Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Sylvestre Marsh.
INASIKITISHA, ni msiba mkubwa kwa wanafamilia wa soka hapa nchini ambao hakika umeacha pengo ambalo ni vigumu kuzibika kutokana na kifo cha kocha wa zamani wa Taifa Stars, Sylvestre Marsh.
Alilazwa kwa mara nyingine tena mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wiki mbili zilizopita akitokea Mwanza, baada ya hali yake kuwa mbaya mpaka umauti ulipomfika juzi Jumamosi asubuhi hospitalini hapo.
INASIKITISHA, ni msiba mkubwa kwa wanafamilia wa soka hapa nchini ambao hakika umeacha pengo ambalo ni vigumu kuzibika kutokana na kifo cha kocha wa zamani wa Taifa Stars, Sylvestre Marsh.
Alilazwa kwa mara nyingine tena mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wiki mbili zilizopita akitokea Mwanza, baada ya hali yake kuwa mbaya mpaka umauti ulipomfika juzi Jumamosi asubuhi hospitalini hapo.
Sylvestre Marsh aliyezaliwa miaka 55 iliyopita, licha ya kuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars tangu enzi za Marcio Maximo hadi Kim Poulsen, pia aliwahi kuwa kocha wa timu kadhaa zikiwemo Azam FC na Kagera Sugar.
Alianza kuugua mapema mwaka jana na kulazwa kwa muda mrefu katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili na baadaye kuhamishiwa Ocean Road kwa matibabu zaidi baada ya kugundulika alikuwa akisumbuliwa na kansa ya koo.
Hakika Marsh amepitia mateso makubwa mpaka pale Mungu alivyoamua kumpumzisha. Awali alipolazwa mwaka jana, alikaa hospitali kwa zaidi ya miezi miwili tangu Februari mwishoni mpaka alipotoka Aprili.
Marsh, kipindi cha ugonjwa wake, alikuwa ni kama mtu aliyekata tamaa kutokana na yale ambayo alikuwa akiyapitia na hakupenda jamii ifahamu nini kinaendelea mpaka alipofariki.
Inasikitisha, kwa kuwa hajaacha chochote nyuma, kwani hakuwahi kuwa na mke wala mtoto. Baadhi ya marafiki zake wa karibu, wameliambia gazeti hili kuwa hawakuwahi kumuona akijihusisha na mambo ya wanawake hata mara moja.
Alikuwa ni mtu wa watu na kipenzi cha wanasoka wengi hapa nchini na nchi za jirani kutokana na ukarimu aliokuwa nao. Ndiyo maana wengi wanamzungumzia vyema:
Kim Pouseln (aliyewahi kuwa kocha wa Stars)
“Alikuwa rafiki yangu na tulikuwa tunawasiliana vizuri baada ya kuondoka huko Tanzania na alikuwa anapigana kuhakikisha afya yake inakuwa imara tena, ni huzuni tumempoteza, kwani alikuwa mtu wa watu.”
Iddrisa Nassor (Katibu Azam FC)
“Msiba umetushtua kwa kiasi kikubwa, marehemu tulifanya kazi pamoja kipindi cha nyuma, pia alikuwa hazina kwa taifa kutokana na kujitoa kwake kuhakikisha Stars inafanya vyema, lakini ndiyo hivyo ametangulia mbele ya haki.”
“Nimefanya kazi na Marsh kwa muda mrefu, kifo chake ni pigo na kimenishtua siyo siri, ingawa ameugua muda mrefu ila nasikitika na naikumbusha jamii, tuwe tunajaliana na kukumbukana nyakati zote, siyo za furaha pekee.
“Marsh amepitia mateso makubwa, mchango wake kwa jamii ni kama ulikuwa hauna thamani.”
Athuman Bilal ‘Billo’ (Kocha Stand United)
“Marsh kwangu mimi alikuwa kama baba, amenifundisha soka nimefika hapa nilipo mpaka nimekuwa kocha. Tumeishi pamoja kama familia tukiwa Mwanza, nilikuwa nafuatilia maendeleo yake mara kwa mara, lakini Mungu ameamua kumchukua, hakika nimepoteza mtu muhimu.”
Juma Kaseja (mchezaji)
“Alikuwa ni zaidi ya mwalimu kwangu, tumeshirikiana kwa muda mrefu na ametengeneza vijana wengi katika soka, binafsi nimeumia kwa sababu tumepoteza mtu muhimu sana kwenye sekta hii.”
Kuzikwa…
Championi lilizungumza na katibu wa kamati ya mazishi, Almasi Moshi ambaye pia ni kiongozi wa Chama cha Soka Wilaya ya Ilemela.“Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza siku ya Jumapili (jana). Marehemu ataagwa siku ya Jumatatu katika Uwanja wa Nyamagana na kuzikwa katika Kijiji cha Ng’ombe wilayani Misumbwi jijini Mwanza.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina la Bwana libarikiwe…
0 comments:
Post a Comment