Abiria waliokuwa wakisafiri katika mabasi ya Kimotco na Florida leo asubuhi walinusurika baada mabasi hayo kugongana uso kwa uso katika barabara ya Iringa-Dodoma leo saa moja na nusu asubuhi. Basi la Kimotco husafiri kati ya Iringa na Arusha na lina namba za usajili T449 CAL wakati Florida husafiri kati ya Migoli na Iringa na lina namba za usajili T571 BDX.
Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo ilisababishwa na kona katika eneo husika na mwedo kasi wa mabasi yote mawili.
0 comments:
Post a Comment