2015-02-28

NI SHIDAAAAAA JACK DUSTUN : NAISHI NA MCHUMBA KUJIANDAA NA NDOA



MAMBO vipi mtu wangu wa nguvu, kama ilivyo ada, tunasonga mbele na tunazidi kukuletea vitu ambavyo roho yako inapenda, kazi yangu ni kutia miguu nyumbani kwa mastaa mbalimbali Bongo na kujua maisha yao halisi.

Jacqueline Dustan.

Leo tumetembelea maeneo ya Mbagala Chamazi katika nyumba anayoishi staa wa Shindano la Maisha Plus Season 2, Jacqueline Dustan ‘Jack’.

Kwenye nyumba hiyo anaishi na mchumba wake aitwaye Hamis, amefunguka mambo mengi, twende pamoja:
Mpaka Home: Mambo vipi Jack mzima? Vipi hapa ni kwako au kwenu na mumeo mtarajiwa?
Jack: (kicheko) Hapa ndiyo nyumbani kwetu, naishi na mume wangu mtarajiwa. Tunaanza kujifunza jinsi ya kuishi pamoja, ndoa haipo mbali.
Mpaka Home: Haya ukiamka cha kwanza unapenda kufanya nini?
Jack: Cha kwanza kabisa nikiamka naanza kusafisha mwili wangu na ninaandaa maji kwa ajili ya Mr (Hamis) na baada ya hapo ndiyo tunapata kifungua kinywa.
Mpaka Home: Hapa naona kuna mashine za nguo zaidi ya tatu, sasa mtarajiwa wako atajuaje kama unajua kufua jinzi kwa mikono yako mwenyewe?
Jack: Siyo kila siku nafulia mashine kuna wakati mwingine naamua kufua kwa mikono yangu.
Mpaka Home: Mastaa wengi wanapenda kukaa maeneo ya Sinza, Kijitonyama vipi wewe kwa upande wako?
Jack: Mimi huwezi amini napenda sana huku niliko, naepuka vitu vingi sana na ninafurahi kweli kama kuna kitu nahitaji huko naenda kufuata na kurudi kwangu.
Mpaka Home: Vipi kuhusu mambo ya jikoni unayamudu au kichenipati ilikupiga chenga?
Jack: Nafikiri hata mpenzi wangu anaweza kukuambia hilo mimi kwa jikoni ni hatari hata yeye hawezi kula chakula ambacho sijapika mimi.
Mpaka Home: Ulisafiri kwa muda mrefu, mpenzi wako alikuwa anakula wapi?
Jack: Kwa kipindi nilichosafiri, alilazimika kula hotelini lakini nikiwa naye kama hivi hathubutu.
Mpaka Home: Unapenda kulala muda gani?
Jack: Napenda kulala mapema kwa sababu napenda sana usingizi na ninapenda kuamka mapema kama saa moja hivi kwa ajili ya usafi wa nyumba nzima halafu nalala tena kidogo.
Mpaka Home: Wageni gani unapenda waje nyumbani kwako?
Jack: Sichagui mgeni wa kuja ili mradi aje kwa mema tu.
Mpaka Home: Ni kitu gani kinachokuvutia hapa nyumbani kwako?
Jack: Kitanda changu tu, nakipenda sana.
Mpaka Home: Kwa upande wa chakula, unapendelea nini zaidi?
Jack: Napenda sana wali maini na samaki hivyo mara nyingi havikosi katika ratiba yangu ya chakula.
Mpaka Home: Nyumba yako unapenda ionekaneje?
Jack: Nyumba yangu napenda ionekane safi wakati wote.
Mpaka Home: Nashukuru sana Jack.
Jack: Karibu sana.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...