Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba.
RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba jana usiku amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akiendesha kupata ajali na kupinduka eneo la Mkindu jirani na mizani mkoani Morogoro.
Mwakifwamba alipata ajali hiyo wakati akijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki 'bodaboda' baada ya gari lake aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 176 CYM kupata pancha na kuanza kupoteza muelekeo.
Katika gari hilo, Simon alikuwemo peke yake na alitoka salama salimini.
Akiongea kwa njia ya simu akiwa njiani kurudi Dar, Mwakifwamba alisema, "Ilikuwa majira ya saa 3 usiku wakati nikitokea mkoani Dodoma na nilipofika Mkindu tairi la mbele la gari langu lilipata pancha na mbele yangu alikuwepo mwendesha bodaboda, nikajaribu kumkwepa na tairi la pili likapata pancha na gari kupinduka. Namshukuru Mungu nilitoka salama."
0 comments:
Post a Comment