Wapenda amani nchini, wasomi, wanaharakati, wapinzani, viongozi wa dini, na hata watu wa kawaida wamepiga kelele nyingi sana juu ya utendaji mbovu na wa fitina wa Tume hii ya uchaguzi. Wengi wanajiuliza endapo hii tume ipo huru kweli au ni danganya toto tu?
Tume ya Uchaguzi nchini chini Mwenyekiti wake Jaji Mstaafu Damian Lubuva imeendelea kusuasua juu ya kuweka mazingira yaliyo huru na ya haki kwa vyama vyote ili kuweza kuwa na ushindani ulio sawa katika uchaguzi mkuu ujao.
Wapenda amani nchini, wasomi, wanaharakati, wapinzani, viongozi wa dini, na hata watu wa kawaida wamepiga kelele nyingi sana juu ya utendaji mbovu na wa fitina wa Tume hii ya uchaguzi. Wengi wanajiuliza endapo hii tume ipo huru kweli au ni danganya toto tu?
Jaji mstaafu Damian Lubuva ameendelea kujitetea kwamba yeye yupo huru katika utendaji wake lakini wananchi bado wana mashaka na tume anayoiongoza.
Waingereza wanasema “ matendo yanaongea kuliko maneno.” Ninasikitika kusema kwamba naona kama Mwenyekiti amewekwa “mfukoni” mwa viongozi wa CCM .
Tume ya uchaguzi inaonekana wazi kuwa “tawi “muhimu la CCM ili kuweza kuibeba katika chaguzi mbalimbali zitakazosimamiwa nayo.
Pamoja na ahadi zote za tume hii toka mwaka jana kuahidi itarekebisha sheria mbovu za uchaguzi, hali ya utendaji wake inazidi kuwa mbaya siku hata siku.
Wakati tunaelekea uchaguzi mkuu 2015 hadi leo inashangaza tume hii haijaanza kuweka mazingira yeyote ya kuwa na “tume huru’ ya uchaguzi nchini.
Nawaomba Watanzania wanaopenda amani ya nchi hii na demokrasia ya kweli lazima waanze kuishinikiza serikali ya CCM kuunda tume huru ya uchaguzi sasa bila kufanya hivi haitaundwa kamwe.
Tume huru ya uchaguzi itaratibu mambo yote ya uchaguzi likiwapo suala la daftari la wapiga kura na kuondoa malalamiko ya vyama vya upinzani na wananchi kwa ujumla.
Binafsi nimeshangazwa na kitendo cha CCM na Tume ya uchaguzi kupendekeza kwamba wanajeshi wa jeshi la wanananchi Tanzania (JWTZ) ati ndiyo watumike katika kusimamia uandikishwaji wa wapiga kura kisa ni nini? Je hayo si maandaizi ya kuhujumu uchaguzi ujao? Wapinzani kuweni makini na hatua hii.
Hatua hii binafsi naipinga kwa nguvu na akili zangu zote na ndiyo kwa maana naandika kwa uwazi kwamba “tume ya uchaguzi” kwa kuungana na Chama tawala, acheni kuhujumu demokrasia nchini kwa kutumia jeshi la wananchi (JWTZ).
Huu ni wakati wa kusema ukweli bila kuogopa mtu wala yeyote ili kulikomboa taifa letu. Kumbuka kuwa ukweli utatuweka huru.
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment