Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Steven Pentzel ‘Jack Pentzel’ akiwa na mumewe Gardner Dibibi. Kikizungumza na Ijumaa Wikienda, chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wanandoa hao, kilisema kwamba, kila kukicha wawili hao wamekuwa wakigombana na sababu kubwa ni Jack kuchelewa kurudi nyumbani.
Ilidaiwa kwamba, tangu Jack awe na ushosti na staa mwenzake wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka amekuwa ni mtu wa kujiachia na kujisahau kwamba ni mke wa mtu. “Yaani ndoa ya Jack inashikiliwa na uzi kwani kila siku wanapigana na hivi karibuni mumewe alikusanya nguo na kuweka kwenye begi akitaka kuondoka nyumbani.
“Tatizo mwanamke anachelewa kurudi nyumbani, mumewe akimuuliza ndiyo mgogoro unaanzia hapo,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilimsaka mume wa Jack, Dibibi ili kueleza ukweli juu ya suala hilo. ‘Jack Pentzel’ na mumewe wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rose Ndauka.
“Kutofautiana ni jambo la kawaida na huwa tunagombana tu kawaida lakini siyo ugomvi mkubwa kama watu wanavyosema. “Sijaondoka nyumbani, mbona nipo tu na mke wangu, hao wanaosema hivyo wanataka kutukosanisha tu.”
Kumekuwa na uvumi wa kuvunjika kwa ndoa hiyo iliyofungwa mwanzoni mwa mwaka jana ambayo haijajaliwa kupata mtoto.
0 comments:
Post a Comment