Umbile la mwanadada aliyefahamika kwa jina moja la Avril kutoka Kenya ambaye aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, hivi karibuni lilionesha kumchengua msanii wa Bongo Fleva, Omari Faraji ‘Ommy Dimpoz’ baada ya kutupia picha inayomuonesha akikitolea macho kiwowowo cha demu huyo.
 
Msanii wa Bongo Fleva, Omari Faraji ‘Ommy Dimpoz’ akiwa na Mwanadada Avril kutoka Kenya.
Ommy alifanya hivyo kupitia ukurasa wake wa Instragram baada kuiweka picha hiyo kisha kuanza kukisifia kijungu cha Avril kiasi cha kumfanya mmoja wa mashabiki wake atupie maoni akisema: “Unaonekana kaka wewe ni mgonjwa wa wanawake waliofungashia, ila huyu demu mkali.”
‘Ommy Dimpoz’ akitupia jicho kijungu cha Avril.
Mbali na maoni hayo mengine yaliendelea kukichambua kiumbile kizuri alichonacho mwanadada huyo na Ommy alipopigiwa simu ili kuulizwa kilichomvutia kwa demu huyo na kama anataka kujiweka kwake alikuwa akikata.
0 comments:
Post a Comment