2014-12-05

DUNIA INA MAMBO! KUTANA NA DAKTARI ANAYETUMIA PAMPU YA BAISKELI KUFANYA UPASUAJI!

Daktari anayetumia pampu ya baiskeli kulifurisha tumbo la mwanamke anayetaka kukatwa kizazi nchini India. 

Jimbo moja nchini India limesitisha shughuli ya kufungwa kizazi wanawake baada ya daktari mmoja kupatikana akitumia pampu ya kuweka pumzi kwenye baiskeli kuweka hewa kwenye matumbo ya wanawake waliokuwa wanafanyiwa operesheni hizo. 
 

Daktari Chandra Rout, aliyetumia pampu hiyo kwa wanawake 56, Ijumaa wiki jana, aliambia BBC kuwa pampu hizo hutumiwa sana katika jimbo hilo la Orissa.
Maafisa wa serikali walisema gesi ya kaboni, ndio inapaswa kutumiwa kwa operseheni hizo wala sio pampu za kuweka hewa baiskeli. 

Maafisa hao wamesema kuwa watu wanaweza kutumia hewa ya kaboni lakini utumizi wa pampu hiyo ni hatari kwa maisha ya binaadamu.


Mwezi Uliopita ,kashfa nyingine ilizuka kuhusu ukataji wa kizazi baada ya wanawake 15 kufariki walipofanyiwa upasuaji katika jimbo jengine.


Madawa ya kulevya yalitumika wakati wa upasuaji huo katika jimbo la Chhattisgarh.


Kambi za ukataji kizazi hufanyika mara kwa mara ili kuwakata kizazi kwa pamoja wanawake nchini India kama mojawapo ya mipango ya kudhibiti ongezeko la idadi ya watu nchini humo.Ripoti kwamba daktari Rout alitumia pampu ya baiskeli ili kuyafurisha matumbo ya wanawake kwa lengo la kupata nafasi ya vifaa vya upasuaji kuingia ndani, imezua pingamizi nchini India tangu habari hizo zitangazwe. 



Maafisa wa serikali wamesema kuwa utumizi wa hewa ya kawaida badala ya ile ya kaboni unaweza kusababisha magonjwa kadhaa. 

Mkuu wa afya katika jimbo la Orrisa Arati Ahuja amesema kuwa ukataji wa kizazi katika jimbo hilo sasa utafanyika katika hospitali zenye vifaa vyote .


''Madaktari watalazimika kuambatana na maagizo ya kimataifa ili kukinga maambukizi yoyote '',bi Ahuja alsema.Ukataji wa kizazi hufanyika kupitia kuzifunga tubu zinazobeba mayai ya mwanamke.


Hii hufanyika kupitia kufunga na kamba na baadaye kukata tubu hizo,swala linalozuia mayai na mbegu za kiume kukutana ili kutengeza mimba.


Lakini daktari Rout amesema kuwa amekuwa akitumia pampu kwa zaidi ya mara 100 lakini hakujawahi kutokea tatizo lolote. 

Anasema kuwa waliamua kutumia pampu hiyo wakati kifaa kinachojulikana kama Insafleta kilipokosekana kwa upasuaji.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...