Mwili wa Mkazi wa kijiji cha Kabalenzi Kata ya Kanazi wilayani Ngara mkoani Kagera Andrew Lazaro (36) ukiwa
kitandani baada ya kuuwawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo
Januari 28,2015 kwa kumkatakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake
baada ya kumvamia akiwa na familia yake kijijini humo.
Kaimu Mwenyekiti wa kijiji hicho Jakson Bamenya amesema kuwa marehemu alivamiwa jana saa 5 usiku ambapo waliotekeleza mauaji hayo walimgongea mlango na kumshambulia.
Bamenya amesema taarifa
zilizopatikana kutoka kwa mke wa marehemu ni kwamba wakati wakifungua
mlango walimwangusha chini na kumshambulia kwa kumkamata na mapanga na
mkewe kumfunga kitambaa usoni.
“Tumepata
maelezo ya mkewe alfajiri na tulipofika tukakuta mwili wa marehemu
unayo majeraha makubwa ambayo yalitokana na kucharangwa mapanga na
wauaji kutokomea kusikojulikana,”- Alisema Bamenya.
Akiongea
na Wanahabari,Mke wa marehemu Revina Andrew (27) amesema kuwa wakati
wamelala ndani ya nyumba yao wakiwa na watoto wao wanne mumewe aliitwa
na watu wakimtaka afungue mlango huku wakishikilia visu na mapanga.
Amesema
aliposita kufungua walibomoa mlango huo na nyumba ikiwa imezingirwa
ambapo baadhi yao waliwafunga watoto kamba na Mama huyo kumfunga
kitambaa cheusi usoni kisha kumkatakata mapanga Mume wake.
Kamanda
wa Polisi mkoani Kagera Henry Mwaibambe alipoulizwa kwa njia ya simu
amesema Jeshi la Polisi wilayani Ngara limefika eneo la tukio lakini
hajaarifiwa kukamatwa watuhumiwa wa mauaji hayo na upelelezi unaendelea.
0 comments:
Post a Comment