2015-01-29

Daaaaaaa;VPL Matokeo ya Simba vs Mbeya City yako hapa


Mechi kati ya timu ya Simba SC na Mbeya City, Simba wamejikuta wakikubali kichapo cha goli 2-1 katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Hamad Kibopile na Yusuph Abdallah aliyefunga kwa njia ya penalti, wakati goli la Simba limefungwa na Ibrahim Hajib ‘Mido’. 

Hata hivyo dakika ya mwisho ya mchezo, Masoud Nassor ‘Cholo’ amekosa mkwaju wa penalti baada ya beki Yusuph kumfanyia madhambi Jonas Mkude katika eneo la hatari.
Hiki ni kipigo cha pili kwa Simba ndani ya uwanja wa Taifa, December 26 mwaka jana walifungwa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...