2014-12-04

HOSPITALI YA MISHENI YA SENGEREMA LAWAMANI KWA KUMUWEKEA DAMU ISIYO GROUP LAKE MTOTO WA MIAKA 5 NA KUSABABISHA KUPOOZA MWILI MZIMA.


Hospitali ya Misheni Wilayani Sengerema mkoani Mwanza imepata lawama kutokana na kitendo chake cha kumuongezea damu ambayo siyo kundi lake mtoto aliyeafahamika kwa jina la Salome Pastory mwenye umri wa miaka mine.

Taarifa hizo zimegundulika kufuatia baba wa mtoto huyo Edward Pastory kufika katika ofisi za Kijukuu Blog zilizopo Mjini Kahama kwa lengo la kuomba msaada wa kuwekwa mtandaoni ili apatiwe msaada.

Pastory alisema kuwa mtoto wake alianza kuugua mafua na kichwa na alipofikishwa katika hospitali ya mgodi wa Bulyanhulu iliyopo wilayani Kahama aliambiwa mtoto wake ana upungufu wa damu na maji.

Kufuatia majibu hayo Pastory akiwa na mke wake waliamliwa kwenda hospitali ya misheni iliyopo Wilayani Sengerema ili aweze kusaidiwa kuongezewa damu na kupatiwa matibabu makubwa.

Inadaiwa kuwa mtoto huyo ambaye alikuwa na damu ya Kundi 0 aliongezewa damu ya kundi A Hali iliyopelekea kupooza viungo vyake vyoye vya mwili ikiwa ni pamoja na kuacha kuona kabisa kwa miaka mitatu sasa.

Taaarifa za mtoto huyo kuchanganyiwa damu zilitolewa na daktari ambaye hakufahamika jina katika hospitali ya misheni ya Sengerema alipowaomba radhi wana familia wa mtoto huyo kuwa walipitiwa na kujikuta wamefanya kosa hilo na kuwaomba watafute damu ya kundi 0 ili wamuwekee tena mtoto huyo.




Baada ya tukio hilo mama wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Yulitha Jeremiah aliamua kukimbia na kumtelekeza mtoto huyo kwa baba yake hali iliyopelekea baba yake kumpeleka mwanaye kwa bibi yake Mereciana Malele aishie katika kijiji cha Kishimba mkoani Geita.

Kwa mujibu wa baba wa mtoto huyo baada ya kuona tatizo linakuwa sugu aliamua kumpeleka mwanaye katika hospitali ya rufaa ya Bugando ambapo aliambiwa atafute shilingi laki tano ili mtoto wake aweze kukaa,kusimama na kushika vitu huku akiambiwa macho yake yataendelea kutoona.

Kufuatia hali ya ufukara ya baba huyo aliamua kufika ofisi za mkuu wa wilaya ya Kahama na kuomba kuandikiwa barua maalumu ya kuomba msaada kwa wasamalimia wema.

Taarifa zilizopatikana kufuatia barua hiyo hivi sasa Edward amefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi laki moja na kwamba bado anahitaji laki nne ili kuweza kumsaidia mwanaye.

Kutokana na tatizo hilo Edward ameamua kuweka namba zake hapa 0764-769868 ili kwa yeyote atakayeguswa jambo hili aweze kumsaidia na kumpigia ili ampe habari kamili la tukio hili.

:

BABA WA MTOTO HUYO KULIA AKIWA NA MTOTO WAKE. 
 


AKICHEZA NA MTOTO WAKE



MWANDISHI NA MMILIKI WA KIJUKUU BLOG AKIWA AMEMBEBA MTOTO SALOME



HAPA AKIJARIBU KUMSIMAMISHA LAKINI ILIKUWA NGUMU SANA.



MTOTO SALOME AKIWA AMELALA HAWEZI KUKAA WALA KUSIMAMA..

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...