Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 Naishi Tabata jijini Dar nimejitokeza kwenu kuomba ushauri, Mimi na mpenzi wangu ambae amenisomesha toka form one hadi sasa nipo chuo kwani wazazi wangu walifariki wakati mimi nikiwa mtoto mdogo sana.
Sasa huyu mpenzi wangu amenigharamia sana yani kuanzia nguo zote hadi chakula nacho kula vyote ni msaada wake yeye na amejitolea kuninunulia gari la kutembelea na kanambia nitafute kiwanja ili tujenge nyumba ya kupangisha.Ila mimi kwa sasa naona kama huyu mwanaume hatuendani kwani yeye
hana elimu ila anafanya kazi kutumiaakili ya kuzaliwa, Jamani mimi nataka kuishi na msomi mwenzanguila huyu kaka mimi naona kama freemasson kwani kanisaidia sana asije akanitoa kafala, Mimi kwa sasa nimepata mpenzi mpya ambae anaelimu ya chuo sio
mshamba kama huyu wa zamani.Sasa please naombeni ushauri wenujamani nimwambiaje kama sipo tayari kuishi na yeye huyu mpenzi wa zamani bila kuumiza moyo wake...?
0 comments:
Post a Comment