2014-12-22

Kada awania ubunge kupitia Chadema ajing`oa CCM


Mapokezi ya Fransico Kimasa Shejamabu (mwenye gwanda) akielekea katika viwanja vya shule ya msingi Pambalu wilayani Sengerema kuhutubia wananchi. 

Aliyekuwa kada wa wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya Sengerema mkoani Mwanza Bw. Fransico Kimasa Shejamabu ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)ambacho amejiunga nacho. 
                      
             
Kauli hiyo ameitoa mjini hapa alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa wilaya Sengerema waliofika katika viwanja vya shule ya msingi Pambalu.

Alisema yeye si mwanachama tena wa CCM na kwamba amekihama chama hicho kutokana na kukosa mvuto kwa kutokana na viongozi wake kuhusishwa na mambo ya kifisadi .



 
                   
Bw. Shejamabu huku akishangiliwa aliwatangazia wananchi kuwa amekwisha weka nia ya kugombea ubunge jimbo la Sengerema kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivyo kuwaomba wanasengerema kumuunga mkono yeye na chama chake ili kiwaletee maendeleo jimboni humo.

Mwanachama mmoja wa CHADEMA Bw. James Ndahihya alisema wanamshukuru Mungu kwa kumuelekeza kada huyo wa CCM kujiunga na chama cha ukombozi wa watanzania kwani sasa jimbo la Sengerema limepata mgombea ubunge.

Bw. Shejamabu amesema ameingia Chadema kulikomboa jimbo la Sengerema .

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...