapiganaji hao kuvuka na kuingia Kenya, msemaji huyo ameongeza. 

Maeneo hayo mawili hutumiwa na wapiganaji hao kupanga mshambulizi nchini Kenya.

Wanajeshi wa AMISOM walitarajiwa kupeleka wanajeshi wao katika eneo hilo la Gedo lakini hadi sasa hawajafanya hivyo.

Hili ni shambulio la kwanza la Kenya kwa shambulizi la alshabaab ambalo lilisababisha mauaji ya watu 148 katika chuo kikuu cha Garissa wiki iliopita. 

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapa kujibu shambulizi hilo kwa njia mbaya zaidi.

Msemaji wa jeshi la Kenya David Obonyo amesema kwamba Jeshi la Kenya lilijibu vitisho kwa kutekeleza mashambulizi ya angani siku ya jumapili usiku katika eneo hilo.

Hakuna maelezo zaidi ya oparesheni hiyo yaliotolewa.

RAPPA THE GAME ASHTAKIWA KWA KUMPIGA KONDE POLISI

                                                         Rappa The Game.

RAPPA wa Marekani, Jayceon Terrell Taylor maarufu kwa jina la The Game ameshtakiwa kwa kumpiga polisi aliyedai kusababishiwa maumivu katika ubongo.

The Game alimpiga konde askari polisi wakati wakifanya mazoezi ya mchezo wa kikapu Machi 29, mwaka huu katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Hollywood jijini Los Angeles, Marekani.

Askari huyo aitwaye, Onyebuchi Awaji ambaye hakuwa zamu siku hiyo ameeleza kuwa hakuchochea chochote kilichopelekea achapwe konde hilo japo The Game amesema alifanya hivyo kujihami baada ya askari huyo kumtishia kwa bastola. 



Wapambe wa The Game wameeleza kuwa rappa huyo aliamua kujihami baada ya Awaji kumtishia kuwa angeenda kwenye begi lake kuchukua bastola baada ya kutokea sintofahamu baina yao.

Awaji anayedai kusababishiwa maumivi katika ubongo alieleza kuwa baada ya Game kumpiga alitokomea kutoka eneo hilo mara baada ya kusikia polisi wakiitwa. 

GPL

2015-03-31

Watengeneza printa ya aina yake Afrika Mashariki



  Meneja wa Maabara ya Buni Hub Jacquline Dismas akieleza namna printa ya 3D inavyofanya kazi hivi karibuni.Picha na Nuzulack Dausen.
Na Nuzulack Dausen

Huenda isiwe inafahamika na Watanzania wengi, lakini mashine ya kwanza ya kuchapa vifaa vya maumbo mbalimbali, imeanza kutengenezwa nchini.

Kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki na Kati, Printa inayochapa kitu katika pande tatu maarufu kwa kiingereza kama ‘3D Printer’, imetengenezwa jijini Dar es Salaam katika kituo cha kukuza ubunifu na ujasiriamali cha Buni Hub.


Printa hiyo, yenye uwezo wa kutengeneza vifaa mbalimbali vya plastiki kutokana na usanifu wake, ilitengenezwa na timu ya wataalamu wa elektroniki na teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) baada ya kupatiwa ujuzi na mtaalamu kutoka Uingereza, Mathew Rogge.


Kwa wengi waliozoea printa za kuchapa karatasi watashangazwa na uwezo mkubwa wa printa hiyo inavyoweza kuuchapa mchoro uliopo kwenye kompyuta hadi kuwa kifaa pasina kukosea.


Baada ya wiki tatu za kuitengeneza, printa hiyo imeshatengeneza vifaa kadhaa vya plastiki vinavyoweza kutumika kama vipuri kutengenezea mashine nyingine ya namna hiyo.


“Mashine hii tulioitengeneza kwa kutumia mabaki ya vifaa vya elektroniki, inaweza kutengeneza vitu unavyoweza kuvishika na kuvitumia katika kazi mbalimbali kama vikombe, midori, sampuli za nyumba, viatu na vinginevyo,” anasema Meneja wa maabara ya Buni Hub, Jacqueline Dismas.


“Tunajaribu kwa hali na mali kuhakikisha mazingira yetu ni safi kwa kupunguza taka ambazo zinaweza ama kutumika tena au kutengenezwa upya.”


Ili kupata vifaa vya kuundia mashine hiyo, anasema iliwahitaji kuzunguka kwenye vituo vya kukusanya taka za kielektroniki kama printa, kompyuta na televisheni vilivyopo jijini hapa.


Matumizi ya taka hizo, zinazosaidia kupatikana kwa mota, chanzo cha nishati ya umeme (power supply) na reli za kujengea printa, yanasaidia kupunguza tatizo la taka ngumu na kujenga tabia ya kutunza mazingira.


Tofauti na printa zinazochapa karatasi ambazo hutumia wino kuchapa, printa za 3D zinatumia malighafi za plastiki, chuma, udongo, na nyinginezo ziitwazo ‘filament’ kuzalisha bidhaa tofauti kutokana na mahitaji.


Kuingia kwa teknolojia ya uundaji printa za 3D hasa kwa kutumia taka za kielektroniki, kutapunguza gharama za ununuzi wa mashine hizo zilizoanza kupata umaarufu ulimwenguni kwa kurahisisha kazi lukuki ambazo awali zilifanyika kiwandani.

2015-03-26

Sad Newzzzzzzzzzzzz:NI AJALI YA NDEGE ILIYOSABABISHWA BAADA YA RUBANI KUFUNGIWA NJE.

Ndege ya Germanwings ilipokuwa ikisafiri katika anga la Duesseldorf nchini Germany mwaka 2014.

Ndege ya shirika la Germanwings, Airbus yenye namba A320 na namba ya safari 4U 9525 iliyokuwa ikitoka Barcelona nchini Hispania kwenda Duesseldorf nchini Ujerumani ilianguka kutoka angani mpaka chini ya aridhi kwa muda wa dakika 8 umbali wa futi 38,000 katika milima ya Alps iliyopo nchini Ufaransa.

Mkurugenzi wa shirika la ndege la Germanwings, Thomas Winkelmann amesema wasafiri 72 kati ya 144 walikuwa raia wa Ujerumani. Wahanga wengine walikuwa ni wanafunzi 16. Wakati huo nchi ya Hispania ikisema watu 51 walikuwa ni raia wa nchini humo. Katibu wa UK Foreign, Philip Hammond amehakikisha kuwa watu 3 walikuwa ni Waingereza.

wengine walikuwa ni kutoka nchi za Australia, Argentina, Iran, Venezuela, Marekani, Uholanzi, Colombia, Mexico, Japan, Denmark na Israel. 

Ramani ikionesha eneo la ajali ya ndege ya Ujerumani

Uchunguzi wa awali wa sauti zilizokuwa ndani ya kifaa cha kurekodia sauti ya ndege iliyoanguka Ufaransa unaonesha kuwa moja wa marubani wa ndege hiyo alikuwa amefungiwa nje ya eneo la marubani wakati ndege hiyo ilipoanguka.

Aidha haijabainika kikamilifu alikuwa ameondoka kufanya nini lakini sauti zinasikika akibisha kwa nguvu akitaka ufunguliwe mlango.

Milima ya Alps, eneo ambalo ajali ya ndege ilitokea.

Duru za kuaminika zinanukuliwa na jarida la New York Times.

Mkuu wa shirika la ndege la Lufthansa amesema kwa kinywa wazi kuwa kuanguka kwa ndege hiyo kuna hila hila.

''Hakuna maelezo kamili ya kiini cha ajali hiyo ''

''Ndege hiyo ilikuwa imefanyiwa ukarabati majuzi tu wala haikuwa na hitilafu yeyote''. 

Ajali ya ya ndege ya Germanwings ilivyotokea.

Wakaguzi wa kifaransa wamesema wamefanikiwa kukipata kifaa cha kurekodia sauti na maneno kutoka katika kisanduku cheusi cha ndege ya shirika la ndege la ujerumani iliyopata ajali katika milima ya Alps.

Wakaguzi hao mpaka sasa wanaendelea kukitafuta kisanduku kingine ,ambacho hurekodi taarifa za ndege hiyo na chanzo cha ajali hiyo .

Wanafunzi katika shule ya Haltern-am-See nchini Ujerumani wakilia baada ya wenzao kupata ajali kwenye ndege ya Germanwing.

Timu hiyo ya uokozi iliyoko katika eneo la ajali lililoko upande wa Kusini mwa Ufaransa wamefanikiwa kukipata kifaa hicho kinachohifadhiwa katika chumba cha rubani kikiwa kimeharibika.

David Gleave ni mkaguzi wa zamani wa ajali za ndege ,anasema kwamba visanduku hivyo vinapaswa kuwa na picha dhahiri za nini kilichotokea.

Waokoaji wakijadiliana katika eneo la ajali ya ndege hiyo.

Pengine tunaweza kupata mawasiliano ya timu ya wafanya kazi wa ndege hiyo,ambayo yatatuelekeza katika kilichojiri na chanzo cha tatizo ambalo walijaribu kulitatua pamoja kama timu, na hatua walizochukua kunusuru janga hilo.

Je rubani alichukua juhudi za makusudi kuwanusuru abiria na wafanyakazi waliokuwemo,na rubani mwingine aliendelea kurusha ndege?

Ama kutatua tatizo?na namna walivyohakiki na nini walichokiacha na mambo kama hayo.

Hata hivyo tunahitaji zaidi taarifa za kinasa taarifa ili tuweze kupata mustakabali kamili wa kile kilichotokea.

Akizungumza katika mkutano na waandishi habari Carsten Spohr ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege la Germanwings shirika dada la kampuni ya usafirishaji ya Lufthansa ameielezea ajali hiyo kuwa isiyoeleweka. 'Niamini baada ya miaka ishirini ijayo katika tasnia hii nami niliwahi kuwa rubani wa shirika la ndege la Lufthansa, bado hainiingii akilini juu ya kile kilichotokea jana'.

Shirika la ndege la Lufthansa halijawahi kupoteza ndege yake katika historia yake ya usafirishaji katika mazingira kama hayo, bado hatuelewi nini kiliisibu ndege iliyokuwa katika hali nzuri kiufundi na marubani wawili waliobobea katika kazi yao na waliopitia mafunzo ya hali ya juu ya safari za anga wa shirika la Lufthansa, kuhusika katika ajali mbaya kiasi kile. 
 
 GPL

2015-03-25

MAREKANI YAFANYA MAJARIBIO YA KOMBORA LA BALESTIKI

                                Kombora la Balestiki.

JESHI la Anga la Marekani limetangaza kuwa limefanyia majaribio kombora la Balestiki linaloweza kuvuka mabara na kwamba majaribio hayo ni ujumbe kwa walimwengu kuhusu uwezo wa silaha za nyuklia wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Anga la Marekani, kombora la Minuteman-III lilifanyiwa majaribio mapema Jumatatu katika kituo cha Jeshi la Anga cha Vandenberg huko California. Taarifa ya Jeshi la Anga la Marekani imesema: Majaribio hayo ya kombola la balestiki la nyuklia yanaonesha picha ya wazi kwa walimwengu kuhusu uwezo wa kombora ya Minuteman-III ambalo linaweza kulenga mahala popote.


                         Kombora la Balestiki linavyolipuka.

Kwa kutilia maanani kwamba Jeshi la Anga la Marekani haliwezi kutumia makombora ya Peace Keeper kwa mujibu wa makubaliano ya silaha ya START II (Strategic Arms Reduction Treaty), kombora la Minuteman-III litakuwa kombora pekee la balestiki linaloweza kuvuka mabara la jeshi la Marekani. Kombora hilo linavishwa kichwa cha silaha ya nyuklia aina ya W87 ambacho kina uwezo mkubwa wa uharibifu. Majaribio hayo yamefanyika sambamba na mazoezi ya kijeshi yanayoendelea kufanywa na majeshi ya shirika la NATO huko Ulaya mashariki.

Inaonekana kuwa kwa majaribio ya kombora hilo la nyuklia, jeshi la Anga la Marekani linafuatilia malengo kadhaa.

Kwanza ni kuwa Marekani inataka kuonesha misuli na uwezo wake wa silaha za nyuklia kwa wapinzani wake wakubwa hususan Russia. Katika kipindi cha miaka kama miwili iliyopita jeshi la Russia limefanya majaribio mtawalia ya makombora yanayoweza kuvuka mabara (Intercontinental Ballistic Missile au IBM) na hata kurusha makombora kama hayo kwa kutumia nyambizi. Kwa msingi huo Marekani ilikuwa ikinyemelea fursa ya kukabiliana na majaribio hayo ya silaha za nyuklia ya Russia.

Suala la pili ni kushadidi mivutano baina ya Russia na NATO huko Ulaya Mashariki ambako kumezifanya pande hizi mbili zijizatiti kwa silaha na majeshi katika eneo hilo na katika Bahari Nyeusi. Kwa msingi huo Marekani inataka kumuonesha adui wake yaani Russia, kwamba iwapo mgogoro huo utaendelea inaweza kutumia silaha zake za nyuklia.

Marekani ni miongoni mwa wamiliki wakubwa zaidi wa silaha za nyuklia duniani na ndiyo nchi pekee ambayo hadi sasa imetumia silaha hizo kuua watu wa taifa jingine. Nchi hiyo kinyume na ahadi zake za kupunguza maghala yake ya silaha za nyuklia, ingali inastawisha na kupanua zaidi silaha hizo na kuzifanyia majaribio.

Marekani pia inasasisha na kuziboresha zaidi silaha zake za zamani za nyuklia licha ya harakati za kimataifa za kupunguza silaha hizo husuan mkataba wa NPT unaosisitiza kupunguzwa na hatimaye kuangamizwa kabisa silaha hizo. Katika uwanja huo Washington imetenga bajeti ya dola bilioni 355 ambazo zitatumika kusasisha na kuboresha mitambo yake ya silaha na kuinua juu kiwango cha majaribio ya silaha za nyuklia. Vilevile Marekani imechukua hatua za kuboresha silaha na maghala yake ya zana za nyuklia barani Ulaya yakiwemo mabomu ya nyuklia ya B-61.

Kwa utaratibu huo, Washington, kinyume na mikataba ya kimataifa ya kuzuia uzalishaji wa silaha za nyuklia, inaendelea kuzalisha na kufanyia majaribio silaha za aina hiyo, suala ambalo linakiuka mkataba wa NPT. 





GPL

2015-03-24

Angelina Jolie akatwa nyumba ya uzazi


Angelina Jolie amelazimika kutoa mishipa ya kupitisha mayai na vifuko vya mayai ilikupunguza hatari ya kuathirika na saratani

Muigizaji Angelina Jolie amelazimika kutoa mishipa ya kupitisha mayai na vifuko vya mayai baada ya uchunguzi kuonesha kuwa alikuwa katika hatari ya kuathirika na saratani ya nyumba ya uzazi.

Muigizaji huyo maarufu wa Hollywood ameidokezea jarida la New York Times, kuwa alilazimika kutoa uzazi wake juma lililopita katika upasuaji wa dharura.

''Upasuaji huo ulitokana na ripoti ya uchunguzi wa daktari uliobaini kuwa nilikuwa na asilimia 50 ya chembechembe zenye hatari ya kuambukizwa saratani'' alisema Bi Jolie

Habari hizi zimewashtua wafuasi na mashabiki wa totoshoo huyo ambaye miaka miwli tuy iliyopita alilazimika kukatwa matiti kwa sababu ya tishio hilohilo la Saratani.

Aidha mamake muigizaji huyo nyota aliaga dunia kufuatia hitilafu iliyotokana na matibabu ya saratani.

''Sio jambo rahisi sana kukabiliana na swala hili gumu linalohusu afya yangu'' alisema Jolie.

Jolie ambaye ni mkewe muigizaji nyota wa Holywood ctor Brad Pitt, anasema kuwa vipimo vilionesha chembechembe za maradhi hayo na ikamlazimu kuchukua hatua hiyo mara moja.

Wawili hao wanawatoto sita.

Mamake tayari aliaga dunia kutokana na Saratani

''Nilimpigia simu akiwa Ufaransa na akarejea nyumbani mara moja ,lakini cha msingi ni kuwa ukikabiliwa na masaibu kama haya ya kiafya na uwe una mtu anayeweza kukusaidia kwa kukuchangia mawazo mzigo unakuwa mwepesi zaidi''

''Mamangu aligunduliwa kuwa na saratani akiwa na umri wa miaka 49 hivi sasa nina miaka 39 ''


''Licha ya hayo hivi sasa nimeshakoma kuzaa kwa hivyo ninatarajia mabadiliko mengi katika mwili wangu .Hivi sasa sina hamu ya kupata watoto wengine ,alisema jolie.

“Nitastahimili kwa njia ileile ambayo nafikiri maelfu ya wanawake wamepitia''

''Nilijiambia mwenyewe ni lazima nijikaze na kuwa na nguvu maanake sikuwa na sababu ya kujifikiria mimi bila kuona watoto wangu wakijuta na kusema looo! mamangu alikufa kutokana na saratani ya nyumba ya uzazi'' alisema bi Jolie.

Tunisia:Makavazi yafunguliwa leo


Hapo jana waziri mkuu wa taifa hilo aliwalaumu maafisa wakuu wa idara za usalama kwa kuzembea kazini

Makavazi ya Bardo nchini Tunisia, yanafunguliwa tena leo Jumanne, juma moja pekee baada ya magaidi kushambulia watalii wa kigeni na kuwauwa 20 kati yao.

Kutakuwa na mkutano wa hadhara kabla ya kufunguliwa tena kwa makavazi hayo ya kitaifa.

Wasanii watawatumbuiza wageni nje ya ukumbi huo unaopendwa na watalii wengi kutoka magharibi kabla ya maafisa kutoa taarifa inayolenga kuthibitisha kuwa magaidi hawataamua maisha ya wenyeji yasalie kuwa ya hofu.

Tangu tukio hilo kumekuwa na hofu kuwa magaidi hao huenda wameangamiza sekta nzima ya utalii ambayo ni kitega uchumi kikubwa cha Tunisia.


Hapo jana waziri mkuu wa taifa hilo aliwalaumu maafisa wakuu wa idara za usalama kwa kuzembea kazini .

Sita kati yao walitupwa nje.


Maafisa wa usalama wakishika doria nje ya makavazi hayo ya kitaifa

Waziri huyo mkuu , Habib Essid alisema mikakati imewekwa ilikuimarisha uwezo wa maafisa wa usalama kushirikiana na vitengo vya kijasusi kuzuia mashambulizi zaidi siku za usoni.

Jumba hilo linashehena kubwa zaidi ya sanamu za enzi za warumi.

Wavamizi wawili kati ya watatu waliotekeleza shambulizi hilo walipigwa risasi na kuuawa huku yule aliyesalia akisakwa na maafisa wa kitengo maalum cha kupambana na ugaidi.

Tukio hilo ndilo kubwa zaidi kuwahi kutokea baada ya mapinduzi ya kiongozi wa muda mrefu wa Tunisia Zine al-Abidine Ben Ali mwaka wa 2011.

NDEGE YA UJERUMANI YAANGUKA IKIWA NA WATU 150


Ndege ya shirika la ndege la Germanwing inayofanana na ile iliyoanguka.

NDEGE ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 imeanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa.

Mchoro ukionyesha eneo ambalo ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na rada.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 142 na wahudumu sita ikitokea jijini Barcelona nchini Uhispania kuelekea Duesseldorf, Ujerumani.

Ubao wa kuonyesha ndege zilizowasili kwenye uwanja wa ndege wa Duesseldorf, Ujerumani.

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa chini ya nembo Germanwings imeripotiwa kuanguka katikati ya Barcelonnette na Digne.

Rais wa Ufaransa amesema: "Mazingira ya ajali hiyo ambayo bado hayajawekwa bayana, yanawapa wasiwasi kufikiri kama kuna mtu yeyote aliyenusurika"

Kuchimba dhahabu kutoka kwa Kinyesi !



Amini usiamini wanasayansi nchini Marekani wameanza mikakati ya kusafisha dhahabu kutoka kwa kinyesi cha watu.

Amini usiamini wanasayansi nchini Marekani wameanza mikakati ya kusafisha dhahabu kutoka kwa kinyesi cha watu.

Kwa mujibu wa ripoti moja watafati hao wanasema kiwango cha dhahabu na madini mengine nadra na yenye thamani ya juu kwenye

vituo vya kusafishia kinyesi inazidi idadi ya utafiti unaofanywa katika katimbo nyingi za dhahabu.

''Kiwango cha dhahabu hapa ni cha juu zaidi ya viwango vinavyotumiwa na watafiti kubaini iwapo mgodi una madini hayo ya kutosha au la''

Ripoti hiyo imechapishwa katika kongamano la 249 la wanakemia wa Marekani '' American Chemical Society (ACS) iliyoandaliwa huko Denver Marekani .

Kulingana nao iwapo kutatambuliwa mbinu ya kusafisha kinyesi na kuitenga dhahabu atakayegundua mbinu hiyo ataisaidia sana mazingira.

Daktari Kathleen Smith, aliyesaidia katika uandishi wa ripoti hiyo kinyesi cha watu kina kiwango cha juu mno cha dhahabu, fedha ,palladium na vanadium.

'' madini hayo ya vanadium shaba yanamanufaa makubwa sana katika utengenezaji wa bidhaa zinazotumika katika simu za mkononi na kompyuta mbali na bidhaa mbalimbali za kielektroniki.




Kinyesi kutoka kwa wamarekani milioni moja inazaidi ya dhahabu na madini yenye thamani ya dola milioni 13.

Marekani huwa inasafisha zaidi ya tani milioni saba ya kinyesi kila mwaka kulingana na dakta Dr Smith.

Nusu ya uchafu huwa hutumika tena kutengeza mbolea katika misitu huku nusu iliyosalia ikitumika kurejesha ubora wa ardhi baada ya kuchimbwa kwa madini tofauti tofauti nchini humo.

Watafiti hao wanatumia mbinu maalumu inayotumia kemikali ifahamikayo kama '' leachates'' kufyonza madini kutoka kwenye mawe.

Utafiti huu unatilia pondo utafiti wa awali uliodai kuwa kinyesi kutoka kwa wamarekani milioni moja inazaidi ya dhahabu na madini yenye thamani ya dola milioni 13.

Sad Nyuzzzzzzzzzz:NDEGE ZA MUUNGANO ZA KIVITA DHIDI YA DAESH ZAUA 66 SYRIA

Ndege za kivita za muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh nchini Syria zimefanya mashambulio katika maeneo kadhaa na kuua raia 66 wa nchi hiyo.
 Harakati ya Kutetea Haki za Binadamu iliyoko nchini Uingereza inayoitwa Syrian Observatory for Human Rights 'SOHM' imeeleza kuwa, raia 66 wa Syria wakiwemo watoto 10 na wanawake 6 wameuawa katika mashambulio yaliyofanywa na ndege za kivita za muungano ulioundwa na Marekani dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh katika mikoa ya al Raqqa, Deir al Zor, al Hassakah, Idbil na mji wa Manjeb ulioko umbali wa kilomita 446 kaskazini mwa Damascus, Mji mkuu wa Syria.

Muungano huo ulianza kufanya mashambulizi ya anga tokea mwezi Septemba mwaka jana ndani ya ardhi za Syria kwa kisingizio cha kushambulia ngome za kundi la kigaidi la Daesh, ambalo limefanya unyama na mauaji makubwa nchini humo.

 Syria ilianza kutumbukia kwenye ghasia na machafuko tokea mwezi Machi 2011, na hadi sasa watu wasiopungua laki mbili na elfu kumi na tano wameshapoteza maisha.
GPL

Utata zaidi waibuka kifo cha Mdogo wake Mwanamuziki Chameleon AK47 Aliyeanguka na Kufariki


Kifo cha msanii wa muziki AK47 wa nchini Uganda, kimeendelea kuzua maswali hasa kutokana na taarifa mpya kuibuka kuwa, baunsa aliyeibuka na kuandika maelezo polisi kuhusiana na namna alivyomkuta marehemu baada ya kuanguka na kuzimia, siyo mwenyewe.

Taarifa hizo mpya zimetolewa na mhudumu aliyekuwa eneo la tukio siku ya kifo cha marehemu, taarifa ambazo zinaongezewa nguvu na ripoti ya msanii Diamond Oscar aliyekuwa na marehemu siku ya tukio kuwa, waliletewa taarifa ya kuanguka na kuzimia kwa marehemu na baunsa ambaye hawamfahamu.


Sambamba na hisia kuwa huenda marehemu alishambuliwa na kuumizwa kabla ya kufariki, imefahamika kuwa Jumamosi iliyopita, marehemu aliingia katika ugomvi na mabaunsa katika baa nyingine iliyopo maeneo ya Cemetery Park huko Uganda.

2015-03-23

INA SIKITISHA SANA: MWANAMKE MJAMZITO ADUNGWA KISU TUMBONI NA MWANAMKE MWENZAKE


Maafisa wa polisi wa Colorado ambapo mwanamke mjamzito alidungwa kisu na mwanawe kuchukuliwa kutoka tumboni
 
Maafisa wa polisi katika jimbo la Colorado wanasema kuwa mwanamke mmoja alimdunga kisu mwanamke mjamzito katika tumbo lake na kumchukua mwanawe ambaye alikuwa hajazaliwa. 

Mwathiriwa ambaye alikuwa mja mzito wa miezi saba anatarajiwa kupona kufuatia upasuaji lakini mtoto aliaga dunia. 

Mwanamke huyo mjamzito alikuwa akimtembelea mshukiwa ili amnunulie mwanawe nguo ambazo zilikuwa zimetangazwa katika katika soko la mtandao la Craigslist. 

Mshukiwa Dynel Catrece Lane alimpoteza mwanawe wa miezi 19 muongo mmoja uliopita alipokufa maji katika kidimbwi cha samaki. 

                             Mjamzito
 
Mwathiriwa mwenye umri wa miaka 26 alikua akitaka kununua nguo hizo wakati aliposhambuliwa siku ya jumatano. 


Wakati alipoingia katika nyumba hiyo alishambuliwa na kupigwa kabla ya mwanawe kutolewa kutoka tumboni'',Afisa mmoja wa Polisi Jeff Satur alisema. 

Mwathiriwa alifanikiwa kupiga simu ya dharura lakini alipatikana katika hali mbaya wakati maafisa walipowasili.

2015-03-19

Ina sikitisha sana:IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA SHAMBULIO TUNISIA YAFIKIA 23

Miili ya baadhi ya watu waliopoteza maisha kwenye shambulio hilo ikifunikwa.

IDADI ya watu waliopoteza maisha katika shambulio la kigaidi lililotokea jana nchini Tunisia imeongezeka na kufikia 23. 


Majeruhi katika shambulio hilo wakipatiwa huduma ya kwanza.

Mwananmke mmoja raia wa Uingereza ameongezeka na kufanya idadi ya watalii waliouawa kwenye shambulio hilo kuwa 18.

Mwananmke huyo ametambulishwa kwa jina la Sally Jane Adey wakati wa mkutano na wanahabari uliofanywa leo na Wizara ya Afya nchini Tunisia. 

Wananchi wa Tunisia wakiwakumbuka wenzao waliofariki katika shambulio hilo.

Watu hao 23 wakiwemo watalii 18, raia wa Tunisia wawili na wapiganaji wawili walifariki baada ya wapiganaji hao kuvamia jengo moja la kumbukumbu za kihistoria liitwalo Bardo ambalo liko jirani na bunge nchini Tunisia. 


Baadhi ya wananchi walionusurika katika shambulio hilo wakielekea eneo salama. 


Usalama ukiwa umeimarishwa katika maeneo ya bunge jirani na shambulio lilipotokea.
GPL

MAREKANI YATHIBITISHA KUMUUA KWA KOMBORA MOJAWAPO YA VIONGOZI AL SHABAAB

Kikundi cha wapiganaji wa Somalia cha Al Shaabab. 

Kikosi cha ulinzi nchini Marekani.

Wizara ya ulinzi nchini Marekani imethibitisha kwamba imemuua mojawapo ya viongozi wa kundi la wapiganaji wa Somalia Al Shabaab kupitia kombora.

Adan Garaar alituhumiwa kupanga shambulio katika jumba la kibiashara la West Gate nchini Kenya miaka miwili iliyopita.

Maafisa nchini Marekani wanasema aliuawa kusini mwa Somalia ijumaa iliyopita. 


Marekani imekuwa ikikagua operesheni hiyo kabla ya kuthibitisha kwamba Garaar ndiye aliyekuwa akilengwa.

Nchi hiyo imewalenga viongozi wengine wakuu katika kundi hilo la wapiganaji wenye itikadi kali za kiislamu kwa mkombora akiwemo kiongozi wa zamani wa kundi hilo, Ahmed Godane.

GPL
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...