2014-10-23

Nisha: Sijafulia jamani

BAADA ya saluni yake iliyopo Sinza jijini Dar kufungwa huku uvumi wa kudaiwa kufulia ukimuandama, msanii wa filamu, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka kuwa uvumi huo hauna ukweli.


                                      
Msanii wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’.

 Akizungumza na mwandishi wetu, Nisha alisema biashara yake ya saluni ipo kama kawaida ila ameihamishia maeneo ya Chuo Kikuu - Mlimani kwa kuwa eneo la awali halikuwa na nafasi kubwa.    “Sijafulia hata kidogo hayo ni maneno tu yanayozagaa, saluni yangu nimeihamishia Mlimani jamani, nashangaa kweli kwa wanaosema nimefulia,” alisema Nisha.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...