Mh. Zito Kabwe
Hatua hiyo ya PAC kuanza kulifanyia kazi inatokana na malalamiko ya wamiliki wa viwanda vya sukari yanayotolewa kutokana na soko la ndani kutekwa na sukari inayoingizwa kutoka nje ya nchi na wafanyabiashara wakubwa.
Wiki iliyopita, Bunge lilifikia maazimio ya kutaka mamlaka za uteuzi ziwachukulie hatua kwa mujibu wa sheria, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo na katibu mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema kutokana na kuhusika kwao kwenye sakata la uchotwaji wa fedha hizo kwenye akaunti ya escrow na kupokea fedha hizo.
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe anasema malalamiko na matatizo yaliyopo, watatumia kipindi cha mwezi huu na ujao kupitia suala la sukari kwa kuwa ni kubwa kuliko hata ufisadi uliojitokeza katika akaunti hiyo ya Tegeta Escrow.
“Hili suala la sukari ni kubwa kuliko hata la escrow kwani linagusa moja kwa moja maisha ya wananchi, wamiliki wa viwanda na uzalishaji na tayari tumeiita Bodi ya Sukari tujadiliane kwa kina kuhusu suala hili,” anasema Zitto. Wamiliki wa viwanda Mkurugenzi wa viwanda vya sukari vya Kagera na Mtibwa, Seif Seif anasema hasara ambayo taifa litapata kutokana na kufungwa kwa viwanda hivyo ni kubwa kuliko serikali inavyofikiria.
Anasema jambo hilo linatokana na sukari inayozalishwa nchini- kwenye viwanda vyote vinne vya Kilombero, TPC, Kagera na Mtibwa- kuwa ni tani 320,000 huku mahitaji yakiwa ni tani 420,000. Seif anasema kutokana na upungufu wa tani 100,000, walikubaliana na Serikali kwamba iwe inaagiza tani 100,000 ili kufidia upungufu huo, jambo ambalo linafanywa kinyume na makubaliano yao.
0 comments:
Post a Comment