Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi NACTE limevifutia usajili Vyuo vya Ualimu 40 ambavyo vimeonekana kutokuwa na sifa na vigezo ya kujiendesha kielimu nchini.
Vyuo vilivyofutiwa ambavyo 39 vinamilikiwa na watu binasi na kimoja kinachosimamiwa na Serikali kilichopo Vikindu vimeonekana kutotekeleza masharti ya kuendana na mfumo wa ufundishaji wa somo la Hisabati.
Katibu Mtendaji wa NACTE Dokta Primus Nkwera amesema vyuo hivyo vimefutiwa usahili huo na kupewa muda wa mwezi mmoja wa kufanya marekebisho ya kujiendesha kielimu ili viweze kuendana na mfumo wa sasa wa Sera mpya ya Elimu ya mwaka 2014.
Nkwera amesema vigezo vya kuvifutia usahili vyuo hivyo vimetokana na baraza hilo kuendesha mfumo mpya wa kisasa wa kitaalamu ambao unatumika hivi sasa kuendana na sera mpya ya elimu nchini.
0 comments:
Post a Comment