2015-03-09

Ina sikitisha sana:WATANO WAUAWA KWA VISU JAPAN

Maofisa wa polisi wakiwa eneo ambapo mtu mmoja amewaua watu watano kwa visu huko Sumoto, Japan.

WATU watano wameuawa kwa kuchomwa visu wakiwa majumbani mwao katika Mji wa Sumoto uliopo katika Kisiwa cha Awaji, magharibi mwa Japan leo alfajiri. 


Wanausalama wakikagua eneo yalipotokea mauaji hayo.

Kwa mujibu wa polisi, mtu mmoja mwenye umri wa miaka 40 anashikiliwa na polisi kwa kuhusishwa na mauaji hayo.

Vyombo vya habari nchini Japan vimeeleza kuwa mtuhumiwa huyo anajulikana kwa jina la Tatsuhiko Hirano na alikamatwa baada ya kukutwa na damu kwenye nguo zake na kukubali kuhusika na mauaji hayo. 

Ramani ikionyesha Mji wa Sumoto yalipotokea mauaji ya watu watano.

Polisi walikuta miili ya wanawake wawili wenye kati ya umri wa miaka 50 na 60 pamoja na mwili wa mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 60 katika nyumba moja iliyopo eneo hilo.

Pia wanandoa wenye kati ya miaka 80 walikutwa wamefariki katika nyumba nyingine iliyopo eneo hilo.

Mtuhumiwa huyo alikuwa akiishi na baba yake pamoja na bibi yake jirani na eneo yalipotokea mauaji hayo. 
GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...