2015-01-26

MAMBO MOTO;SHIJA AMWANIKA MWANAYE

Msanii wa filamu Bongo, Deogratius Shija akiwa na mwanaye, Theresia Shija (14). 


Stori: Gladness Mallya/Ijumaa Wikienda
KWA mara ya kwanza msanii wa filamu Bongo, Deogratius Shija amemwanika mwanaye na kudai ndiye faraja kwake kila anapomuona.

Shija alisema mwanaye aliyemtaja kwa jina la Theresia Shija (14), amekuwa ni faraja kubwa katika maisha yake na kila anapomwangalia anapata nguvu ya kufanya kazi.

“Ukweli nimekuza, mwanangu ndiyo ameanza kidato cha kwanza kila ninapomwangalia napata nguvu ya kufanya kazi zaidi ili niweze kumlipia ada aweze kupata elimu nzuri itakayomsaidia maishani mwake,” alisema Shija.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...