2015-03-05

MZEE HUKO CLEVELAND OHIO AMPA KIBANO JIRANI YAKE BAADA YAKUSAIDIA KUMWONDOLEA THELUJI



Kijana mmoja huko Cleveland jimbo la Ohio alijikuta wakati mgumu baada ya kukunjwa na jirani yake ambaye ni mzee anayekadiriwa kufikia umri wa miaka 80. 
Kijana huyo alikua akisaidia kumwondolea theluji iliyokua imezunguka nyumba yake na kuziba njia ya kutembelea kwa miguu na alifanya hivyo kwa lengo la kumsaidia mzee huyo ili aweze kumrahisishia upitaji wa miguu iwapo atahitaji kufanya hivyo. 

Mzee huyo baadae alipofuatwa na vyombo vya habari kuulizwa ni kwanini amefanya hivyo wakati kijana alikua akimsaidia kuondoa theluji nyumbani kwake yeye alijibu nilishamwambia sihitaji kuondolewa theluji lakini yeye aliendelea kufanya hivyo.

Majirani wamesema mzee huyo alimfuata kijana yule na kuanza kumkaba na baadae kuanza kumrushia theluji ili asiendelee na jitihada zake za kukwangua theluji hiyo ambayo ilileta adha kwa watumiaji wanaotembea pembezoni mwa nyumba yake

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...