Baadhi ya miili ya abiria waliouawa jana na Al-Shabaab eneo la Mandera, Kenya.
Basi lililotekwa na Al-Shabaab eneo la Mandera likiwa njiani kuelekea Nairobi.
MSHAURI wa Rais Uhuru Kenyatta wa nchini Kenya, Abdikadir Mohammed amesema kuwa mauaji ya watu 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi nchini humo jana yalilenga kusababisha vita vya kidini.
Kwenye mahojiano na BBC Abdikadir Mohammed alitoa wito kwa Wakenya kutoka madhehebu yote kuungana pamoja dhidi ya kile alichokitaja kuwa vitendo vya uhalifu.
Wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab waliwapiga risasi wasafiri ambao walishindwa kukariri Koran .
Al-Shabaab ilisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi mauji ya hivi majuzi ya waislamu yaliofanywa na wanajeshi wa Kenya kwenye mji wa pwani wa Mombasa.
Serikali ya Kenya imesema kuwa imeanza kuwatambua waliotekeleza mauaji hayo na itawafikisha mbele ya sheria hivi karibuni.
Wanajeshi wakiwa eneo la tukio.
Baadhi ya miili ya watoto ambao nao waliuawa katika shambulio hilo.
Miili ya marehemu ambao wengi walikuwa siyo waislamu.
Ndugu wa marehemu wakiwa na simanzi wakati wa kupokea miili ya wapendwa wao
0 comments:
Post a Comment