Katika kukabilina na matukio ya mauaji na ukatwaji viungo vya watu wenye
ulemavu wa ngozi 'Albinisim' ambayo yameanza tena kushika kasi mwishoni
mwa mwaka jana serikali imepiga marufuku wapiga ramli ikiwa ni pamoja
na kuunda kikosi kazi kwa ajili ya operesheni maalum ya kuwasaka
watuhumiwa.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh Mathias Chikawe ameyasema hayo
jijini Dar es Salaam ambapo amekiri kuongezeka kwa matukio hayo tangu
mwishoni mwa mwaka jana na kuongeza kuwa timu hiyo itaundwa na watu
sita, wawili kutoka chama cha Albinisim Tanzania na wanne jeshi la
polisi na wataanza na mikoa mitano ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Tabora
na Geita na baadaye Sumbawanga, Kagera na Mbeya.
Akijibu maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari likiwemo la
malalamiko ya ucheleweshwaji wa kesi pamoja na watuhumiwa kuachiwa bila
kufikishwa mahakamani Mh Chikawe amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kudai
kuwa linatokana na msongamano wa kesi zilizopo mahakamani na kuongeza
kuwa kwa sasa wameanza mkakati ya kuzipa kipaumbele kesi ambazo
zinaigusa jamii moja kwa moja.
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye Albinisim nchini Bw Ernest Kimaya
amesema katika kukabiliana na tatizo la ucheleweshwaji wa kesi pamoja na
watu wanaoachiwa huru kwa kisingizio cha kukosa ushahidi wa kutosha
chama hicho kinatafuta udhamini kutoka mataifa ya nje ili wapate fedha
za kuendesha kesi kwani hadi sasa kesi zilizofanyiwa kazi ni tano tu
kati ya kumi na moja.
0 comments:
Post a Comment