2015-01-16

Sad news:Ajali ya basi yaua wanne Bagamoyo

Screen Shot 2014-09-08 at 3.29.59 PM

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Ulrich Matei alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea jana saa mbili asubuhi wakati basi hilo likitokea wilayani Handeni, Tanga kwenda Dar es Saalam.

Bagamoyo. Watu wanne wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya basi la Hajees kupinduka katika Kijiji cha Mnazi, Kata ya Mandela wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Ulrich Matei alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea jana saa mbili asubuhi wakati basi hilo likitokea wilayani Handeni, Tanga kwenda Dar es Saalam. 


Aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Mkomwa Juma (35) aliyekuwa kondakta wa basi hilo mkazi wa Kimange, Mayunga Ramadhan (45), Siasa Idd (22) mkazi wa Kwamakocho na Rehema Omary (35).

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kutaka kulipita lori lingine lililokuwa mbele yake, ndipo alipokutana na basi hilo.

Alisema hali hiyo ilimlazimu dereva wa basi kujaribu kulikwepa lori, lakini alishindwa na kupinduka pembeni ya barabara kuu ya Chalinze-Segera.

Alisema dereva wa lori lililosababisha ajali hiyo amekamatwa na hatua zaidi za kisheria zinaendelea, huku akisema dereva wa basi alikimbia.

Kamanda alisema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo. 


Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Bagamoyo, Ahmed Kipozi alitoa wito kwa madereva kuacha kuendesha magari kwa kasi.
 Alisema wanapaswa kuwa waangalifu hususan wanapopita kwenye maeneo ya miinuko na kona kali ili kuepusha ajali.
 Mwananchi.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...