Askari wauziwa vinywaji, chakula bei juu, washindwa, wakimbilia kwa Mama Ntilie, wasema bora zifungwe
Asilimia kubwa ya askari polisi nchini wamekerwa na kitendo cha kantini zao kumilikishwa kwa wafanyabiashara binafsi ambao wengi wao wamekuwa wakiuza vyakula na vinywaji kwa bei ghali tofauti na makusudio.
Fukunyuafukunyua imebaini kuwa hali hiyo imefanya askari polisi wengi kuzikacha kantini hizo na kukimbilia vyakula vya Mama Lishe ambao wamesogeza huduma zao karibu na vituo hivyo vya polisi.
Asilimia kubwa ya askari polisi nchini wamekerwa na kitendo cha kantini zao kumilikishwa kwa wafanyabiashara binafsi ambao wengi wao wamekuwa wakiuza vyakula na vinywaji kwa bei ghali tofauti na makusudio.
Fukunyuafukunyua imebaini kuwa hali hiyo imefanya askari polisi wengi kuzikacha kantini hizo na kukimbilia vyakula vya Mama Lishe ambao wamesogeza huduma zao karibu na vituo hivyo vya polisi.
Wakizungumza na gazeti hili askari wengi walilalamikia utaratibu wa ‘kubinafsisha’ kantini za polisi kwa raia na kusema ni hatari.
Askari mmoja wa kituo kimoja cha polisi (jina lake na la kituo vinahifadhiwa) jijini Dar, alisema: “Wengi tumeamua kuzikimbia kantini za polisi kutokana na ukweli kwamba siku hizi zimekuwa ni za kibiashara kuliko kutoa huduma kwetu askari.
“Kwa kweli bei za kwenye kantini nyingi ni mara mbili ya kwa Mama Lishe, kama hivyo ndivyo kwa nini tutumie huduma za kantini?“Pendekezo letu ni kwamba wafanyabiashara kwenye kantini za polisi waondolewe na badala yake jeshi la polisi litoe huduma hiyo kama zamani au zifungwe.”
Askari mwingine mwenye cheo cha koplo alisema: “Hatujui hawa watu waliruhusiwa na nani kufanya biashara kwenye kantini za polisi na wanafanya biashara kwa utaratibu upi. Haya ni maeneo ya jeshi, kwa nini raia atoke huko na kuja kufanya biashara hapa?”
Polisi mwingine ambaye naye hakutaka kuandikwa jina alisema: “Kwani sisi polisi tunashindwa kuendesha kantini na kuzisimamia? Ama hizi biashara ni za vigogo wa polisi?
“Tunamuomba Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu (picha ndogo juu) atusaidie kulitatua tatizo hili maana tunaumia sana na ni aibu askari kuikimbia kantini yao na kwenda kula kwa Mama Lishe.
“Kwanza tunapokula nje ya kituo usalama wetu huwa mdogo kuliko tungekuwa tunakula hapa kituoni, lakini pia wafanyabiashara kuruhusiwa kuendesha kantini ni hatari kwa usalama wetu kwa sababu zinaingiza watu wa kila aina na zimegeuka baa za uraiani, huwezi kumjua mbaya wako pia asilimia kubwa ya wahudumu ambao ni raia wana lugha chafu.”
Waandishi wa safu hii walitembelea kantini za Vituo vya Polisi vya Oysterbay, Kijitonyama, Central, Chang’ombe, Buguruni, Stakishari, Kilwa Road, Magomeni na kufanya uchunguzi juu ya kilio hicho cha askari na baadhi ya vituo hivyo walikuta kuna wafanyabiashara wamepewa kazi hiyo.
Katika Kituo cha Polisi cha Kijitonyama bei ya vyakula kwenye mabano ni kama ifuatavyo, ugali nyama choma shilingi 5,000, mitaani 2,500, wali nyama 3,000, mitaani (2,000), pilau 3,000, mitaani (2,000), ndizi nyama 3,000, mitaani (2,000) na yai 500, mitaani (350).
Kwa upande wa vinywaji bia ni shilingi 2,500, mitaani (2,300), maji madogo 700, mitaani (500), makubwa 800, mitaani (600).Hata hivyo, Mkurugenzi wa Kantini ya Polisi Kijitonyama, Joseph Chuwa alipoulizwa alisema kwamba bei hizo zinategemeana na manunuzi.
Uchunguzi unaonesha bei za maeneo mengine hazitofautiani sana isipokuwa kantini za Kituo cha Polisi Stakishari na Buguruni ni nafuu kwa sababu zinaendeshwa na vituo husika na siyo watu binafsi.
Aidha, kantini za mikoani hasa Arusha, Mwanza, Mbeya na Morogoro waandishi wetu walipata malalamiko kama hayo.
Hakuna kiongozi wa polisi katika vituo hivyo aliyekuwa tayari kuzungumzia hilo na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba hakuweza kupatikana.
GPL
0 comments:
Post a Comment