2015-02-17

Ina huzunisha sana:Awekwa mbaroni kisa kumuua baba yake............bofya hapa kuona jinsi alivyokuwa akimuua baba yake


           Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime.

Mkazi wa Kitongoji cha Nyamorege kilichopo Mtaa wa Forodhani mji mdogo wa Sirari Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Marwa Kihiri Mwita, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi Kihiri Mwita kinyama kwa kumpiga na koleo kichwani na ubavuni.

Vilevile inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alijeruhiwa kwa kucharangwa kwa panga na baba yake huyo kabla ya kumjeruhi kwa kumpiga na koleo kichwani na ubavuni baada ya kuzuka ugomvi baina yao.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Forodhani Sirari, Nyangoko Paulo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo Ijumaa ya wiki iliyopita jioni katika kitongoji hicho.

Paulo alisema kuwa ugomvi huo uliibuka baada ya baba kumtuhumu mwanaye kuwa anatabia ya wizi.

Alisema inadaiwa kuwa baba huyo alimweleza mwanaye huyo kuwa aliwahi kufanya wizi kitendo kilichosababisha kutozwa faini ya ng'ombe.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...