2014-10-30

Updates: Watu wapoteza maisha baada ya Hiace na Lori kugongana Arusha. ANGALIZO: Picha zinasikitisha


Simanzi zimetanda jiji la Arusha baada ya watu zaidi ya 15 kufa katika ajali iliyotokea eneo la Tengeru.

Akiongea na Kajunason Blog mmoja ya mashahidi aliyefika eneo la tukio na hospitali ya Mount Meru amesema ajali ilitokea majira ya saa kumi jioni huko maeneo ya Sadec-Darajani -Tengeru iliyohusisha gari la abiria aina ya Hiace linalobeba watu toka Usa-River kwenda Arusha mjini na Lori la mafuta.

Aliongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa hiace (gari la abiria) iliyokuwa ikijaribu kupita magari mengine ndiyo akakutana uso kwa uso na lori hilo. Habari kamili zitawajia punde.


















2014-10-29

KUHUSU NANI KUPEWA TAJI LA MISS TANZANIA 2014 KAMA SITTI MTEMVU ALIDANGANYA UMRI, LUNDENGA ATOA JIBU.

Inawezekana wewe ukawa miongoni mwa wengi wanaofuatilia skendo ya Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu na inawezekana pia umeshajiuliza nini kitatokea uchunguzi wa BASATA utakapokamilika na ikibainika kuwa alidanganya umri wake.


Baada ya mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania bwana Hashim Lundenga kuulizwa na 255 ya XXL ya Clouds Fm, kama ‘ikitokea’ Sitti akijivua taji/akithibitika alidanya umri, taji hilo atapewa nani au shindano litarudiwa? hiki ndicho alichojibu:

“Sitaki kuzungumza hiyo sitaki kuzungumza mpaka ikitokea tutajua nini la kufanya lakini haijatokea kwamba taarifa hizi ziko sahihi”.

TUNAFUKUA: KAMA WEWE UMESOMA AU ULISOMA, ANGALIA PICHA HIZI KWA DAKIKA 2 TU.

Nenda Google images andika Maneno Haya 'Wanafunzi wa Chuo'
Kama hazitatoka picha hizi nyingi za Aina hii Hapa Chini naacha kufukua:


Halafu baada ya hapo andika ''University Students'' Zitakuja Picha za Aina Hii Hapa Chini:

Je Tumlaumu nani?

TUNAFUKUA: Rais aipasua kichwa UKAWA 2015: FUKUFUKU

 

Dar es Salaam. Baada ya vyama vinne vya upinzani nchini kusaini makubaliano ya kushirikiana pamoja na kusimamisha mgombea mmoja katika chaguzi zote zijazo, umoja huo sasa unakabiliwa na kazi ngumu ya kuweka sawa mambo, ikiwa ni pamoja na mchakato wa kumpata mgombea urais, kabla ya filimbi ya uchaguzi kupulizwa.

Vyama hivyo vitalazimika kufanya uamuzi katika sera tofauti za vyama vyao, kukabiliana na Sheria ya Uchaguzi, taratibu za kupata wagombea wa kuanzia ngazi ya chini hadi urais na jinsi ya kuendesha kampeni zao kabla ya kuwaendea wananchi kuwaeleza kuwa wameshajizatiti kukabiliana na chama tawala, ambacho kina mtandao karibu nchi mzima uliojengwa kwa miaka mingi.
Vyama hivyo vimeibuka na nguvu mpya baada ya kuunganishwa na hoja ya kutetea Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilielezewa kuwa ilitokana na maoni ya wananchi na hivyo kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupambana na wajumbe wa CCM kwenye Bunge Maalumu la Katiba.

Vyama hivyo, Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na NLD vilisusia mchakato wa Katiba kwa kile vilichodai kuwa ni kutoridhishwa na mambo yalivyokuwa yakiendeshwa na sasa umoja wao umekwenda mbali zaidi kutaka kushirikiana kwenye chaguzi.

Kutekeleza hilo, Jumapili iliyopita wenyeviti wa vyama hivyo, Profesa Ibrahimu Lipumba (CUF), Freeman Mbowe (Chadema), James Mbatia (NCCR- Mageuzi) na Dk Emmanuel Makaidi (NLD) walisaini makubaliano ya ushirikiano huo katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Jangwani.

Moja ya kazi ngumu inayoukabili umoja huo ni jinsi ya kumpata mgombea wa urais atakayetoa upinzani mkubwa zaidi kwa mgombea wa chama tawala na kuendelea kupunguza kura za CCM baada ya mafanikio ya mwaka 2010 ya kupunguza asilimia 20 za kura alizopata RaisJakaya Kikwete mwaka 2005.

Kazi hiyo ngumu inatokana na tofauti za kisera baina ya vyama hivyo, wagombea urais wanaoonekana kuwa na sifa na matokeo ya uchaguzi uliopita uliompa mgombea wa Chadema, Dk Willibrod Slaa asilimia 26 ya kura zote na kuweka rekodi ya upinzani kukusanya kura nyingi.

Wakati Chadema ikitegemea mtaji wa Dk Slaa, ambaye ni katibu mkuu wa Chadema, wa asilimia 26.34 ya kura za mwaka 2010, CUF imekuwa ikimsimamisha mwenyekiti wake, Prof Lipumba katika chaguzi nne zilizopita, huku NCCR-Mageuzi ikiwa na mwenyekiti wake, james Mbatia na NLD ikiwa na Makaidi.

Mbowe alisema hilo halitakuwa tatizo kubwa katika kufikia uamuzi wa mgombea urais.

“Kwanza niseme tu kuwa hapa tulipofika haikuwa rahisi sana kama watu wanavyodhani, kwa hiyo yako mengi ambayo yamefanyika kwa kujadiliana na katika mchakato huu tumejifunza mengi. Kwa hiyo taratibu zitawekwa na zitafuatwa. Kutakuwa na vigezo na mambo kama hayo,” alisema mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alipozungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki akijaribu kuonyesha kuwa wamezingatia mambo mengi kabla ya kusaini makubaliano hayo.

“Suala la mgawanyo wa nafasi za kugombea haliwezi kutugombanisha. Ushindani si jambo geni kwetu maana tumekuwa na ushindani siyo sasa tu, bali hata ndani ya vyama. Hata katika chama kimoja huwa kuna wagombea zaidi ya mmoja.”

Kauli ya Mbowe iliungwa mkono na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila ambaye alisema ili kuondoa utata wowote unaoweza kujitokeza, kamati ya ufundi itaundwa kwa ajili ya kushughulikia masuala yote muhimu.

“Kamati hiyo itakayojumuisha vyama vyote, itatakiwa kutoa mwongozo wa nini kifanyike kulingana na masilahi na changamoto iliyopo kama inavyoelezwa katika azimio la Ukawa,” alisema Kafulila.

Uwezekano mkubwa ni Ukawa watalazimika kuamua kati ya Dk Slaa na Profesa Lipumba kwa kuwa tayari Mbatia, ambaye kwa sasa ni mbunge wa kuteuliwa, ameshaanza kampeni za kuwania ubunge wa Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Historia ya kugombea
Katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, Profesa Lipumba alipata kura 418,973, ikiwa ni asilimia 6.43 ya kura zote na kushika nafasi ya tatu akiwa nyuma ya mgombea wa CCM, Benjamin Mkapa aliyeibuka mshindi na Augustine Mrema.

Profesa Lipumba aliingia tena uchaguzi wa mwaka 2000 na kushika nafasi ya pili baada ya kuzoa kura 1,329,007 (sawa na asilimia 16.26) akiwa nyuma ya Mkapa na uchaguzi uliofuata alipata kura 1,327,125 (sawa na asilimia 11.68) kabla ya kushuka tena mwaka 2010 alipopata kura 695,667 (asilimia 8.06).

Dk Slaa alishangaza wengi alipoamua kutogombea ubunge mwaka 2010 baada ya Chadema kumteua kugombea urais. Mwaka huo, Dk Slaa alipata kura 2,271,941 (sawa na asilimia 26.34), matokeo ambayo yalishusha ushindi wa kishindo wa CCM wa mwaka 2005 kutoka asilimia 80.28 hadi asilimia 61.17 mwaka 2010.

Takwimu hizo na masuala mengine yatakuwa moja ya mambo ambayo Ukawa watalazimika kukuna vichwa kabla ya kumchagua mgombea wao.

Jambo ambalo litakuwa faraja kwao ni kuongezeka kwa idadi kubwa ya kura za wapinzani mwaka 2010.
Mwaka 1995 jumla ya kura za wapinzani zilikuwa 2,486,323, sawa na asilimia 38.17, lakini uchaguzi uliofuata 2000 wapinzani walipata jumla ya kura 2,309,123, sawa na asilimia 28.26 na kupungua zaidi mwaka 2005 walipopata kura 2,241,525 (sawa na asilimia 19.72. Mwaka 2010, upinzani uliibuka kwa nguvu na kusomba kura 3,121,136. Ingawa kwa asilimia, kura hizo zilikuwa asilimia 37.16 pungufu ya asilimia za uchaguzi wa 1995, idadi ya kura za wapinzani ilikuwa kubwa kwa tofauti ya zaidi ya kura 700,000, hali inayoashiria mwamko mpya kwa wapinzani.

“Kwa sasa wanatakiwa kuwa makini na propaganda za CCM, kwani ni rahisi kusambaratishwa kabla ya 2015. Hivyo wahakikishe wanapata mgombea atakayekuwa tishio kwa CCM,” alisema Profesa George Shumbusho wa Chuo Kikuu cha Mzumbe.

“Ni muhimu kama wamesaini makubaliano hayo wakati kuna jambo zito mbele yao na bado kuna hofu ya kuimarika kwao.”

Pia, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Eligius Danda alionyesha wasiwasi, akisema umoja huo umejikita zaidi katika kutafuta njia ya kwenda Ikulu, akiungana na mawazo ya Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitila Mkumbo.
“Wote wanne bado nina wasiwasi na dhamira zao. Viongozi walioko kwenye fikra ya madaraka siyo viongozi sahihi kwenye vyama vya siasa,” alisema Danda.

Danda alisema ili muungano huo uwe na nguvu na kukubalika, ni lazima dhamira zao ziwe katika kushughulikia matatizo ya msingi ya wananchi, lakini siyo kujikita katika kutafuta madaraka.
Suala la mgombea urais wa Zanzibar halionekani kuwa na kikwazo kikubwa kutokana na nguvu ya CUF visiwani humo pamoja na kukubalika kwa katibu mkuu wake, Maalim Seif Sharrif hamad.

Kumalizika kwa suala la urais wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar, kutafungua mlango kwa suala jingine gumu kutafutiwa ufumbuzi; wagombea wa ubunge katika majimbo, hasa ya Bara.

Vyama hivyo vimejenga ngome zake katika maeneo tofauti Bara na Zanzibar. Wakati CUF ina uhakika na viti vingi vya Zanzibar, hasa Pemba na baadhi ya mikoa ya Bara, Chadema, NCCR-Mageuzi na NLD vimegawana majimbo ya Bara, huku Chadema ikiongoza kwa kuwa na majimbo mengi.

Kazi ngumu itakuwa ni kuamua mgombea katika majimbo ambayo wagombea wa vyama hivyo wanapambana vikali, hasa majimbo ya Ubungo, Vunjo na Tarime.

Katika Jimbo la Ubungo, Ukawa watalazimika kufanya uamuzi kati ya mbunge wa sasa kutoka Chadema, John Mnyika na Julius Mtatiro wa CUF, wakati jimbo la Vunjo linaweza kuwa na mvutano baina ya Mbatia na John Mrema wa Chadema, ambao wameonyesha nia ya kuwania ubunge, huku CUF na Chadema wakichuana Tarime ambako jumla ya kura zao kwenye uchaguzi uliopita zingeweza kumuondoa mgombea wa CCM. Hali hiyo iko katika majimbo mengi ambayo vyama hivyo vilipambana vikali mwaka 2010.

Katika majimbo ambayo CCM ina nguvu, Ukawa wanaweza kuwa na matatizo zaidi katika kufanya uamuzi kwa kuwa yanaweza kuzua wagombea wengi kutoka vyama vinavyounda umoja huo ambao watadai kuwa ndio wanaoweza kupambana na chama hicho tawala. Mikoa kama ya Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Ruvuma na wilaya ambazo ziko pembezoni, CCM ina nguvu kubwa, lakini Ukawa itakuwa katika hali ngumu kufanya uamuzi wa kupata mgombea.
Nyongeza na Julius Mathias na Kelvin Matandiko, Dar na Daniel Mjema, Moshi.

VIEWERS REPORT, TBC YASHIKA NAFASI YA MWISHO

Kwa hali ya kushangaza, kituo cha television cha matangazo cha tbc 1 kati ya vituo vinne maarufu vya matangazo ya habari nchini Tanzania kimeshika nafasi ya mwisho baada ya kufanyiwa utafiti,

Kwa habari za uhakika ni kwamba kituo kilichoongoza kuangaliwa na watazamaji wengi ni ITV kikifuatiwa na Star TV, nafasi ya tatu imeshikwa na Channel 10 na hatimaye TBC1.

Kwa utafiti uliofanya na TCRA imebainika kuwa ni aibu kama kituo television ambacho ni cha Taifa na ni UMMA kushika mkia nyuma ya vituo binafsi jambo ambalo ni hatari.

Vyanzo vya kuaminika vinadai kuwa TBC1 imefikia hapo baada ya kugundulika inabagua baadhi ya habari ya vyama vya siasa na kutoa habari ya chama kimoja tu jambo ambalo siyo sahihi katika utashi wa utangazaji na kutofuata uhuru wa kiutangazaji ndani ya uongozi wa shirika la habari la Tanzania,

Utafiti umeonyesha kuwa ili chombo cha habari kiweze kuangaliwa na watu wote wa vyama vyote ni lazima chombo cha habari kitoe habari bila kubagua vyama vya siasa maana watazamaji wana misimamo tofauti na itikadi tofauti, na kama chombo cha habari kikiamua kutoa habari kwa chama kimoja cha siasa basi ujue hapo watakaoangali hizo taarifa za habari ni hao hao wa chama kimoja.

Watafiti pia walienda mbali zaidi na kukinyoshea vidole kituo cha taifa cha utangazaji kuwa ni chombo cha UMMA na kisipende kubagua baadhi ya taarifa za habari za vyama vya siasa kwa misingi ya kuelekezwa na wanasiasa au viongozi wa nchi maana madhara yake ni wananchi kushindwa kuangalia hicho kituo.


Mwisho wake kitashindwa kufanya biashara na hatimaye kutegemea tuu ruzuku serikalini na hapo ndo nchi itazidi kupata hasara badala ya kukiacha chombo kijiendeshe kwa uhuru. Wametoa mfano kama shirika la habari la Uingereza BBC lingefanya kama TBC inavyofanya basi nayo ingeishia kutazamwa tuu nchini uingereza na tena kwa watu wachache tofauti na ilivyo sasa BBC inatazamwa duniani kote.

Utafiti umeonyesha kuwa hivi vyombo vingine vya habari ITV, Star TV na Channel 10 vimepata watazamaji wengi kwa kuwa havibagui matangazo ya kada tofauti ya vyama vya siasa na hapo ndio inasababisha waweze kupata watazamaji wa kutosha.

ONA LORI LA MAFUTA- LAANGUKA, LATEKETEA KWA MOTO DAR

Mashuhuda wakieleza yaliyotokea.
Wafanyakazi kampuni inayomiliki lori hilo ambayo bado haijafahamika, wakifanya tathmini ya hasara iliyopatikana.Sehemu ya matairi ilivyobaki.Sehemu ya juu ilivyoungua.Maofisa wa polisi wakijadiliana la kufanya.…Wakielekea eneo la tukio baada ya kufikia muafaka.Askari wakilinda usalama eneo la ajali.Afisa wa polisi akimpa maelekezo askari wa usalama barabarani.Mashuhuda kila mmoja akieleza lake.Madereva wa bodaboda wakiwa wameacha shughuli zao ili kushuhudia tukio hilo.
LORI la mafuta aina ya Scania likiwa limesheheni dizeli likitokea bandarini jijini Dar es Salaam kuelekea mikoani, liligonga tuta katika Barabara ya Morogoro, eneo la Kimara-Baruti, likapoteza mwelekeo na kupinduka kisha kuwaka moto na kuteketea kabisa.

Wakati lori hilo likiwaka, mafuta yenye moto yalisambaa na kutaka kuunguza nyumba za jirani lakini Kikosi cha Uokoaji na Zima Moto cha Halmashauri ya Jiji, kiliwahi kufika eneo la tukio na kuudhibiti moto huo.
Tukio hilo limesababisha usumbufu mkubwa kwa magari yanayotumia njia hiyo kutokana na sehemu hiyo kupitika kwa shida.
GPL

Roketi ya Marekani ya Antares yalipuka


Roketi ya safari za anga za juu iliyokua ikielekea Kituo cha Kimataifa cha Anga za juu imelipuka wakati ikiruka kutoka jimbo la Virginia nchini Marekani.

Roketi Antares, yenye urefu wa ghorofa 14 ikiwa imetengenezwa na shirika la Orbital Sciences Corp, ililipuka sekunde chache baada ya kuruka katika kituo cha Wallops Flight Facility.


Chanzo cha tatizo la kulipuka kwa roketi hiyo ya mizigo bado hakijafahamika.

Mipango ya kurusha roketi hiyo ya anga za juu Jumatatu, ilicheleweshwa kutoka na boti iliyokuwa karibu na eneo la maji la kurukia roketi hiyo.

Ndege hiyo ilitarajiwa kuwa ya tatu kupewa kandarasi na Shirika la taifa la kusimamia safari za anga za juu la Marekani, NASA.

Roketi hiyo ilitarajiwa kubeba karibu kilo 2,200 za shehena kwa ajili ya wanaanga sita walioko katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.

"Tutajua kilichotokea, tunatumaini hivi karibuni, na tutaendelea vizuri na mipango yetu," amesema Frank Culbertson, makamu-rais mtendaji wa shirika la Orbital Sciences.

"Wote tumeona hili jambo likitokea kabla katika shughuli zetu, na wote tumeona kampuni husika zikiimarika kutokana na tukio kama hili, na tutafanya vivyo hivyo."

               
                     Roketi muda mfupi kabla ya kuruka

Hakuna aliyejeruhiwa, amesema Bwana Culbertson, na kundi la wataalam wachunguzi tayari walikuwa wakipitia data kujaribu kubaini chanzo cha ajali hiyo. ENDELEA KUSOMA


BBC

SAD NEWS: RAIS MICHAEL SATA WA ZAMBIA AAGA DUNIA

 

Rais Michael Sata wa Zambia afariki dunia

Familia ya Bwana Sata wameiambia BBC kuwa Rais wa Zambia, Michael Sata, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77 katika hospitali ya London alikokuwa akitibiwa ugonjwa ambao haujatajwa.

Kifo chake kimetokea siku chache baada ya Zambia kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo.

Mwanasiasa huyo mkongwe aliingia madarakani mwezi Septemba 2011 baada ya kuongoza chama chake cha Patriotic Front, na kumshinda Rupiah Banda, ambaye alikuwa rais wakati huo na chama chake cha Movement for Multi-Party Democracy, kikiwa madarakani kwa miaka ishirini.

Michael Chilufya Sata alizaliwa mwaka 1937 katika mji wa Mpika, eneo ambalo lilikuwa wakati huo ni Northern Rhodesia. Muumini wa dini ya Kikristo ya madhehebu ya Katoliki, alifanya kazi kama afisa polisi, mfanyakazi wa reli na mwanachama wa chama cha wafanyakazi wakati wa utawala wa kikoloni. Baada ya Zambia kupata uhuru wake, pia aliishi kipindi fulani mjini London, akiwa mfanyakazi wa reli, na kurejea Zambia, akiwa na kampuni ya teksi.

Akiwa mwenye sauti ya mkwaruzo yakiwa ni matokeo ya kuvuta sigara kwa muda mrefu, Bwana Sata aliibuka katika siasa na kupata umaarufu katika miaka ya 1980.

Haraka akapata sifa ya kuwa gavana mwenye kuchapa kazi kwa bidii, wakati akiongoza jimbo la Lusaka na mtu wa utekelezaji kwa vitendo.

Lakini pia alijulikana kama mtu wa kutoa amri, mtu asiyeendekeza urafiki na mkali- na wapinzani wake walisema jina alilopewa la bandia la "King Cobra" alikuwa anastahili kuitwa hivyo.

Kwa mara ya kwanza alionekana kama mtu ambaye angetekeleza ahadi za kupambana na rushwa na kupata ufumbuzi wa tatizo la ajira na kuleta ustawi wa jamii. Lakini kipindi chake madarakani kiligubikwa na kuuzima upinzani wa kisiasa na kudorora kwa uchumi.

Bwana Sata ni rais wa pili wa Zambia kufariki dunia akiwa madarakani.
BBC

2014-10-28

PHOTOS: CHID BENZ AKIWA CHINI YA ULINZI MKALI AKIPELEKWA MAHAKAMANI


Msanii wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini leo Dar es Salaam kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)

Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akiingia Mahakamani leo.

                       

Chidi Benzi akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi.


Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Chidi Benzi akipanda karandinga kwa ajili ya kuelekea katika mahabusu ya Segerea.



Na Mwandishi Wetu

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benzi’ leo amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la matumizi ya dawa za kulevya.

Chid Benzi, alipandishwa kizimbani majira ya saa nane mchana, mbele ya Hakimu Warialwande Lema, ambaye alimtaka msanii huyo atolewe nje kutokana na uvaaji mbaya wa suruali yake kwani alivaa ‘Kata kei’ ili avae vizuri nguo.

Akisomewa mashitaka yake, na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono, alidai kwamba mnamo 24 Oktoba 2014, Chidi Benzi alikutwa na dawa hizo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Alidai kwamba, shitaka la kwanza linalomkabili ni kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya sh.38, 638. Pia shitaka la pili ni kukutwa na gramu 1.72 za dawa kulevya aina ya Bangi yenye thamani 1,720.

Mbali na hilo, shitaka la tatu ni kukutwa na vifaa vinavyotumika kuvutia dawa hizo za kulevya, ambapo alikutwa na Kifuu cha nazi kitupu na kijiko kimoja.

Hata hivyo, wakili huyo alidai kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika. Hakimu Lema alihairisha kesi hiyo hadi Novemba 11, mwaka huu baada wadhamini kushindwa kujitokeza kwa haraka.

Hakimu Lema alisema, mshitakiwa huyo anatakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili wa kudumu pamoja na bonfdi ya Sh.milioni 1.

Hali hiyo ya kushindwa kupata dhamana ilizua hali ya simanzi kwa familia yake, kutokana na kuchelewa kujitokeza kwa wadhamini wake mbele ya Hakimu na hivyo kushindwa kupata dhamana.

Chidi Benzi alikamatwa na dawa za kulevya katika hatua ya ukaguzi kwaajili ya kupanda ndege ya Fastjet akielekea jijini Mbeya, juzi jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Statoil scholarship for Master Programme in Energy and Petroleum

 

Since 2011 the University of Dar es Salaam (UDSM), specifically the Department of Chemical and Mining Engineering, the Norwegian University of Science and Technology (NTNU) of Norway and the Angolan University of Agostinho Netto are collaborating under the ANTHEI project to train professionals for petroleum engineering and geosciences at Masters level. Already three batches of a total of 28 Tanzanian students have been enrolled under the program. In this program the students spend one year in Norway for class work and another year at the University of Dar es salaam and the industry for project work and thesis. While in Tanzania the students are under the responsibility of the Tanzanian project coordinator at the University of Dar es Salaam with the support of local professors, NTNU Professors and Statoil Professionals. Statoil is a Norwegian oil Company already engaged in petroleum activities in Tanzania.

Under the same scheme, another batch of 10 students will be granted scholarship next year (2015) to undertake M.Sc. in Petroleum Engineering and in Petroleum Geosciences. The scholarship covers subsistence allowance (stipend), travel grant to and fro, tuition, insurance and stationeries. The certificate will be issued by NTNU. Continue


To read more: http://www.wavuti.com/2014/10/scholarship-for-statoil-master.html#more

RAIS PROF. KIKWETE AHITIMISHA ZIARA VIETNAM





President Dr Jakaya Mrisho Kikwete lies a wreath at
the Mausoleum of the First President Ho Chi Minh in Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014 . 

President Dr Jakaya Mrisho Kikwete visits the Hung Fen Food Stuff Corporation at Trung Son in Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014
President Dr Jakaya Mrisho Kikwete in a souvenir photo with workers of the Garment 10 Corporation textile mill he visited at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014

:President Dr Jakaya Mrisho Kikwete shown some historical items as he visits the Garment 10 Corporation textile mill at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014

President Dr Jakaya Mrisho Kikwete visits the Garment 10
Corporation textile mill at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014. Photo by Ikulu.

BOMU LATEGULIWA NA JWTZ SONGEA

Bomu lililotengenezwa kienyeji kama linavoonekana katika picha.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akipata maelekezo kutoka kwa mtaalam wa mabomu ambaye ni kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kabla ya kulitegua bomu hili.

Hili ni eneo la tukio ambalo limezungushiwa mkanda huu wa pilisi uliandikwa hairuhusiwi kupita eneo hili. Lakini chini ya huo mti kama inavoonekana katika picha kukiwa na udongo umetifuliwa ndipo mahara ambapo lilitegwa bomu hili la kutengenezwa kienyeji pia hapo ndipo huwa wanakaa askari wa Usalama barabarani kwa kujikinga na jua ama kupumzika pindi wanapokuwa kazini

Bomu lililotengenezwa kienyeji


Mtaaramu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiweka vifaa vyake vya kutegulia bomu hilo lililo tengenezwa kienyeji.

Mtaalamu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiwa anaonyesha umahili wake alionao aweze kulitegua bila kuleta madhara yoyote yale katika jamii(Picha na demasho.com)
Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania(JWTZ) wamefanikiwa kulipua bomu lililotegwa katika eneo la kituo cha kurushia matangazo kilichopo mshangano cha shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Songea Mkoani Ruvuma siku ya jana majira ya saa moja jioni.


Bomu hili linalosadikiwa kutengenezwa kienyeji na watu wasiojulikana lilitegwa hatua zinazokadiliwa thelathini kutoka kitika kituo kilipo katika eneo ambalo askari wa usalama barabarani wanakaa kwa ajili ya kufanya kazi zao za kila siku.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema kwa mujibu wa wataalamu wa milipuko kutoka jeshi la Ulinmzi la Wananchi wa Tanzania bomu hili linaonekakana limetengenezwa kienyeji. Ameitaka jamii kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kuwabaini watu waliowalipua kwa bomu lililotengenezwa kienyeji askari polisi watatu wakiwa katika doria katika kata ya misufini Manispaa ya Songea.

Msikhela amesema Jeshi la polisi linafanya jitihada za kuwapata watu hawa wanaohusika na mtandao huu wa utegaji wa mabomu na ulipuaji. Aidha ameitaka jamii kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili liweze kuwabaini watu wanaousika na matukio ya namna hii.

Na hii ni mara ya pili katika manispaa ya songea kutokea kwa matukio haya ambapo tarehe Oktoba 16 mwaka huu askari watatu wa jeshi la polisi katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,  walijeruhiwa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono ambalo lilisadikiwa kutengenezwa kienyeji, katika eneo la matarawe mjini songea mkoani Ruvuma.

Askari hao walikutwa na mkasa huo saa moja na nusu usiku wakati wakiwa katika doria ambao ni WP Felista Abel, PC John Kaduma na PC Ramadhani Ally

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti amesikitishwa na kitendo hicho cha utegeji wa Mabomu ikiwa nikutaka kuhatarisha amani iliyopo katika mkoa huu wa Ruvuma. Aidha amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata wale wote wanaohusika na vitendo hivi.

MSANII CHID BENZ, APANDISHWA KISUTU




Msanii wa Hip Hop, Rashid Makwiro 'Chid Benz' leo amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka matatu ya kukutwa na madawa ya kulevya, vifaa vya kutayarishia uvutaji wa madawa, kusafirisha madawa ya kulevya na utumiaji wa madawa hayo ambayo alikamatwa nayo kwenye Uwanja wa Ndegee wa Julius Nyerere, Novemba 23. 


Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 11 mwaka huu na msanii huyo ametupwa rumande kwa kukosa wadhamini. 


Hata hivyo, atarudishwa kesho kukamilisha taratibu za wadhamini ambapo wadhamini hao wawili walitakiwa kutoa Shs. Milioni moja kama bond. 

OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA YATOA MAJIBU YA SENSA YA 2012

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Albina Chuwa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Kamishna wa Sensa, Hajjat Amina Said, akitoa ufafanuzi kwa wadau (hawapo pichani).

Mwakilishi wa UNFPA, Dk. Natalia Kanem akizungumza katika hafla hiyo.

Wadau mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.

OFISI ya Takwimu ya Taifa (NBS) kwa kushirikiana na Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) leo limetoa taarifa ya majibu ya Sensa ya Taifa ya mwaka 2012 kwa wadau mbalimbali waliohusika katika sensa hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamishna wa Sensa, Hajjat Amina Said, jijini Dar es Salaam ambapo amewataka wadau mbalimbali kutumia takwimu sahihi kutoka ofisi hiyo ili kusimamia maendeleo ya taifa.

GPL
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...