2015-02-28

UNDANI WA KIFO CHA KEPTENI JOHN KOMBA!

Marehemu Kapteni Komba. 

Picha ya kwanza ya Marehemu komba mara baada ya kufariki dunia. 

...Komba enzi za uhai wake. 

MBUNGE wa Mbinga Magharibi, Kapten John Komba amefariki dunia jioni hii jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, hata hivyo hakuwa tayari kuelezea kwa undani kwa madai kuwa taarifa hizo zimemfikia sasa hivi. 

Mmoja wa watoto wa Komba ambaye aliyejitambulisha kwa jina la Herman amethibitisha kutokea kwa msiba huo na akasema, huku akilia, msiba wa baba yake upo nyumbani kwake Mbezi Tangi Bovu, Dar. 

Habari zinasema asubuhi ya leo Komba alikwenda kwenye shughuli zake za kikazi kama kawaida lakini baadaye akajisikia vibaya, hivyo akaamua kurudi nyumbani ambako alizidiwa ndipo familia yake ilipoamua kumkimbiza Hospitali ya TMJ lakini alipopimwa na madaktari ikathibitika kuwa alikuwa tayari ameaga dunia. habari zaidi zinasema kuwa hivi sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo. 

Kapteni Komba ambaye pia ni Mkurugugenzi wa Kikundi cha Maigizo cha Tanzania One Theatre (TOT), ambacho kina kikundi cha taarabu na bendi inayokwenda na mtindo wa Achimenengule, amekuwa akikisaidia sana chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kampeni zake wakati wa uchaguzi kwa kutunga nyimbo za kuhamasisha wapiga kura na kushiriki kupiga live kwenye majukwaa ya kisiasa. 

...alipokuwa bungeni 

Enzi za uhai wake alitamani sana na kufanya juhudi kubwa ili mtindo wa Achimenengule uwe wa kitaifa lakini ikashindikana, na badala yake Watanzania sasa tuna muziki wa Mduara ambao umekuwa kama mtindo wa muziki wetu kwa sababu zifuatazo. 

Kwanza, ni mtindo halisi wa Kitanzania uliochipuka kutoka mahadhi ya kimwambao ya Tanzania. Pili, ndiyo mtindo pekee uliowahi kutumiwa na bendi nyingi baada ya kuasisiwa na ‘mabingwa’ wa muziki wetu, wana Njenje, The Kilimanjaro Band. 

Baada ya bendi hiyo kuuasisi, mtindo huo, tayari umepigwa na bendi kama TOT Plus, Chuchu Sound, Pamo Sound, Inafrika Band, wana mipasho kadhaa na mwanamuziki mahiri lakini asiyethamini kiwango chake kikubwa cha muziki, Bob Haisa. 

Sababu ya tatu ni kwamba mtindo huo umekuwa wa kupigwa na bendi nyingi, vikundi vingi na wanamuziki wengi si kwa kulazimisha bali kwa mapenzi tu ya mashabiki wa muziki wa Tanzania. 

Kapteni Komba awali alikuwa mwalimu wa shule ya msingi kabla ya kuingia jeshini na kuwa kiongozi wa kikundi cha maonesho cha jeshi na baadaye Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akamshawishi aachane na jeshi na kujiunga na CCM wakati wa mfumo wa vyama mingi ulipoingizwa mwaka 1992. 

“Mzee Mwinyi ndiye aliyenifanya niache jeshi wakati huo nikiwa na cheo cha ukapteni. Aliniomba nikisaidie chama kwa kuanzisha kikundi ambacho lengo lake lilikuwa kukipigia debe CCM,” aliwahi kusema hivyo Kapteni Komba. 

Ameshiriki kampenzi za marais Ally Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na aliye madarakani hivi sasa, Jakaya Mrisho Kikwete. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi hadi kifo kinamchukua. 

Licha ya siasa Kapteni Komba alikuwa anamiliki shule na pia alikuwa na biashara kadhaa.
Mwaka 2012 Komba aliwahi kupelekwa India kwa matibabu ambapo alifanyiwa upasuaji wa nyonga baada ya kupata ugonjwa uliosababisha mifupa kusagana sehemu hiyo ya nyonga. 

Baada ya kurejea nchini alisema upasuaji huo ulichukua saa tano na ulifanyika katika Hospitali ya Apollo, India na alikanusha kuwa alikuwa na ugonjwa wa figo.Ugonjwa uliomuua ni shinikizo la damu ambalo lilikuwa likimsumbua kwa muda mrefu. 

..marehemu Komba akiongea na wanahabari nyumbani kwake Mbezi tangi Bovu akielezea kuimarika kwa afya yake aliporejea kutoka India kwenye matibabu, Julai 27, 2012. 



MALI ZAKE ZATISHIWA KUUZWA 

Mapema mwezi uliyopita mwaka huu, mali za Kapteni John Komba zilitangazwa kupigwa mnada kutokana na kushindwa kulipa deni analodaiwa na Benki ya CRDB. 


Mali hizo zilihusisha eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 2,214 lililopo Mbezi Tangi Bovu, Dar es Salaam, kiwanja namba 1030 kilichosajiliwa kwa jina la John Damiano Komba na Salome Komba. 


Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa kwenye vyombo vya habari, Kampuni ya Uwakili ya Mpoki & Associates Advocates inayoiwakilisha CRDB ilitangaza kuuza eneo hilo la kibiashara lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya mafuta, maduka makubwa, benki, sehemu ya kufanyia mazoezi, hospitali na huduma nyingine za kijamii. 

Marehemu Komba ameacha mjane, Bi Salome, ambaye ni mwalimu kitaalumu na watoto kadhaa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi- ameen! 

(Stori: Gladness Mallya/ GPL)

JAJI MKUU AENDELEA NA ZIARA YA KIKAZI MKOANI TABORA


Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (kulia), akijadili jambo na Mhe. Ludovick Mwananzila, Mkuu wa Mkoa wa Tabora alipotembelea Ofisi ya Mkoa wa Tabora alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea Mahakama mkoani humo. 
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (kulia), Mhe. Ludovick Mwananzila, Mkuu wa Mkoa wa Tabora (katikati), Mhe. Jaji Amir Mruma, Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora (kushoto), wakitoa nje ya jengo la Ofisi ya Mkuu wa Tabora, mara baada ya Mhe. Jaji Mkuu na ujumbe alioambatana nao kumsalimia Mkuu huyo wa Mkoa.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (katikati), Mhe. Jaji Amir 
Mruma, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora (wa pili kushoto), Mhe. Sam Rumanyika, Jaji wa Mahakama Kuu,Kanda ya Tabora (wa pili kulia), Mhe. David Mrango, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora (wa kwanza kulia),na Mhe. Jaji Leila Mgonya, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya 
Tabora (wa kwanza kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora. (Picha na Mary Gwera, Mahakama)

Kiongozi wa upinzani auawa Urusi



Mmoja wa wanasiasa maarufu wa upinzani nchini Urusi Boris Nemtsov ameuawa kwa kupigwa risasi kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Moscow.

Mwanasiasa huyo alipigwa risasi nne kutoka nyuma na watu waliokuwa ndani ya gari alipokuwa akitembea nje ya makao makuu ya serikali.

Bwana Nemtsov ambaye alihudumu kama naibu waziri mkuu wakati wa uongozi wa rais Boris Yeltsin alikuwa akimshutumu vikali rais Vladimir Putin.



Alikuwa akipanga mkutano ambao ungefanyika kesho Jumapili kupinga kile alichokitaja kuwa vita vinavyoendeshwa na Urusi nchini Ukrain.

Kwenye mahojiano mapema mwezi huu bwana Nemtsov alisema kuwa alikuwa na hofu kuwa rais Putin angemuua

Marekani kufungua ubalozi wake Cuba



Marekani inasema kuwa itafungua ubalozi wake nchini Cuba kuanzia mwezi Aprili.

Baada ya duru ya pili ya mazungumzo mjini Washington yenye lengo la kurejesha uhusiano kati yao mwanadiplomasia wa cheo cha juu wa Marekani katika nchi za Marekani ya kusini Roberta Jacobson, alisema kuwa itawezekana kufunguliwa kwa ubalozi kabla ya mkutano wa kimaeneo ambao utafanyika nchini Panama kuanzia tarehe kumi mwezi Aprili.

Mkuu wa ujumbe wa Cuba Josefina Vidal alisisitiza kuwa Marekani ni lazima iondoe Cuba kutoka kwa orodha ya nchi ambazo zinaunga mkono Ugaidi kabla ya kurejesha tena uhusiano huo.

Mwezi Disemba Cuba na Marekani walitangaza kuwa walikubaliana kuboresha uhusiano wao baada ya zaidi ya miaka 50 .

Mtoto wa Sokoine ataka Jimbo la Lowassa





                           Namelock Sokoine.

Mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametangaza nia ya kutogombea tena jimbo hilo, hali ambayo imeibua mvutano kwa makada kadhaa wa CCM wilayani Monduli. Namelock alikuwa mmoja wa watoto kipenzi cha hayati Sokoine,

Monduli. Viongozi wa Mila ya kimasai, maarufu kama Laigwanani wa Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha wamesema wanamruhusu kuwania ubunge wa Jimbo la Monduli, mtoto wa kike wa Waziri Mkuu wa zamani, hayati Edward Moringe Sokoine, Namelock Sokoine. 

Mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametangaza nia ya kutogombea tena jimbo hilo, hali ambayo imeibua mvutano kwa makada kadhaa wa CCM wilayani Monduli. Namelock alikuwa mmoja wa watoto kipenzi cha hayati Sokoine,

Katibu wa viongozi hao wa kimasai, Buluka Ngaimeria na Makamu Mwenyekiti wake, Mepukori Mberekeri, kwa nyakati tofauti alisema wao kama viongozi wa mila, hawajatoa msimamo wa kumkataa Namelock kwa kuwa ni mwanamke.

Ngaimeria alisema, hivi karibuni walikutana katika Kata ya Makuyuni, lakini hakukupitishwa azimio la kumkataa Namelock kwa kuwa ni mwanamke.

“Mimi kama Katibu wa viongozi wenzangu, hatukufikia maamuzi ya kumkataa mtu, kile kikao kilikuwa cha kujadili mambo yetu ikiwepo kutokuwa na ofisi na masuala ya siasa haikuwa hoja kuu,” alisema.

Naye Makamu Mwenyekiti wa viongozi hao, Mepukori Mberekeri alisema, yeye ndiye alitoa taarifa kwenye kikao hicho, juu ya tangazo la Namelock kuwania ubunge alilotoa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Monduli. 

“Baada ya kuwapa taarifa mjumbe mwingine alisema pia kuna mgombea mwingine, Loota Sanare na baada ya majadiliano suala hilo liliachwa lije kuamuliwa na wananchi,” alisema.

Alisema sio kweli kuwa wao, wametangaza kupinga kuongozwa na Mbunge mwanamke na sio kweli kuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Edward Lowassa anawashinikiza kumtaka Sokoine.

Uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Monduli, umeibua gumzo kubwa hasa kutokana na uamuzi wa Lowassa kutajwa kuutaka urais.
Mwananchi

Makada CCM wamvaa JK


Aliyekuwa Mwenyekitiwa CCM Mkoawa Dar es Salaam John, Guninita akizungumza na wandishi wahabari, Dar es Salaam jana kuhusiana na kutaka kumshitaki Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 
Kauli hiyo, ilitolewa jana na wenyekiti wa wa zamani wa chama hicho wa Dar es Salaam, John Guninita na Mgana Msindai wa Singida walipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali ya kisiasa.

Dar es Salaam. Makada wawili wa CCM wamemuomba Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha kabla ya Uchaguzi Mkuu, anaondoa makundi ndani ya chama hicho, ambacho kinakabiliwa na kazi ngumu ya kumpata mgombea wake bila ya kutokea mpasuko. 

Kauli hiyo, ilitolewa jana na wenyekiti wa wa zamani wa chama hicho wa Dar es Salaam, John Guninita na Mgana Msindai wa Singida walipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali ya kisiasa.

Wenyeviti hao wa zamani walitishia kumpeleka mahakamani mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kwa madai kuwa amekuwa akiwadhalilisha kwa kuwaita vibaraka wa kada mwingine wa CCM, Edward Lowassa katika mikutano yake na waandishi wa habari.

Tayari wameshamuandikia barua ya kusudio la kumfungulia mashtaka iwapo hataomba radhi kwa vitendo hivyo, lakini Makonda aliwajibu kuwa alitoa maneno hayo kwa niaba ya chama na kwamba aliyetakiwa kufungua kesi ni Lowassa.

Jana kwenye mkutano na waandishi wa habari, Guninita, ambaye alisema mwenyekiti mwenzake alikuwa na udhuru, alidai kuwa katika kipindi cha hivi karibuni chama hicho kimekumbwa na changamoto ambazo zinatakiwa kutafutiwa ufumbuzi haraka kutokana na baadhi ya viongozi kutokuwa na uchungu na kutotetea chama hicho kwa ajili ya kukijenga.

“Mwenyekiti wa chama, Rais Kikwete kwa kutumia uzoefu anaoufanya wa kutafuta maridhiano katika nchi mbalimbali za Afrika, atumie uzoefu huo kuondoa mpasuko ndani ya chama chetu,” alisema Guninita.

“Hivi sasa chama kinapotea, kila mtu anafanya anavyotaka. Chama cha miaka ya nyuma si cha sasa, viongozi tulikuwa tukiandika barua za malalamiko na yalikuwa yanashughulikiwa, lakini hivi sasa hata ukiandika hakuna anayekusikiliza wala kukujibu.” 


Hata hivyo, katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipotafutwa kuzungumzia tuhuma hizo haikupatikana.

Akizungumzia kukashifiwa kwao na makonda, ambaye pia ni katibu wa hamasa wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Guninita alisema: “Licha ya kumtaka atuombe radhi, amekataa sasa tumepanga kwenda mahakamani.

“Mimi siwezi kutukanwa na kijana mdogo, nimekuwa mkuu wa wilaya miaka 25 iliyopita, nimekuwa mwenyekiti wa UVCCM kwa miaka kumi... UVCCM ni sehemu ya kuwapika vijana kuja kuwa viongozi, lakini sasa imekuwa sehemu ya kuzalisha watu wanaopiga viongozi.”

“Taratibu za kuwasiliana na mawakili wangu zimekamilika na Jumatatu tunatarajia kwenda mahakamani kwani alichotufanyia Makonda hatuwezi kukiacha hivi hivi,” aliongeza

Guninita alisema: “Eti Makonda ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya, Rais ana uhuru wa kuteua lakini hapa niseme tu kuwa wanaomshauri walikosea kabisa kama mtu anateuliwa kwa kumpiga mtu tena kiongozi mkubwa serikali iliyopita ni jambo la hatari.”

Mwananchi

Prof. Muhongo agoma kuzungumzia urais Sababu ni Hizi

Image result for pks za sospeter muhongo
SIKU chache baada ya wazee wa Wilaya ya Musoma, na jana tena baadhi ya viongozi wa mashina na matawi wa Chama Cha 

Mapinduzi (CCM) jijini Dar es Salaam kumtaka aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, achukue fomu ya kuwania urais, mwanasiasa huyo amesema hataki kujisumbua kuzungumzia mambo ya urais kwa sasa.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu katikati ya wiki hii kuhusiana na tamko hilo, Profesa Muhongo, licha ya kukiri wazi kuwa amesikia taarifa hizo kutoka katika makundi mbalimbali ya kijamii, lakini alishindwa kutanabahisha kama anayo nia ya kugombea urais mwaka huu.

“Nimesikia hata wanafunzi wa vyuo vikuu wakitoa tamko la namna hiyo, lakini nyie si mna mtu wenu mnayemjengea hekalu?Kwa hiyo hata nikiwaambia mambo ya urais kwa sasa nitakuwa najisumbua bure, niacheni nipumzike,” alisema Profesa Muhongo.

Hata hivyo, gazeti hili lilidokezwa juu ya kile kinachoitwa mkakati uliokuwa nyuma ya tamko la wazee hao wa Musoma, kwamba liliratibiwa na kijana mmoja aliyetajwa kwa jina la Peter Haule.

Gazeti hili limebaini kuwa mkakati huo ulikuwa ni mpango wa Profesa Muhongo mwenyewe kupima kina kuona kama anaweza kujitosa kwenye siasa kupitia mgongo wa wazee hao wa Musoma.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, mmoja wa wajumbe wanaounda umoja wa wazee wa Musoma (jina tunalo), alidokeza kuwa tamko lao linatokana na msukumo wa Haule, aliyedai kuwa ameagizwa na Profesa Muhongo awaambie wazee hao watoe tamko la kumtaka mwanasiasa huyo achukue fomu ya kuwania urais.

“Sisi wazee tuliitwa na mwenyekiti wetu wa muda, ambaye alituambia kuna ujumbe kutoka kwa Profesa Muhongo, tulipokutana alitutambulisha kwa kijana huyo 
aliyejitambulisha kwa jina la Haule, kijana huyo akatuambia kuwa ujumbe aliotumwa ni kutuomba tumuunge mkono Profesa Muhongo kwenye urais,” alisema.

Alisema kijana huyo ndiye aliyewasaidia kuandika tamko lao ambalo lilisambazwa kwenye vyombo vya habari.

Gazeti hili liliwasiliana na Haule kwa njia ya simu kuhusiana na jina lake kutajwa kuinjinia mkakati huo, lakini katika hali ya kushangaza alishtuka na kukata simu.

Hata hivyo, baada ya dakika chache, Haule alipiga simu mwenyewe na kukana kuhusika kwenye mkakati huo.

“Siku wazee walipotoa tamko nilipigiwa simu na rafiki yangu akiniambia nifuatilie taarifa ya habari ya TV, usiniguse, mimi ni mfanyabiashara, kuwa makini katika kipindi hiki cha uchaguzi,” alisema Haule.

Alipoulizwa msingi wa kupigiwa simu na rafiki yake huyo kumtaka afuatilie taarifa za wazee hao kutoa tamko la Muhongo, Haule alisema alifanya hivyo kwa sababu yeye ni mtu anayefuatilia siasa.

Jana baadhi ya viongozi wa mashina na matawi wa CCM jijini Dar es Salaam nao wameibuka na kutoa tamko la kumtaka Muhongo achukue fomu ya kugombea urais.

Wamesema, pamoja na kwamba kuna wagombea wengi wa nafasi hiyo kupitia CCM, Profesa Muhongo ndiye chaguo lao kwa kuwa wanaamini anaweza kuiongoza nchi na kuifikisha mahali pazuri.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa chama hicho katika Kata ya Magomeni, Sadick Kadulo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

“Rais Kikwete alipokuwa akizungumza katika sherehe za CCM za kutimiza miaka 38 mjini Songea hivi karibuni, alisema tuwahamasishe wana CCM wenzetu wenye uwezo wa kugombea urais ili wagombee.

“Kwa hiyo, sisi tumetumia fursa hiyo kumuomba Profesa Muhongo agombee urais kwa sababu uwezo anao na hana woga wala hamung’unyi maneno pindi anapokuwa akitetea haki za wanyonge.

“Narudia tena, tunamuomba Profesa Muhongo popote alipo na kama anatusikia, muda wa kuchukua fomu ukifika, achukue na sisi tutamuunga mkono kwa sababu tunaamini ana uwezo wa kuiongoza nchi hii,” alisema Kadulo.

Kwa mujibu wa Kadulo, uwezo wa uongozi alioonyesha Profesa Muhongo wakati akiwa Waziri wa Nishati na Madini ni kielelezo kingine kitakachowashawishi Watanzania kumpigia kura za ndiyo pindi watakapotakiwa kufanya hivyo.

“Wakati akiwa pale Wizara ya Nishati na Madini alionyesha uwezo wa hali ya juu kwa kupeleka umeme vijijini pamoja na kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha Watanzania wote.

“Kwa mfano, aliruhusu vijana wa Kitanzania kwenda kusomea masuala ya mafuta na gesi na aliwezesha mikataba kati ya wizara yake na wawekezaji isainiwe hapa hapa nchini kwa manufaa ya Watanzania.
 Haya yote aliyafanya kwa sababu ana uchungu na nchi hii, ingawa baadaye alianza kupigwa vita na baadhi ya watu waliokuwa wakiitumia wizara hiyo kujinufaisha wao,” alisema.

Kabla ya kukumbwa na sakata la Escrow, Profesa Muhongo alihusishwa na mbio za kuwania ubunge katika Jimbo la Musoma Vijijini.

Harakati zake hizo zinadaiwa kusababisha mvutano mkubwa baina yake na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Nimrod Mkono.

Ni mazingira hayo hayo ya kuwania Jimbo la Musoma Vijijini ndiyo yanahusishwa na uamuzi wa Profesa Muhongo wa kuvunja mkataba uliokuwapo baina ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na kampuni ya kusimamia masuala ya kisheria ya Mkono & Co Advocates.

Hata hivyo, kufuatia kuwapo kwa mashinikizo ya muda mrefu ya kutaka ajiuzulu baada ya kuhusishwa na sakata la uchotwaji wa mabilioni ya fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, Profesa Muhongo aliamua kujiuzulu wadhifa wake wa uwaziri wa Nishati na Madini na kubaki katika nafasi yake ya ubunge wa kuteuliwa.

Kitaeleweka tu Chadema Mbeya yasema mwisho wa CCM Oktoba


Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi
Na Lauden Mwambona, Mwananchi

Mbeya. Mwenyekiti wa Chadema mkoani hapa, Joseph Mwachembe maarufu kwa jina la China amesema chama chake hakina ndoto ya kuwapo kwa serikali ya mseto awamu ya tano ya uongozi wa nchi, kwa vile kimejiandaa kushinda kuanzia ngazi ya uis, ubunge hadi udiwani .

China alisema Chadema inaamini kwa niaba ya Watanzania kwamba mwisho wa utawala wa CCM ni Oktoba mwaka huu, hoja za baadhi ya watu kwamba CCM ikikosa wabunge wengi ikubali kuunda serikali ya mseto ni propaganda za wafuasi wa CCM.

Alitoa kauli hiyo alipoulizwa maoni ya chama chake kuhusu taarifa kwamba upinzani watapata wabunge wengi, lakini rais atatoka CCM katika uchaguzi ujao na kuishauri CCM ijiandae kuunda serikali ya mseto.

Hivi karibuni mwanasiasa mstaafu Kanali Edmund Mjengwa (68) aliishauri CCM iwe na mawazo ya kujiandaa kuunda serikali ya mseto ikiwa rais atatoka CCM na wabunge wengi ndani ya Bunge wakawa ni wa upinzani.

Naye Mbunge wa zamani wa Musoma Vijijini, Paul Ndobho alitoa kauli kama hiyo alipozungumza na mwandishi wetu Kanda ya Ziwa.

Akifafanua hoja zake jana, China aliwasihi Watanzania kushika moja la kuwachagua wagombea wa chama kuanzia rais hadi madiwani ili kuundwa kwa serikali itakayofanya kazi kwa uhakika zaidi .

Alisisitiza kwamba Chadema itashinda kwa wingi viti vya udiwani, ubunge na urais na kwamba hawana ndoto za kuwapo kwa mseto.

Naye Mwenyekiti wa CUF mkoani hapa Yassin Mrotwa akitoa maoni yake alisema CUF ina uhakika kwamba CCM imefika kikomo kwa sababu Watanzania wamechoshwa na ufisadi uliopo serikalini.

Wafanyakazi wamechoshwa na kukopwa fedha zao kupitia mishahara hata mifuko ya hifadhi, wakulima wamechoshwa kukopwa mahindi na mpunga,” alisema na kuongeza: “Kibaya zaidi ni kwamba CCM haina mgombea safi na makini.”

Mrotwa alisema mazingira ya chama chake kushinda urais ni makubwa kuliko hesabu za wabunge na madiwani na kwamba kinachotakiwa ni CCM kujiandaa kukabidhi madaraka kwa utulivu.

Kuhusu maoni ya kuwapo kwa serikali ya mseto, alisema haiwezekani kwa vile katiba iliyopo na hata inayopendekezwa haijaruhusu kuwapo kwa serikali ya aina hiyo. 
Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM mkoani Mbeya, Bashiru Madodi alipoulizwa maoni yake kuhusu suala hilo alisema chama chake hakina ndoto ya kuwapo kwa serikali ya mseto kwani kitapata ushindi wa kishindo kuanzia madiwani, wabunge hadi rais.

Madodi alisema CCM imejipanga kuwakata ngebe wapinzani kwa kuwapoka baadhi ya majimbo na kwamba imejipanga haina wasiwasi.

Aangusha ng’ombe watatu kusherehekea uwaziri...........bofya hapa kuona jinsi sherehe ilivyokuwa


NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage, anadaiwa kuandaa ng’ombe watatu ambao watachinjwa leo kwa ajili ya kusherehekea kuteuliwa kushika wadhifa huo.

Mwijage, ambaye ni Mbunge wa Muleba Kaskazini (CCM), aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika nafasi hiyo Januari 24, mwaka huu, baada ya kufanya mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziri baada ya kuibuka sakata la uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Taarifa ambazo gazeti hili limezipata kutoka eneo la Kamachumu, Muleba ambako mapokezi hayo yatafanyika leo, zinasema kuwa mbali na ng’ombe hao, pia kutakuwa na maakuli ya kila aina.

“Maandalizi yanaendelea, ingawa baadhi ya wananchi wamekataa kushiriki, hali iliyosababisha waandaaji kutumia wanafunzi katika maandalizi hayo, kwa mfano wanafunzi waliotumika kuchagua mchele ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Kamachumu B.

“Lakini pia wamechukua tena wanafunzi wa Sekondari ya Rutabo, ndio walikuwa wanashughulika kufanya usafi na kujenga jukwaa atakalotumia Mwijage kuzungumza na wananchi,” alisema mtoa taarifa wetu huyo kutoka Kamachumu.

Alisema waandaaji wa mapokezi hayo ambao ni viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Kamachumu, walifikia hatua ya kuwatumia wanafunzi baada ya kukosa ushirikiano sehemu mbalimbali.

“Ilifika mahali hadi wakataka kwenda kutoa mahabusu kinyemela ili wawasaidie kufanya usafi na wananchi wamekataa kushiriki kwasababu Mwijage amefiwa na mama yake mdogo aliyemlea hivi karibuni lakini hajashiriki mazishi, sasa watu wanashangaa anajiandalia sherehe ya mapokezi,” alisema mtoa taarifa huyo.

Katika kunogesha mapokezi hayo, miongoni mwa waratibu katika shughuli hiyo ni yule aliyepewa jukumu la kushughulikia magari ambapo amekuwa akipita kwa baadhi ya watu wenye magari ili kuwashawishi washiriki katika mapokezi ya Naibu Waziri huyo.

Baadhi ya wenye magari wamekuwa wakiambiwa kwamba watawekewa mafuta endapo watashiriki kwenye shughuli hiyo.

MTANZANIA Jumamosi liliwasiliana na Katibu wa CCM Kata ya Kamachumu ambaye simu yake iliita bila kupokelewa.

Ofisa Mtendaji Kata ya Kamachumu, George Rugangila, alithibitisha kuwepo kwa maandalizi hayo, lakini alikataa kuzungumza kwa undani kwasababu yeye siyo mhusika mkuu.

Alipoulizwa kuhusu ushiriki wa wanafunzi katika maandalizi hayo, alikiri kuwaona, lakini alidai walikuwa wanakwenda kucheza shule ya jirani.

“Kweli niliona kundi kubwa la wanafunzi wanapita katika eneo hilo, lakini niliona wanakwenda kwenye shule ya jirani ya Ibuga, siyo kweli kwamba walikuwa wanajenga majukwaa,” alisema Rugangila.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Rutabo alipopigiwa simu kuthibitisha taarifa hizi simu yake haikupatikana.

Kwa upande wake, Waziri Mwijage alipotafutwa kwa njia ya simu kupitia ujumbe mfupi wa maneno alijibu kuwa; “Salaam, nipo kwenye kikao Mwanza”.

Pumzi ya mwisho Lowassa, Membe


Dar es Salaam. Wakati makada wa CCM wakivuta pumzi ya mwisho kwa matarajio ya kuondolewa kifungo cha miezi 12 ili wajitose rasmi kuwania urais, Kamati Kuu ya chama hicho inakutana leo kukiwa na habari kuwa itatumia muda mwingi kujadili mwelekeo wa mchakato wa Kura ya Maoni na badala wa wanachama hao sita.

Adhabu ya makada sita wa CCM ya kufungiwa miezi 12 ilishaisha tangu kastikati ya mwezi huu na sasa wanasubiri kwa hamu tangazo la Kamati Kuu la kumalizika kwa adhabu yao ili wawe huru kutangaza nia ya kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho na kuendelea na shughuli nyingine za kujiandalia mazingira ya kupitishwa na Halmashauri Kuu.


Makada hao ni Bernard Membe, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa na Fredrick Sumaye, ambao waliwahi kuwa mawaziri wakuu, William Ngeleja, Steven Wasira, ambaye ni Waziri wa Kilimo na Chakula, na January Makamba, ambaye ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia.


Hadi sasa makada hao, ambao walituhumiwa kuanza harakati za kampeni kabla ya muda, hawajatangaza rasmi nia ya kuwania urais na habari zinasema kuwa wamekuwa kwenye maandalizi ya kufanya hafla kubwa ya kutangaza mpango huo.


Lakini habari ambazo Mwananchi imezipata zinasema kuwa kuna uwezekano mdogo wa Kamati Kuu kuzungumzia suala hilo kwa kuwa kikao hicho kitajikita zaidi kuzungumzia mwenendo wa mchakato wa Kura ya Maoni ambao unaonekana kuyumba.


“Watu wameandika sana kuhusu Kamati kufanya uamuzi wa wagombea urais waliofungiwa, lakini nakuhakikishia suala hilo halitazungumzwa labda iweje sijui,” alisema mpashaji habari wetu aliye ndani ya chama hicho.


“Suala linalosumbua kwa sasa ni Kura ya Maoni na hilo ndilo litachukua muda mwingi.”


Alisema kamati Kuu itatoa mwelekeo wa Kura ya Maoni, ambayo mchakato wake unapingwa vikali na vyama vya upinzani ambavyo vinasema uchache wa vifaa, muda mdogo wa maandalizi, watendaji na matumizi ya teknolojia ya uchukuaji wa taarifa za wapigakura kuwa vinaweza kfanya kazi ya uandikishaji kuchukua muda mrefu na hivyo Kura ya Maoni isipigwe Aprili 30 kama ilivyotangazwa na Rais Jakaya Kikwete.


Kada mwingine wa chama hicho pia aliidokeza Mwananchi kuwa wagombea hao waliofungiwa watabidi kuvuta pumzi zaidi kabla ya kuachiwa huru rasmi.


Mmoja wa wasaidizi wa kada aliyefungiwa alipoulizwa kuhusu mipango ya bosi wake kutangaza rasmi kugombea, alisema: “Sisi tunaisubiri Kamati Kuu tu. Ikitangaza kumalizika kwa adhabu tu, hata wiki ijayo tutatangaza rasmi.”


Alipoulizwa kuhusu kikao hicho cha leo, katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye hakutaka kuzungumzia ajenda.


Hivi karibuni, Nape alithibitisha kuwa muda wa adhabu hiyo ulikuwa ukingoni na kuwa viongozi hao sita wangefanyiwa tathmini na kamati ndogo ya maadili ili kubaini iwapo adhabu hiyo ilitekelezwa ipasavyo.

KINANA AKUTANA NA KAMATI KUU YA CHAMA CHA SPLM CHA SUDANI YA KUSINI


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumzana na Kamati Kuu ya Chama Cha SPLM ambapo alipeleka ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,kikao hicho kilikuwa chini ya 
Mwenyekiti wa chama cha SPLM ambaye pia ni Rais wa Sudan ya Kusini Rais Salva Kiir, Ikulu mjini Juba. Mwenyekiti wa chama cha SPLM ambaye pia ni Rais wa Sudan ya Kusini Rais Salva Kiir akiongoza kikao maalum cha Kamati Kuu ambacho Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alihudhuria.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Rais wa Sudan ya Kusini Rais Salva Kiir mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu cha chama cha SPLM ,kikao hicho kilimalizika usiku wa manane mjini Juba ,Sudan.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao maalum cha Kamati Kuu ya chama cha SPLM mjini Juba,kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa SPLM ambaye pia ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo James Wani.

Ndege ya JWTZ yaanguka, rubani wake ajiokoa kwa parachuti



Ndege ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) baada ya kuanguka katika uwanja wa ndege Mwanza.

Ndege hiyo ambayo ilidaiwa kuwa ni ya kivita na ilikuwa mpya ilianguka saa mbili asubuhi na kuteketea kwa moto, huku rubani wake akinusulika kifo baada ya kuruka kutoka angani kwa kutumia parachuti. 

Mwanza. Hali ya taharuki ilitanda kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza baada ya ndege ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuanguka na kuteketea kwa moto.

Ndege hiyo ambayo ilidaiwa kuwa ni ya kivita na ilikuwa mpya ilianguka saa mbili asubuhi na kuteketea kwa moto, huku rubani wake akinusulika kifo baada ya kuruka kutoka angani kwa kutumia parachuti.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatika uwanjani hapo zilidai kuwa ndege hiyo ilikuwa inaongozwa na rubani ,Peter Augustino Lyamunda.

Waandishi wa habari mkoani hapa walifika kwenye uwanya huo muda mfupi baada ya kutokea kwa ajali hiyo, ambapo baadhi ya maofisa wa JWTZ walikataza wanahabari wasipige picha wala kuripoti kitu chochote kuhusu ajali hiyo. 

Kutokana na kuzuiliwa kwa waandishi wa habari, hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusu ajali hiyo. Gazeti hili jana lilimtafuta Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Esther Madale hakupatikana, lakini baadhi ya maofisa wa uwanja huho ambao hawakutaja majina yao walidai kuwa suala hilo linahusu mamlaka nyingine, na wao hawawezi kulizungumzia.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo naye alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo hakuweza kupatikani kwa kuwa alikuwa kwenye kongamano la viongozi wa dini.

Uwanja wa ndege wa Mwanza umekuwa na matukio kaadha ya ajali za ndege ikiwamo ndege kushindwa kuruka kutokana na hitilafu mbalimbali.
Mwananchi

Pumzi ya mwisho Lowassa, Membe...........soma hapa kilichojiri



Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete akipiga makofi wakati alipowasili katika mkutano wa chama hicho Mjini Dodoma hivi karibuni.

Adhabu ya makada sita wa CCM ya kufungiwa miezi 12 ilishaisha tangu kastikati ya mwezi huu na sasa wanasubiri kwa hamu tangazo la Kamati Kuu la kumalizika kwa adhabu yao ili wawe huru kutangaza nia ya kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho na kuendelea na shughuli nyingine za kujiandalia mazingira ya kupitishwa na Halmashauri Kuu.

Dar es Salaam. Wakati makada wa CCM wakivuta pumzi ya mwisho kwa matarajio ya kuondolewa kifungo cha miezi 12 ili wajitose rasmi kuwania urais, Kamati Kuu ya chama hicho inakutana leo kukiwa na habari kuwa itatumia muda mwingi kujadili mwelekeo wa mchakato wa Kura ya Maoni na badala wa wanachama hao sita.

Adhabu ya makada sita wa CCM ya kufungiwa miezi 12 ilishaisha tangu kastikati ya mwezi huu na sasa wanasubiri kwa hamu tangazo la Kamati Kuu la kumalizika kwa adhabu yao ili wawe huru kutangaza nia ya kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho na kuendelea na shughuli nyingine za kujiandalia mazingira ya kupitishwa na Halmashauri Kuu.

Makada hao ni Bernard Membe, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa na Fredrick Sumaye, ambao waliwahi kuwa mawaziri wakuu, William Ngeleja, Steven Wasira, ambaye ni Waziri wa Kilimo na Chakula, na January Makamba, ambaye ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia.

Hadi sasa makada hao, ambao walituhumiwa kuanza harakati za kampeni kabla ya muda, hawajatangaza rasmi nia ya kuwania urais na habari zinasema kuwa wamekuwa kwenye maandalizi ya kufanya hafla kubwa ya kutangaza mpango huo.

Lakini habari ambazo Mwananchi imezipata zinasema kuwa kuna uwezekano mdogo wa Kamati Kuu kuzungumzia suala hilo kwa kuwa kikao hicho kitajikita zaidi kuzungumzia mwenendo wa mchakato wa Kura ya Maoni ambao unaonekana kuyumba.

“Watu wameandika sana kuhusu Kamati kufanya uamuzi wa wagombea urais waliofungiwa, lakini nakuhakikishia suala hilo halitazungumzwa labda iweje sijui,” alisema mpashaji habari wetu aliye ndani ya chama hicho.

“Suala linalosumbua kwa sasa ni Kura ya Maoni na hilo ndilo litachukua muda mwingi.”

Alisema kamati Kuu itatoa mwelekeo wa Kura ya Maoni, ambayo mchakato wake unapingwa vikali na vyama vya upinzani ambavyo vinasema uchache wa vifaa, muda mdogo wa maandalizi, watendaji na matumizi ya teknolojia ya uchukuaji wa taarifa za wapigakura kuwa vinaweza kfanya kazi ya uandikishaji kuchukua muda mrefu na hivyo Kura ya Maoni isipigwe Aprili 30 kama ilivyotangazwa na Rais Jakaya Kikwete. 

Kada mwingine wa chama hicho pia aliidokeza Mwananchi kuwa wagombea hao waliofungiwa watabidi kuvuta pumzi zaidi kabla ya kuachiwa huru rasmi.

Mmoja wa wasaidizi wa kada aliyefungiwa alipoulizwa kuhusu mipango ya bosi wake kutangaza rasmi kugombea, alisema: “Sisi tunaisubiri Kamati Kuu tu. Ikitangaza kumalizika kwa adhabu tu, hata wiki ijayo tutatangaza rasmi.”

Alipoulizwa kuhusu kikao hicho cha leo, katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye hakutaka kuzungumzia ajenda.

Hivi karibuni, Nape alithibitisha kuwa muda wa adhabu hiyo ulikuwa ukingoni na kuwa viongozi hao sita wangefanyiwa tathmini na kamati ndogo ya maadili ili kubaini iwapo adhabu hiyo ilitekelezwa ipasavyo. 
Mwananchi

MH. AL SHAIMAR KWEIGYIR AMTEMBELEA MAJERUHI WA TUKIO LA UPORWAJI WA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO) N AKUSEMA HAYA



Na Mwandishi Wetu, Mwanza.
Mbunge wa kuteuliwa, Al Shaimar Kweigyir, amtembelea majeruhi wa tukio la uporwaji wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino,Yohana Bahati, aliyetekwa nyara na kukutwa akiwa amekufa. 

Katika ziaraa hiyo kwenye Hospitali ya Bugando jijini Mwanza, Mh Shaimar aliongozana pia na Katibu Tawala Msaidizi wa Ofisi ya Mkoa wa Mwanza, Crencencia Joseph na August Tesha, ambaye ni Meneja wa Bayport Financial Services mkoani Mwanza.
Wakiwa Hospitali ya Bugando, Mbunge Shaimar na alioambatana nao alipata fursa ya kuzungumza na wahudumu katika wodi aliyolazwa Ersther ambaye ni wa Yohana na kumfariji katika kipindi kigumu cha kuuguza majeraha yake pamoja na kulia msiba wa mwanae. 

Tukio la utekaji na uporwaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi limezidi kushika kasi, ambapo kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau, hususan wale wenye ulemavu wa ngozi wakiamini kuwa serikali imeshindwa kuwapatia ulinzi wa kutosha. 

Akiwa jijini Mwanza, Mbunge Shaimar na taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services watakuwa kwenye safari ya kuelekea wilayani Kwimba kwa ajili ya kwenda eneo alilokuwa akiishi Ester na watoto wake, hususan wawili kati ya watano waliobaki wakiwa ni albino.

Mbunge wa kuteuliwa Shaimar Kweigyir katikati akiwa na bibi wa Yohana Bahati (Tabu Maganiko) kulia ambaye ni mlemavu wa ngozi aliyeuawa hivi karibuni mkoani 
Mwanza, huku mama yake akiachwa na majeraha makubwa wakati wanagombania mtoto katika tukio hilo la kusikitisha. Kushoto kwake ni Mweka Hazina wa Chama Cha Albino Tanzania Abdullah Omari.

Katibu wa Mheshimiwa mbunge, Semeni Kingalu, kulia akipiga picha wakati walipomtembelea majeruhi Ester Maganiko, ambaye mtoto wake Yohana Bahati mwenye ulemavu wa ngozi aliuliwa katika tukio hilo la kusikitisha. Anayefuata ni Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Bugando na Clencencia Joseph, Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.

DC Paulo Makonda Kufikishwa Mahakamani kwa Udhalilishaji.........bofya hapa kuona jinsi anavyopandishwa kizimbani


Viongozi wawili wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wanakusudia kumfikisha mahakamani Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, Jumatatu ijayo kwa madai ya kuwakashifu, kuwadhalilisha na kuwatukana.

Viongozi hao ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai.

Akisoma kusudio hilo jana mbele ya waandishi wa habari kwa niaba ya mwenzake, Guninita alisema. 

Makonda hakustahili kuteuliwa kushika wadhifa huo kwa kuwa hana maadili ya kuwa kiongozi.

Alisema cheo alichonacho ni cha uyoga ndio maana amekuwa akitukana watu bila sababu za msingi.

“Sifa ya mtu kuchaguliwa ni lazima awe mnyenyekevu, awe na adabu ya kuzaliwa na siyo ya photocopy na awe anaheshimu watu hivyo wenye vyeo vya uyoga hawana sifa hizo,” alisema Guninita.

Alisema alipofikia Makonda, wameshindwa kumvumilia hali ambayo wametaka haki zao kuzipata kupitia mahakama kwa kuwa chama kinaendelea kumlinda.

Alisema hawana ugomvi na Makonda lakini wanamshangaa amekuwa akiwatukana kila wakati kwa kuwaita ni vibaraka wa CCM na kuwataka waondoke kwenye chama.

Alisema alishaandikiwa barua na mwanasheria wake, Benjamini Mwakagamba, ya kumtaka aombe radhi dhidi ya kauli zake na matokeo yake amegoma na kueleza kuwa alitumwa na chama.

“Waliomshauri rais kumchagua awe mkuu wa wilaya hawakuwa sahihi na kama ningekuwa nina uwezo ningetengua hivi ni mtu gani unawatukana viongozi wa dini halafu leo hii unafanyaje nao kazi,” alihoji.

Guninita alisema alitegemea kama kuna kosa amelifanya angeitwa na badala ya kutukanwa na kukashfiwa na kijana huyo ambaye alidai amempita umri na vyeo.

Alisema Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) unatumika kuwatukana viongozi wakati dhana yake ni kuandaliwa kuwa viongozi wenye maadili.

“Huyu kijana hana maadili ukiachilia mbali kutukashifu alishawahi kumshambuliwa Jaji Warioba...Alishawahi kumpiga Jaji Warioba eti alijitetea alikuwa anamlinda. Je huyu Makonda ana mkataba wa kumlinda jaji Warioba,” alihoji

Guninita alisema Makonda aliwahi pia kuwatukana viongozi wa dini lakini waliamua kukaa kimya huku wakimuombea aendelee kuwa na uhai ili wapambane na Makonda mahakamani.

Alisema Makonda amekuwa akibebwa na kulindwa na viongozi wa CCM wakimtetea, lakini mahakama ni chombo ambacho kitamtenda haki. 

Alisema chama kimefikia sehemu mbaya kuwapo na matabaka ya watu kupewa vyeo kama uyoga ndiyo maana wanakuwa na jeuri kwa watu. Alisema tabaka hilo ndilo linalosababisha kuwapo na mgogoro ndani ya chama.

Alisema Jumatatu wataenda mahakamani kuandaa hati ya mashtaka na hivi sasa wanaandaa mchanganuo wa fidia atakayotaka kulipwa.

Alisema Mwenyekiti wa Chama ambaye ni Rais Jakaya Kikwete anaheshima kubwa ya kushughulikia migogoro mbalimbali ya nje ya nchi, hivyo wakati umefika wa kushughulikia migogoro iliyopo ndani ya chama.

Pia alisema kitendo cha Makonda kuwataka wajiondoe kwenye chama alieleza kuwa hawatatoka kwa kuwa wamewekeza kwa zaidi ya miaka 40 ndani ya CCM.

Alisema kama anataka watoke ndani ya chama awalipe fidia la sivyo wao wanauwezo wa kumlipa fidia kwa miaka mitatu ambayo amekitumikia chama.

Mwanasheria anayewawakilisha viongozi hao Benjamini Mwakagamba, alisema wateja wake watafungua kesi Jumatatu dhidi ya Makonda ya udhalilishaji.

Alisema awali alishaandikiwa barua na kutakiwa kuomba radhi, kuacha kuwazungumzia viongozi hao pamoja na kulipa fidia ya Sh milioni 100.

Alisema barua hiyo aliijibu na kueleza kuwa alifanya hivyo kwa maelekezo ya chama.

Tibaijuka atibua hasira za wananchi.............kwa habari zaidi soma hapa


KAULI iliyotolewa na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, mbele ya Baraza la Maadili lililoketi kumhoji juu ya mgawo wa fedha za Escrow, kuwa alitumia Sh milioni 10 kwa ajili ya kununulia mboga, imeibua hasira kutoka kwa wananchi, wasomi na viongozi wa kada mbalimbali.

Wamesema kauli hiyo ni mwendelezo wa kejeli ambazo zimewahi kutolewa kwa nyakati tofauti na wanasiasa pamoja na baadhi ya viongozi nchini.

Kauli zinazolinganishwa na hii ya sasa ya Tibaijuka kiasi cha kuzua mijadala mikubwa kwenye maeneo mbalimbali, ni zile za hivi karibuni zilizowahi kutolewa na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge na aliyekuwa mmiliki mwenza wa Kampuni ya IPTL, James Rugemalira, ambao kwa nyakati tofauti wamepata kuyaita mabilioni yao vijisenti na vijipesa vya ugoro.

Kauli hiyo ya Tibaijuka imeelezwa kuwa ni dharau na dhihaka iliyokosa kipimo kwa Watanzania ambao asilimia 40 wanaishi kwa mlo mmoja kwa siku.

Kwenye mitandao ya kijamii kama WhatsApp, Instagram, facebook, twitter, blog na mingine, wamehoji kama milioni 10 ni fedha za mboga, kijijini anakotoka Tibaijuka mwenyewe migomba imekufa kwa ugonjwa na mnyauko, huku watu wakiteseka kwa njaa na wengine wakikosa hata Sh 1,000 kwa siku.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliozungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, walisema kauli hiyo haipimiki katika mzani wa maisha ya kawaida ya Watanzania.

Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu, Hellen Kijo Bisimba, amesema kauli ya Profesa Tibaijuka ni dharau iliyopita kiwango na inadhihaki asilimia 40 ya Watanzania wote ambao wanaishi chini ya dola moja.

Alisema kauli za namna hiyo ni za kukatisha tamaa wananchi wazalendo ambao wanatumia nguvu yao kubwa kujenga uchumi wa nchi.

“Watu wa namna hii hawajitambui wapo katika kundi gani la jamii wanayoiongoza, hawana uchungu na wavuja jasho na wanadharau kupita kiasi, eti unatumia Sh milioni 10 kwa ajili ya mboga na wakati mwananchi mwingine hana hata Sh 500 ya kumwezesha apate walau mlo mmoja kwa siku,” alisema Dk. Bisimba.

Dk. Bisimba alikwenda mbali kwa kueleza kuwa hata uamuzi ya Baraza la Maadili unaweza kuwa dhaifu kwa sababu haoni sehemu itakayowabana watuhumiwa ili warejeshe fedha walizopewa.

“Ninachokiona au ninachokitarajia juu ya hukumu ya Baraza la Maadili ni sawa na bure, kwa sababu watuhumiwa hawana kazi kwamba watafukuzwa na sidhani kama Baraza la Maadili lina ubavu wa kutengua ubunge wao, ndiyo maana Chenge anawachezea kama watoto wadogo,” alisema Dk. Bisimba.

Kauli hiyo iliungwa mkono na mwanasheria mmoja ambaye hakupenda jina lake kutajwa gazetini, ambaye alisema japokuwa baraza hilo lina nguvu ya kisheria, lakini halina meno ya kuwakabili watuhumiwa hao.

Pasipo kutoa ufafanuzi wa kina wa kisheria, mwanasheria huyo alisema hukumu ndiyo itakayotanabahisha mitazamo iliyopo kuhusu nguvu ya baraza hilo.

Awali mwanasheria huyo aliizungumzia kauli ya Profesa Tibaijuka kwa kusema kuwa ameyatusi maisha ya Watanzania.

“Angekuwa huko Umoja wa Mataifa kauli yake isingewaudhi wengi kwa sababu alikuwa anaishi na watu wa hadhi yake, lakini kama kiongozi wa wananchi ambao wengi wao ni maskini wa kutupwa, kauli hiyo haistahili na kama Baraza la Maadili litakuwa makini limbane kupitia kauli hiyo,” alisema mwanasheria huyo.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, alisema kauli aliyotoa Profesa Tibaijuka ina uasili wa hasira.

Alisema, kwa kuwa mara nyingi wanasiasa wamekuwa wakihukumiwa kabla ya hukumu, mazingira hayo huwajengea hasira, hivyo hujikuta wanatoa kauli mbaya pasipo kutarajia.

“Ukiziweka kwenye mzani kauli ya Chenge, Profesa Tibaijuka na hata ya Rugemalira ambaye ni mfanyabiashara, utabaini kuna kihasira fulani na mazingira ya kauli yao yanatokana na kuhukumiwa kabla ya hukumu, lakini ombi langu ni moja tu, kwamba wanasiasa wanatakiwa wawe wavumilivu, nadhani Lowassa hata Chenge wameonyesha uvumilivu wa kisiasa baada ya kukumbwa na kashifa nzito na zimedumu kwa muda mrefu midomoni mwa watu,” alisema Dk. Bana.

Akitoa mtazamo wake kuhusu Baraza la Maadili, Dk. Bana alisema bado hajaelewa ukomo wa mamlaka ya mwenyekiti wa Baraza la Maadili, hivyo hali hiyo inampa wakati mgumu wa kuzungumzia jambo hilo.

“Napata shida kidogo kujua ukomo wa mamlaka ya mwenyekiti wa Baraza la Maadili, najiuliza kama watuhumiwa watakutwa na hatia ubunge wao utatenguliwa? Je, kama wakitengua vyama vyao au wananchi wataridhia? Hapa ndipo ninapojiuliza kuwa inawezekana nguvu ya Baraza la Maadili si kubwa,” alisema Dk. Bana.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa, alikataa kuzungumzia kauli ya Tibaijuka kwa kusema kuwa haina mashiko katika mustakabali wa Taifa.

“Siwezi kuzungumzia kauli ya mtu wakati kuna ajenda nyingi za kuzungumzia Taifa, binafsi nasubiri hukumu ya Baraza la Maadili,” alisema Dk. Slaa.

Baadhi ya wananchi walipiga simu chumba cha habari kuzungumzia kauli hiyo ya Tibaijuka.

Miongoni mwa wananchi hao ni pamoja na Victor Kabalasa, aliyesema ameshangazwa na kauli hiyo ya Tibaijuka, wakati yeye hiyo milioni 10 hajawahi kuishika hata siku moja tangu azaliwe na sasa ana miaka 43.

Mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la William Kangesha, alisema wakati Tibaijuka akitoa kauli hiyo, kuna watoto wengi wa Kitanzania na Watanzania kwa ujumla wanakufa mahospitalini kwa kukosa matibabu sahihi.

Zaidi alisema wapo mamilioni ya watoto wa Kitanzania ambao mbali na kutokuwa na sare za shule wanatembea peku, wanakaa katika madarasa yasiyo na madawati, dirisha wala milango.

Kauli za kejeli
Mbali na kauli hiyo ya Tibaijuka, kauli nyingine za kejeli zilizopata kutolewa na viongozi na ambazo zimebaki katika vichwa vya Watanzania ni pamoja na ile iliyowahi kutolewa na Rugemalira kwa kusema kuwa alilipwa vijipesa vya ugoro.

“Niliiambia serikali kuwa nyie mmeibiwa na sisi tumeibiwa. Mimi nikawaambia kuwa ‘the end justify the means’ (jambo la muhimu ni matokeo, si njia ulikopitia), mwisho tulikubaliana kwamba kwa masilahi ya Taifa tumalize kesi hii, na mimi ndiyo nikalipwa hivyo vijipesa vya ugoro,” alikaririwa Rugemalira.

Mwaka 2008, aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, alihojiwa na waandishi wa habari juu ya tuhuma nzito za kumiliki kiwango kikubwa cha fedha kinachokadiriwa kuzidi dola za Marekani milioni moja, katika akaunti iliyoko Kisiwa cha Jersey, Uingereza, ambapo alijibu kwa kifupi kwamba fedha hizo kwa viwango vyake zilikuwa ni vijisenti.

Mwingine aliyewahi kutoa kauli ya kejeli ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ambaye alisema kwamba kama kuna watu watashindwa kulipa nauli ya Sh 200 katika kivuko cha Kigamboni, itabidi apige mbizi.

Aliyekuwa Waziri wa Fedha wa awamu ya tatu, Basil Mramba, naye aliwahi kutoa kauli iliyokera wengi pale aliposema ununuzi wa ndege ya rais ni lazima, hata kama wananchi watakula nyasi.

Miaka ya 1980, John Malecela wakati akiwa Waziri wa Mawasiliano, alitoa kauli ya kejeli akiwa jimboni kwake kwa kusema kwamba, waliokuwa wanahoji ufanisi wa Shirika la Reli (TRC), waende kuzimu.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...