Mchezaji nyota wa mpira wa miguu anaeichezea timu kubwa tajiri duniani Real Madrid alionekana na kupigwa picha na mapaparazi kwenye matembezi yake binafsi Dubai akiwa amevalia mavazi ya Kiislam na yaliompendeza sana.
Cristiano Ronaldo ambaye yeye si Muislam lakini alipendezwa na uvaaji huo kwani alisema aliona watu wengi waishio Dubai ndio vazi lao kuu na kwanini yeye asiwe miongoni mwa waliovaa vazi hilo.
Pia hakuwahi kuvaa vazi la dini hiyo alionelea avae kwa ishara ya kuiheshimu dini hiyo na kuona sio kitu kibaya kuwa miongoni kwao kimavazi.
Mchezaji huyo alikuwa Dubai wiki iliyopita kwenye mapumziko yake binafsi mbali na shughuli za kimpira. Alienda kutembea huko kabla ya wiki ya sikukuu za christimas.
Alionekana ni mwenye kufurahishwa na mandhali ya mji huo pia utamaduni wao wa chakula pia kimavazi ndio mana nae alipendezwa kuvaa kama wao.
Mchezaji huyo alikaa Dubai kwa siku nne wiki ilopita na baadae aliondoka kurejea Hispania ambapo alijiunga na wachezaji wenzake kwenye kambi ya maandalizi ya mechi zilizoendelea katika ligi ya ichi hiyo amakochezea.
0 comments:
Post a Comment