2015-02-12

Hukumu ya Nahodha wa meli iliyozama karibu na ufuko Itali, Costa Concordia afungwa jela

Capt.Francesco Schettino ahukumiwa miaka 16 jela

Nahodha wa meli ya Costa Concordia iliyosababisha vifo vya watu watu 32 wakiwemo wafanyakazi wa meli hiyo amehukumiwa kwenda jela.
Meli ya Costa Concordia ikiwa imelala ufukoni
Kwa mjibu wa hukumu hiyo Nahodha huyo atatumikia kifungo cha miaka 16 jela baada ya kubainika kuwa na makosa ya kuua bila kukusudia.

Francesco Schettino hakuwepo Mahakamani wakati hukumu hiyo ikitolewa. Miaka mitatu iliyopita Meli hiyo ya Costa Concordia iligonga miamba karibu na pwani ya Giglio nchini Italia na kusababisha vifo hivyo.

Hata hivyo Schettino bado anafursa ya kuweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
bbc swahili

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...