Mmoja wa wataribu wa kongam, ano hilo kutoka FPTC, Lucas Mhenga akiwa na wadau.
Baadhi ya waandaaji wa kongamano hilo wakiwa kwenye kikao kilichofanyika ndani ya ukumbi uliopo Luther House, Posta jijini Dar cha kufanikisha tukio hilo.
Magreth Malunda (kushoto) kutoka kitengo cha watu wenye ulemavu, Wizara ya Afya akiwa na Agnes Shemela kutoka FPCT idara ya wanawake.
Kulia pichani ni Mchungaji Oscar Kindole wa City Church FPCT Buguruni akiwa na mdau.
Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania ‘FPCT’ kwa kushirikiana na taasisi za kuhudumia watu wenye elemavu kutoka Sweden, FUB na ERIKS Development kupitia Mradi wa Pamoja (Come Together Project) wameandaa kongamano kubwa la kimataifa katika Viwanja vya Karemjee, Dar es Salaam.
Mmoja wa waratibu kutoka FPCT, Lucas Mhenga ameuambia mtandao huu kuwa, kongamano hilo litafanyika Machi 6, mwaka huu na litashirikisha watoto na vijana wenye ulemavu kutoka Tanzania, Sweden na Rwanda huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Pinda.
Mhenga alisema kuwa, kauli mbiu itakuwa ni; ‘Vijana wenye ulemavu wapaza sauti juu ya elimu kwa wote’.
“Ni kongamano kubwa la kimataifa litakaloanza Machi 3 na kilele chake kitakuwa Machi 6 mwaka huu pale katika viwanja vya Karemjee, Waziri Pinda atakuwepo pamoja na viongozi mbalimbali wa dini, siasa na taasisi mbalimbali. Tunachoomba ni wadau kujitokeza siku hiyo ili kuungana na walemavu ambao wanastahili kuangaliwa kwa jicho la tatu ili nao waweze kuishi maisha mazuri,” alisema Mhenga.
Akilizungumzia Kanisa la FPCT, Mhenga alisema limekuwepo nchini tangu mwaka 1932 na licha ya huduma za kiroho limekuwa likitoa huduma kwa jamii kupitia miradi ya maendeleo ipatayo 56 nchini kote ikiwa ni pamoja na huduma kwa watu wenye ulemavu tangu mwaka 1963.
Mpaka sasa kanisa hilo lina vitengo vitano vya masuala ya ulemavu vilivyopo Tanga, Korogwe, Arusha, Nzega na Tabora mjini.

0 comments:
Post a Comment