George H.W Bush. ALIYEKUWA Rais wa 41 wa Marekani, George H.W Bush amekimbizwa katika hospitali ya Houston Methodist nchini Marekani baada ya kupatwa na tatizo la kupumua. Alipelekwa katika hospitali hiyo kwa gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) jana usiku.
Wawakilishi wa Bush wanasema kuwa hatua hiyo ya kupelekwa hospitali ni kama tahadhari. Bush mwenye umri wa miaka 90 alikuwa madarakani tangu mwaka 1989-1993 na ndiye Rais mzee kuwahi kuiongoza Marekani akimshinda Jimmy Carter kwa miezi michache. Alihudumu kwa muhula mmoja baada ya kushindwa na Rais Bill Clinton. Bush ambaye hawezi kutumia miguu yake, hivi karibu
0 comments:
Post a Comment