Ofisa uandikishaji katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura, Alen Simon (kulia) akichukua taarifa muhimu za wakazi wa Mangula, Makambako waliojitokeza kujiandikisha katika kituo cha Kata ya Mjimwema jana. Picha na Shaban Lupimo.
Na Shaban Lupimo na Fidelis Butahe, Mwananchi
Njombe/Dar. Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapigakura kwa kutumia mfumo wa teknolojia ya kisasa wa BVR (Biometric Voter Registration), umeanza kwa kusuasua na kasoro nyingi.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) jana ilianza kuandikisha wakazi wa mji mdogo wa Makambako, ambapo kwa kasoro hizo wakazi wake walilazimika kuiomba Nec kuongeza maofisa na vitendea kazi ili kuwezesha shughuli hiyo kukamilika ndani ya muda uliopangwa.
Gazeti hili lilitembelea vituo vilivyopo kata ya Mjimwema, Ubena na Lyamkena na kushuhudia umati mkubwa wa watu ukiwa katika foleni kwa ajili ya kujiandikisha, kadri muda ulivyozidi kwenda baadhi waliamua kurejea majumbani mwao huku wakieleza kuwa foleni ni kubwa kuliko kasi ya shughuli yenyewe.
Uandikishaji huo ulianza jana kwenye vituo 87 katika kata 11 za halmashauri hiyo na utazinduliwa leo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Wakati wananchi wakitoa kauli hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Bara John Mnyika aliyepiga kambi katika mji huo kuhamasisha wananchi kujiandikisha, amegundua udhaifu mkubwa wa uandikishaji katika vituo mbalimbali na kuitaka Serikali kutoa kauli juu ya kasoro hizo.
Akizungumza na gazeti hili mkazi wa mji huo, Alen Fungo alisema, “Nimefika hapa tangu asubuhi lakini mpaka sasa (saa 9 alasiri) bado sijajiandikisha. Hapa Makambako watu wengi ni wafanyabiashara hawawezi kukaa muda mrefu katika foleni. Foleni hii haiwezi kupungua leo (jana) wala kesho (leo).”
Elisia Mgeni alisema uandikishaji unasuasua kutokana na Nec kuwa na maofisa wachache, “eneo la uandikishaji wameweka mtu mmoja na eneo la upigaji picha wameweka mtu mmoja . Ilitakiwa wawepo maofisa wawili kila eneo ili kuharakisha uandikishaji.”
Kauli ya Mgeni iliungwa mkono na mkazi mwingine wa mji huo, Tumaini Mbinda ambaye pamoja na mambo mengine alisema kwa jinsi anavyofahamu tabia za wananchi wa Makambako ni vigumu kukaa muda mrefu katika foleni huku akiitaka Nec kutafuta mwarobaini wa kero hiyo.
Hata hivyo, baadhi ya maofisa wa watendaji wa Nec waliliambia gazeti hili kuwa uandikishaji unafanyika taratibu kwa sababu mashine za kuchukua alama za vidole kuwa na tatizo.
“Uandikishaji unakwenda vizuri ila kuna changamoto chache, mfano hizi mashine za kuchukua alama za vidole zinasumbua. Pamoja na hayo kazi itafanyika, “alisema Alen Simon ambaye yupo kituo cha Mangula mjini Makambako.
Katika hatua nyingine, Mnyika ambaye yuko mjini Makambako alieleza kushangazwa na hali aliyoikuta katika kituo cha Malombwe na Liamkena ambapo mpaka jana saa 6 mchana mashine zilikuwa hazifanyi kazi, huku watu wengi wakisubiri kuandikishwa. “Watu ambao vidole vyao
vimekomaa kutokana na kufanya kazi ngumu mashine zimeshindwa kusoma alama zao za vidole na wamekataliwa kujiandikisha. Hali hii imetokea katika kituo cha Sigfrid, Malombwe
0 comments:
Post a Comment