2015-02-24

AMANDA AZIDIWA, ASHINDWA KUMZIKA MEZ B............bofya hapa kuona jinsi alivyozidiwa



MREMBO kunako tasnia ya filamu Bongo, Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’ ameshindwa kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Moses Bushagama aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani Dodoma kutokana na kuugua ghafla. 



Mrembo kunako tasnia ya filamu Bongo, Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’.

Akizungumza na Uwazi kwa masikitiko, Amanda ambaye pia ni mtu wa karibu na marehemu, alisema kuwa alishapanga kusafiri kwenda Dodoma kwa ajili ya maziko lakini kitendo cha kuugua ghafla kimeharibu kila kitu.
 “Imeniuma sana kwa sababu ya ugonjwa wa taifodi kuniandama ambapo nilikuwa nikitapika mfululizo,” alisema Amanda.
Mez B alikuwa akiumwa ugonjwa wa homa ya mapafu, alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mwananchi kabla ya umauti kumkuta. Amezikwa Jumatatu katika makaburi ya Wahanga mkoani Dodoma.
GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...