2015-04-08

Lulu: Nilishalia Sana, Nishaumia Sana Lakini Kwasasa…….



Staa mrembo kutoka Bongo Movies Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameamua kutoboa kile alichokiita kama faraja yake kwa hivi sasa. 

“Faraja YANGU...Nishalia sana,nishaumia sana lakini kwa sasa nikiona mmoja kati ya hawa analia au kuumia ndo kitu kinachoweza kuniumiza zaidi...!MUNGU awatunzeeee”-Lulu aliandika hayo jana usiku kwenye ukursa wake mtandaoni mara baada ya kuweka picha ya mama yake na mdogo wake. 

Kufuatia andiko hilo komenti za mashabiki wengi zilielekea zaidi kumzungumzia kifo cha Steven Kanumba kwani leo tarehe 7 mwezi huu ni siku ya kumbukumbu cha kifo cha staa huyo wa Bongo Movies ambae alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Lulu. 

Japo kuna baadhi ya watu amabo sio wastaarabu wamekua wakimshabuliaLulu kwa maneno makali, lakini kwa maneneo hayo ya Lulu nadhani wenye busara wamekuelewa.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...