2015-02-24

MFANYABIASHARA APIGWA...RISASI NA KUUWAWA PAPO KWA HAPO


MFANYABIASHARA wa Kisesa wilayani Magu, Mwanza, Nestory Andrew ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi usiku wa Februari 16, mwaka huu huku mke wake akishuhudia. 


Mke wa mfanyabiashara huyo (kulia) akiwa na simanzi kubwa.

Imedaiwa kuwa kabla ya majambazi hao hawajafanya mauaji hayo, waliuteka Mtaa wa Kisesa kwani jirani na duka la mfanyabiashara huyo kulikuwa na mafundi baiskeli ambao walizuiwa kupiga kelele na wauaji hao.

“Tukio hili lilitisha kwa sababu lilitokea mita kama 55 kutoka kituo cha polisi na hawakutoa msaada wowote,” alisema shuhuda mmoja.
Akisumulia tukio hilo, mfanyakazi wa marehemu aitwaye Emmanuel Kulwa alisema bosi wake huyo alifika dukani saa mbili usiku ghafla wakati analifunga duka aliona mtu akiwa amevaa koti jeusi ambaye alipiga risasi kadhaa hewani, yeye akakimbia. 


             Nestory Andrew enzi za uhai wake.

“Baada ya hali kutulia nilirudi dukani nikakuta bosi wangu ameshauawa na mwili wake ukiwa umepelekwa Hospitali ya Mkoa Sekeoture,” alisema.
 Mke wa marehemu, Sara Limbu alisema alishuhudia tukio hilo la kuuawa mume wake baada ya kushuhudia risasi zikirindima eneo la tukio. 
“Nilikimbia lakini nilirudi dukani baadaye na kumkuta mume wangu ameshafariki kwa kupigwa risasi mbili kifuani… ameniachia watoto sita. Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake,” alisema mama huyo.
 
GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...