2015-03-03

Malaria yamlaza Madee hospitali...........ni huruma sana

Staa wa Bongo Fleva,Madee hivi karibuni alilazwa kwenye hospitali ya AAR iliyopo maeneo ya Sinza,jijini Dar baada ya kuugua ugonjwa wa Malaria.

Akizungumza na Clouds Fm,Madee alisema kuwa mwishoni mwa wiki hii alizidiwa sana na kukimbizwa hospitali alipopimwa aligundulika kuwa ana ugonjwa wa Malaria na kupumzishwa kwa muda katika hospitali hiyo.
 ‘’Yaah! Ni kweli nilikuwa naumwa sana ikabidi niende hospitali nikagundulika kuwa nina malaria daktari akashauri nipewe kitanda nikalazwa pale hospitali ila kwa sasa namshukuru Mungu naendelea na matibabu nipo vizuri,’’alisema Madee.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...