2014-12-20

MDAHALO WA KATIBA WAFANYIKA LEO MWANZA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiwasili jioni ya leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini mwanza.

Umati wa watu waliojitokeza katika mdahalo wa Katiba katika Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini mwanza. Aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji msitaafu Joseph Sinde warioba amewahutubia wananchi jijini Mwanza kuhusiana na katiba inayopendekezwa na kuwashauri wananchi hao kuisoma kwa umakini kwanza kabla ya kuipigia kura kwani kuna baadhi ya vipengele vimentofolewa katika katiba hiyo.



Akizungumza katika mdahalo maalum ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika hotel ya Gold Crest Warioba amesema kuwa watanzania kwa pamoja wapige kura ya ndiyo kama yale waliyoyapendekeza yamo kwenye katiba na wapige kura ya hapana kutokana na kuwa yale waliyoya pendekeza hayapo katika katiba hiyo


GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...