2014-12-27

HABARI;KAMILI YA BOMU LILILOLIPULIWA SONGEA NA KUUA MLIPUAJI

Kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akitoa
maelezo kwa DCP Diwani Athumani ambaye aliwasili mkoani humo jana
kwaajiri ya bomu la kutengenezwa kienyeji ambalo askari wa doria
walinusurika kurushiwa na kumlipukia mlipuaji wa bomu hilo ambaye
alifariki papo hapo. 





Askari WP Mariam mwenye namba 8616 akiwa amelazwa wodi ya 

majeruhi hospitali ya Mkoa baada ya kujeruhiwa mkono wa kushoto kwenye
bega baada ya vipande vya bomu kumfikia akiwa na askari wenzake kwenye
doria siku ya sikukuu ya krisimas.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiuangalia mwili wa
mtuhumiwa wa ulipuaji wa bomu ambaye alitaka kuwarushua askari wa
doria wakati wa sikukuu ya krismas kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. 

NA AMON MTEGA,SONGEA
JESHI la Poilisi mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na timu ya makachelo
toka makao makuu ya jeshi hilo wanawasakaka watu watatu ambao 

wanasadikiwa kujihusisha na ulipuaji wa mabomu huku mwenzao mmoja
akiwa amefia katika eneo la tukio baada ya kutaka kufanya jaribio la 

kuwatupia bomu bomu askari waliyokuwepo doria katika sikukuu ya
Krisimas ambalo lilimshinda na kumlipukia mwenyewe na kusababisha 

kupoteza maisha papo hapo huku utumbo ukiwa umemwagika nje na mkono
wake wa kushoto ukiwa umekatika kabisa na vipande vyake hajijulikani
vilipo. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa mikutano wa
jeshi la polisi Mkoa wa Ruvuma Naibu Kamishna wa jeshi la Polisi, 

kaimu mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jina nchini (DCP) Diwani 

Athumani alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 1.30
usiku huko katika mtaa wa Kotazi uliopo kata ya Majengo manispaa ya 

Songea ,timu ya askari wakiwa doria kulitokea mlipuko wa kitu
kinachozaniwa kuwa ni bomu ambalo limetengenezwa kienyeji na 

kusababisha kuwajeruhi askari wawili .
DCP Athumani aliwataja askari waliojeruhiwa kuwa ni PC Mselem mwenye 

namba G 7903 ambaye alijeruhiwa mkono wake wa kushoto na alitibiwa na
kuruhusiwa na mwingine PC Mariam mwenye namba WP. 8616 ambaye 

amejeruhiwa kwenye bega la mkono wa kushoto na amelazwa katika
hospitali ya Mkoa Songea(HOMSO)akiendelea kupata matibabu. 

Alisema kuwa timu ya makachelo toka makao makuu wakishirikiana na 

makachero wa Mkoa wa Ruvuma wamejipanga vizuri kuhakikisha watuhumiwa 

watatu waliohusika na tukio hilo pamoja na kufuatilia mtandao wake wa 

hualifu wanakamatwa mara moja kwani vitendo vya ulipuaji wa mabomu 

umekithiri nchini ikiwemo Mkoa wa Ruvuma kwani hadi sasa ni tukio la
tatu kwa mwaka huu. 

DCP Athumani alieleza zaidi kuwa wahalifu hao watakamatwa kirahisi
kutokana na tukio walilolifanya baada ya mwenzao kulipukiwa na bomu 

hilo na kusababisha kifo chake walijaribu kutorosha mwili wa mwenzao 

ili kupoteza ushahidi lakini ilishindikana baada ya askari polisi 

doria wengine kuwahi eneo la tukio na wahalifu hao waliacha mwili wa 

mwenzao na kutokomea kusikojulikana.
“Wahalifu hao waliuvuta mwili wa mwenzao kutoka katika eneo la tukio 

kwa umbali wa mita zisizopungua 80 na 90 kwa lengo la kutaka kupoteza
usahidi lakini waliwahiwa na askari wengine wa doria na kuuacha mwili 

na kutokomea kusikojulikana” alisema DCP Athumani.
Hata hivyo amewaomba wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa 

dini,wanasiasa,wazee, makundi mbalimbali ya kijamii pamoja na 

waandishi wa habari kuwa kitu kimoja katika kuwafichuwa waharifu hao
ili matukio hayo yasiweze kujirudia tena hususani Mkoa wa Ruvuma. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu aliyetembelea
eneo la tukio na kuzungumza na waandishi wa habari kwa masikitiko 

makubwa alisema kuwa waharifu hao wanaishi kwenye jamii inayotuzunguka
hivyo ni vyema kila mmoja akaliona jambo hili kwa umuhimu wake wa 

pekee kulipa uzito na kuwafichuwa wahalifu ili Mkoa uendelee kuwa na
amani kwani linaleta taharuki kwa jamii jambo ambalo linarudisha nyuma 

shughuli za maendeleo.
Naye Mganga Mkuu mfawidhi Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Dkt. Benedkto 

Ngaiza amethibitisha kupokea mwili mmoja wa mtu ambaye amekufa ukiwa 

utumbo umetoka nje na majeruhi wawili ambao ni askari na kwamba 

askari mmoja alitibiwa jana na kuruhusiwa huku mmoja akiwa amelazwa 

wodi ya majeruhi namba mbili akiendelea kupatiwa matibabu na hali
yake inaendelea vizuri.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...