2015-01-21

Afunguka;Kajala Asema Yupo Tayari Kugharamia Harusi ya Wolper na Manaiki


Jack Wolper na Kajala 


Mrembo na mwigizaji anayefanya vizuri kunako soko la filamu za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ ameweka wazi kuwa yuko tayari kugharamia sherehe ya harusi ya Manaiki Sanga na Jacqueline Wolper Massawe kama mambo yataenda sawa.


Jack Wolper na Manaiki Sanga

Akizungumzia swala la mwigizaji na rafiki yake Jackline Wolper kuchumbiwa na msanii Manaiki Sanga,Kajala alisema kutokana na ukaribu alionao kwa watu hao basi mambo yote yanayohusiana na sherehe yatakuwa chini yake kwa maana ya gharama zote na kikubwa ni kuwaombea tu maana ni muda mrefu sana Manaiki alikuwa na ndoto za kumuoa Wolper.

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni manaiki aliibuka na kutangaza kumposa Wolper. Ngoja tuendelee kusubiri "Movie" hii.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...