JITIHADA za kuopoa miili kutoka katika Ndege ya AirAsia QZ8501 iliyoanguka baharini Jumapili iliyopita ikiwa na watu 162 zimeendelea kukwamishwa na hali mbaya ya hewa.
Ndege hiyo ilianguka katika Bahari ya Java nchini Indonesia na hali ya dhoruba katika eneo la uokoaji imezidi kukwamisha zoezi hilo.
Mamlaka nchini Indonesia yamethibisha kuwa mabaki yaliyoonekana majini eneo la Borneo ni ya ndege iliyopotea ya AirAsia.
Rais wa Indonesia, Joko Widodo, ameahidi kuendelea kufanya uchunguzi wa kina kwa kutumia meli na helkopta kuhakikisha miili ya watu waliokuwa kwenye ndege hiyo inapatikana.
Maombolezo ya pamoja yanatarajiwa kufanyika leo huko Surabaya nchini Indonesia na Gavana wa Jimbo la Java Mashariki, Soekarwo ameeleza kuwa sherehe zote za Mwaka Mpya zimesitishwa kutokana na ajali hiyo ya AirAsia.
0 comments:
Post a Comment