Mmoja wa vijana walioshambuliwa kwa kipigo nyumbani kwa wema.
Mkono wa sheria! Achana na drama zake na aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mcheza sinema ‘grade one’ Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ anapandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar kujibu kesi ya kushambuliwa vijana wawili, Rashid Balazi na Juma Bushiri, wakazi wa jijini Dar
HAYUKO PEKE YAKE
Katika kujibu kesi hiyo, Madam Wema hatakuwa peke yake kwani mpambe wake, Petit Man naye anahusika katika kesi hiyo kwa kuwa ndiye mshtakiwa wa kwanza.
Hivi karibuni kabla Madam Wema hajasafiri kwenda nchini Ghana kufanya kazi na staa wa huko, Van Vicker, Petit Man alidaiwa kuhusika kuandaa mchezo mchafu wa kuwateka na kuwashushia kipigo cha mbwa mwitu Rashid na Juma, tukio ambalo lilichukua nafasi nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar.
Ilidaiwa kwamba, Petit Man alipoteza simu na kuwahisi vijana hao ambao mmoja wao alikuwa ni fundi bomba, ambaye alikuwa akitengeneza bomba nyumbani hapo.
0 comments:
Post a Comment