KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeiagiza Bodi ya Korosho Tanzania, kuandika barua inayoeleza hatua walizochukua katika kurudisha nyumba iliyouzwa kwa Mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry Koka (CCM).
Akitoa agizo hilo, Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alisema kamati yake haijaridhishwa na namna nyumba hiyo ilivyouzwa.
Akitoa agizo hilo, Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alisema kamati yake haijaridhishwa na namna nyumba hiyo ilivyouzwa.
Zitto aliitaka Bodi hiyo kuhakikisha inapeleka barua yenye taarifa na lazima iifikie kamati leo saa 6, ikieleza mchakato, taratibu na hatua waliyofikia katika kushughulikia suala hilo.
Taarifa ya CAG inaonesha nyumba ya Bodi ya Korosho iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam, iliuzwa kwa Koka kwa thamani ya Sh milioni 300 na iliyokuwa Bodi ya Kilimo, ambayo kwa sasa haipo.
Pia, Zitto aliiagiza Bodi hiyo kuhakikisha wanatafuta hati za nyumba na viwanja vyake na kila hatua wanayofuatilia watoe taarifa kwa kamati.
Aidha, PAC imeitaka Bodi ya Korosho kuhakikisha mapato ya nje yanayopatikana kutokana na kuuza korosho, wayatumie kuongeza thamani ya zao hilo ikiwamo kufufua viwanda.
0 comments:
Post a Comment