IDADI ya wanachuo 4,124 wanachukua mafunzo maalum ya Stashaada ya Elimu ya Awali ya miaka 3 katika vyuo 19 vya Ualimu kuanzia mwaka 2014/2015, Serikali imeanzisha mafunzo haya ili kuweza kupata walimu mahiri na wa kutosha wa ngazi hiyo ya Elimu.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Anne Kilango (pichani) wakati akujibu swali la msingi la Mhe. Rosweeter Kasikila, Mbunge wa Viti Maalumu aliyetaka kujua mpango wa Serikali katika kuhakikisha Elimu ya Awali inatolewa kwa ukamilifu.
Mhe. Kilango amesema katika jitihada za Serikali za kuipa uzito Elimu ya Awali, Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, kifungu cha 3.1.2, imetamka bayana kuwa Serikali itaweka utaratibu wa Elimu ya Awali kuwa ya lazima na itatolewa kwa watoto wenye umri kati ya miaka mitatu hadi mitano kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja.
“utoaji wa elimu katika ngazi zote nchini huongozwa na Sera ya Elimu na Mafunzo ambayo hutafsiriwa katika Mipango mbalimbali ya Maendeleo ya Elimu wakati wa utekelezaji” aliongezea Mhe. Kilang
Serikali kupitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya mwaka 1995, kifungu cha 5.2,ilielekeza Elimu ya Awali kuingizwa katika Mfumo rasmi wa Elimu (Formalisation of Pre-primary Education) ili iweze kusimamiwa, kudhibitiwa na kuratibiwa vizuri kulingana na Sera, Kanuni na Miongozo ya Elimu.
Aidha Sheria ya Elimu Na.25 Sura ya 353 kifungu cha 36 (ambayo itafanyiwa marekebisho ili kuendana na Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014) imetamka kuwa kila mototo aliye na umri usiopungua miaka mitano ana haki ya kuandikishwa elimu ya Awali kwa kipindi cha miaka miwili.
0 comments:
Post a Comment