2015-01-29

Daaaaaaaaaa;Prof Lipumba kupigwa: Bunge Lahairishwa tena hadi Kesho Asubuhi


Spika wa Bunge Anna Makinda jioni hii amelazimika kuahirisha tena kikao cha Bunge hadi kesho asubuhi kwa madai kuwa serikali bado inajipanga kutoa majibu sahihi kutokana na tukio la kupigwa mabomu Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba. 







Kuahirishwa kwa bunge kumetokana na vurugu zilizotokea leo asubuhi bungeni baada ya kutolewa kwa hoja binafsi kutoka kwa Mbunge na Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia kuhusu jeshi la polisi kumshambulia Profesa Ibrahimu Lipumba jana akiwa kwenye maandamano .

Timbwili zima la vurugu hizo za Asubuhi toka bungeni liko hapo chini katika video iliyopachikwa. Bonyeza 

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...