2015-01-29

Unajua;Kwa nini Leo Zitto Kabwe Alitia Mgomo wa kwenda kusoma taarifa ya PAC Bungeni?????.....Majibu yote Yako hapa.



Wakati wa Vurugu za Asubuhi leo Bungeni, Spika wa Bunge alimtaka Mwenyekiti wa PAC, Mh Zitto Kabwe aende kusoma taarifa ya kamati yake....


Kilichotokea ni kwamba, Zitto alitia mgomo, nikiwa na maana kwamba alipuuza agizo hilo na hakunyanyuka kabisa.

Unajua ni kwa nini? Zitto Kabwe mwenyewe amekwisha lijibu hilo swali kupitia ukurasa wake wa Facebook.

"Kwa nini sikwenda kusoma taarifa ya PAC leo nilipoitwa na Spika? Jibu rahisi kabisa, siwezi kuona madhila na uvunjifu mkubwa wa HAKI za binadamu nikaendelea na mambo kama hakuna kilichotokea.Kitendo cha polisi kutumia nguvu, kupiga raia hovyo na kumdhalilisha kiongozi wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ni kitendo cha kulaaniwa kwa nguvu zote"- Zitto Kabwe



0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...