Haya ndio maoni ya mrembo na staa wa Bongo Movies, Faiza Ally juu ya sanaa ya uigizaji hapa Bongo, ususani vipaji vipya.
“Kama wasanii wa kuigiza filamu wangekua kweli wako kisanaa na wanapenda kazi zao basi naamini vipaji vingeongezeka mara dufu lakini tatizo wakisha pata mabwana tu na kununuliwa magari wanasahau kabisa .
Kazi zao wanakua sio wabunifu tena - ubunifu wao unakua kugawana wanaume- kubadilisha nywele- nguo mwisho wa siku wana shuka katika uigizaji.
Kazi zao unakuta katika movie kabadilisha nguo ishirini na viatu lakini ukiangalia katika kuigiza ni yule yule na pengine ujinga umezidi maana stori hazieleweki kazi mbaya basi ili mradi tu na mbaya zaidi wanawake kwa wanaume wanapeana kazi wenyewe kwa wenyewe tu ndio maana hakuna changamoto .
Mimi nashangaa hata marekani wangekua wanapeana kazi wasanii wachache basi kusingekua na mastaa wengi lakini huku mastaa hawafiki hata kumi halafu kila siku wana kazana wanataka kunyayua vipaji kha! sasa mtanyanyuaje Kama hamtoi nafasi ??? nauliza ?”-Faiza alimaliza kwa kuhoji.
Nadhani kuna ‘point’ hapa, tafakari chukua hatua.
0 comments:
Post a Comment