2015-04-08

HUSNA MAULID YAMKUTA!............soma hapa


MSHIRIKI wa shindano la Miss Tanzania 2011/2012, Husna Maulid.
MSHIRIKI wa shindano la Miss Tanzania 2011/2012, Husna Maulid yamemkuta ya mwaka, kwa kudaiwa kutolewa vitu vyake nje na mwenye nyumba baada ya kushindwa kulipa kodi, huko Shekilango jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, zoezi lililosimamiwa na mabaunsa.

Chanzo cha kuaminika kililiambia gazeti hili kuwa mrembo huyo alikuwa akidaiwa pango kwa kipindi kirefu, kiasi cha mwenye nyumba kushindwa kuvumilia. 

“Tatizo hawa mastaa wetu wanapenda kuishi maisha ya kuigiza, kama mtu huna fedha jitahidi kuishi maisha ya kawaida, siyo ndiyo unataka kuonekana umekamilika kwa kila kitu, mimi naamini kwa kilichomkuta Husna wengine watajifunza pia,” kilisema chanzo hicho kwa masharti ya kutotajwa jina. 


“Mimi sijafukuzwa na wala sijatolewa vitu vyangu nje eti kisa nimeshindwa kulipa kodi ya nyumba, niliamua kuhama mwenyewe baada ya kuona mwenye nyumba kanipandishia kodi na sasa hivi ninaishi Mbezi Beach,” alisema Husna baada ya kuulizwa na kuongeza kuwa hataki kujionyesha anapoishi, lakini wanaomfahamu wanajua sehemu gani anaishi hivi sasa.
GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...