2015-01-16

INAHUZUNISHA SANA:WANA HARAKATI WA DODOMA WAKIMJULIA HALI MWANAFUNZI WA UDOM ALIYEVUNJIKA MGUU


Mr Dannis akiwa na Msouth kato baada ya kumtembelea kijana ambaye ni mwanafunzi wa Udom aliyepata majanga ya kuvunjika mguu baada ya kuruka kwenye gari na kutaka kuwakwepa Polisi waliokuwa wanahakikisha usalama unapatikana katika chuo hicho cha Udom kutokana na baadhi ya wanafunzi kuwashawishi wanzao kufanya maandamano yasiyokuwa ya Maani kutokana na kile kinachodaiwa kutopata Mkopo kwa muda unaostahili


Kijana ambaye ni mwanafunzi wa Udom anayefahamika kwa jina la Iddy aliyepata masaibu baada ya kuvunjika mguu katika vurugu za mgomo uliyofanywa na wanafunzi wa Udom wa college ya social science..
 
 Kijana Iddy ambaye amelazwa katika hospitali ya General Dodoma leo hii amepatiwa msaada Mh Shabiby wa fedha za 

matibabu pamoja na while chair baada ya kuzuiliwa kutoka hospitali hapo nkutokana na deni kubwa la matibabu aliyokuwa anadaiwa hospitalini hapo..
 Paparazi wa blog ya Boss Ngasa alifanikiwa kupata nafasi ya kuongea na mzazi wa mwanafunzi huyo na kudai kuwa aliambiwa atapata msaada kutoka chuoni hapo lakini cha kushangza mpk muda huu wa jioni hatujapa msaada wowote kutoka chuo hicho zaidi ya kupigwa chenga na kutupiana mpira..
 Baba wa kijana huyo ametoa shukrani za pekee kwa Mh Shabiby baada ya kuguswa kiubinadamu na kumsaidia kijana wake... Kijana Iddy kwa sasa anaendelea vizuri 
 


0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...