2015-03-16

Polisi wakamata majangili sugu 40..........tazama hapa kuona video


Akizungumza mjini hapa jana, Mratibu wa kikosi kazi hicho katika eneo la Ikolojia ya Serengeti, Robert Mande ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili (NCAA), alisema watuhumiwa hao baadhi tayari wameshafikishwa mahakamani.

Arusha. Kikosi kazi kilichoundwa na Serikali kudhibiti matukio ya ujangili, kimefanikiwa kuvunja mtandao wa ujangili kwa kuwakamata watuhumuhiwa zaidi ya 40 na silaha mbalimbali. 


Akizungumza mjini hapa jana, Mratibu wa kikosi kazi hicho katika eneo la Ikolojia ya Serengeti, Robert Mande ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili (NCAA), alisema watuhumiwa hao baadhi tayari wameshafikishwa mahakamani.

Mande alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na juhudi za vyombo vya usalama.

Alisema mtandao huo katika ngazi ya kwanza ya ujangili unahusisha watu wanaoishi jirani na maeneo ya hifadhi na yenye wanyamapori na ndio watoa taarifa. 


Akizungumzia kazi ya kupambana na ujangili katika eneo la Ikolojia ya Serengeti, Kaimu Meneja wa Utalii wa NCAA, Asanaeli Merita alisema imeonyesha mafanikio makubwa.

Alisema kudhibitiwa kwa ujangili katika eneo hilo kunatokana pia na mpango maalumu uliopitishwa na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mpango huo umegawa kanda tatu kama maeneo muhimu ya kukabiliana na ujangili.
Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...