2015-03-23

Taasisi Ya Kiislam Yaitaka Serikali Iwakamate Maaskofu Waliotoa Tamko......Yasema Wasipokamatwa Itahamasisha Waislam Wote Kupiga Kura Ya HAPANA


Taasisi ya dini ya Kiislam imeitaka serikali kuwakamata maaskofu na wachungaji ambao inadai wametoa matamko ya kichochezi na endapo serikali itashindwa kuwakamata, basi jumuiya hiyo itawahamasisha waamini wa dini ya kiislam popote walipo kuipigia kura ya HapanaKatiba inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.

Kauli ya taasisi hiyo yenye misimamo mikali inatokana na Tamko lililotolewa na muunganiko wa jumuiya ya Kikristo,ikiwemo Baraza la Maaskofu katoliki (TEC),Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Baraza la Makanisa la kipentekoste(CPCT) ambao wote kwa pamoja waliwataka waunini wa dini ya kikristo nchini kuipigia kura ya Hapanakatiba inayopendekezwa kutokana na serikali kuruhusu mahakama ya Kadhi kisheria.

Akitoa tamko la Taasisi ya Dini ya Kiislam ambalo ni muunganiko wa taasisi za dini hiyo zaidi ya 11 hapa nchini,Naibu Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Sheikh Rajab Katimba wakati wa Mkutano na Vyombo mbalimbali vya habari jana Jijini Dar es Salaam, aliitaka serikali kuwachukulia hatua maaskofu hao kwa madai ya kufanya uchochezi.

“Serikali iwachukulie hatua za kisheri maaskofu na wachungaji kwa kutoa matamko yakichochezi yaliyokusudia kuumiza hisia ya kidini kwa waislam kinyume cha sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16.

"Tunataka Maaskofu hao wakamatwe,wafikishwe mahakamani na dhamana izuiliwe kama inavyofanya kwa masheikh pindi wanapotoa kauli zinazopingana na mtazamo wa serikali,lasivyo hatutaipigia kura ya Ndiyo katiba iliyopendekezwa”alisema Seikh Katimba.

Aidha, Sheikh Katimba aliitaka Serikali kuendelea na Mchakato wa uundwaji mahakama ya kadhi kwa kufuata maoni yaliyotolewa mbele ya kamati ya sheria na utawala wa bunge kwa kuzingatia mambo muhimu mawili.

Mosi: Serikali iache njama na hila za kuigeuza mahakama ya Kadhi inayohitajika kuwa miliki ya taasisi ya BAKWATA na MUFTI wa BAKWATA. 


“Endapo serikali itaendelea na kuwasilisha muswaada wa Mahakama ya Kadhi unaoipa mamlaka Bakwata kuunda,kusimamia,kuteua makadhi nakadhalika kinyume na maoni ya Waislam wengi itakuwa imethibitisha kuwa serikali haikuwa na nia ya kweli ya kuunda na kuanzisha mahakama ya Kadhi” alisema Sheikh Katimba.

Pili: Serikali igharamie mahakama hiyo kama inavyogharimia uendeshaji wa mashauri yaliyopo kwenye mahakama za kawaida yanayohusu sheria za kiislam ambayo mara nyingi yanaamuliwa kwa makosa.

“Na pia mahakama hiyo igharamiwe na serikali kama inavyogaramia huduma za makanisa chini ya mkataba maarufu uitwao memorandum of understanding (MOU) , mkataba ambao haukuwahusisha wala kutaka ridhaa ya waislam” alisema sheikh huyo.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...